Kwanini kikao cha Bunge kinaanza Jumanne?

huko kwenu vipi

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
1,519
1,462
Habari wanajamvi...

Jaman samahani naombeni msaada kidogo kuna kaubishi hapa,

Swali: Kwann kikao cha Bunge kinaanza jumanne?

Kuna mtu hapa anasema jumamos wabunge watakuwa wanasafiri jumapili na jumatatu wanapunzika then jumanne wanaanza kikao rasmi je ni kweli anachokisema huyu bwana?
 
Ingekuwa live mubashara tungekuwa na majibu sahihi.
 
Kabla ya bunge kuanza kunakuwa na vikao mbalimbali na shughuli mbalimbali sasa inawezekana hivyo vikao na hizo shughuli zinaisha jumatatu kwahiyo ndiyo sababu ya bunge kuanza jumanne.
Nafikiri kijana wa Bavichaa utakuwa umeelewa.
 
Kabla ya bunge kuanza kunakuwa na vikao mbalimbali na shughuli mbalimbali sasa inawezekana hivyo vikao na hizo shughuli zinaisha jumatatu kwahiyo ndiyo sababu ya bunge kuanza jumanne.
Nafikiri kijana wa Bavichaa utakuwa umeelewa.

Asante sana,

Sasa hili bango la Bavicha limeingiaje hapa?
 
Hivi huu mradi wa chama chetu CCM wa eti kufifisha upinzani kwa kuzuia bunge mubashara (Live), yaani matangazo ya moja kwa moja na kuzuia mikutano ya kisiasa unatulipa? Binafsi naona huu mradi unakula kwetu. Hawa wapinzani wanazidi kupaa kuliko CCM. Wao wanafaidika zaidi kuliko sisi. Ona sasa upepo mbaya unavuma kuhusu mwenyekiti wetu wa Taifa. Tungeenda kwa wananchi tungejitathmini kuona wana hisia gani kuhusu chama chetu. tukisubiri 2020 tutakuwa tumechelewa sana! Ona sasa Tundu Lissu akina Tundu Lissu, Sumaye, waitara, Lowassa, Mtatiro, Seif, Mbowe ndo wanasikika kila kukicha huku wamebeba taswira ya vyama vyao. Kila siku tunasikia vikao vya ndani vya vyama vyao. yaani kwa upinzani vikao vya ndani vimekuwa na mshindo kuliko mkutano mkuu wa chama chetu. Tulikuwa tumebaki na JPM kama nembo ya kuuza chama chetu, lakini nembo hii imefubaa haraka kweli. Wananchi hawataki hata kumsikia. Amekusanya hela zote kwenye mzunguko na mitaani amezifungia benki kuu. watumishi wa umma hawapandishwi mishahara, madaraja wala vyeo. yaani wana hamu ya 2020 ili nao wamtumbue kwenye sanduku la kura. wanadai ni kutumbuana kwa zamu. Wanasema hata aje na push up nyingi kiasi gani hawampi kura tena maana hata wakimpa anawageuka na kusema hakuna aliyemsaidia kupata cheo alichonacho, eti amepata kwa nguvu zake mwenyewe. Na wale wajumbe wa NEC waliopunguzwa eti ni mzigo kwa chama nao wameahidi kutugeuka na 2020 wameahidi nao kumpunguzia kura. Nao wanasema ni kupunguzana kwa zamu. Mwee! Twafaaaaaaaaaaa!

Come 2020, come please! Labda sisi na chama chetu tutapata akili.
 
Kitulo: Kwa hiyo na wewe hujui ni kwa nini vikao vya bunge huanza Jumanne. Naona unasema "inawezekana...." Kwani hizo shughuli unazosema ni mwiko kuisha kabla ya Jumanne? Au hizo shughuli ni mwiko kuvuka Jumanne? Uje na sababu ya msingi na kama huna sema tu, kwa kweli na mimi sijui kwa nini bunge huanza Jumanne. Halafu kila swali lenye mantiki mnalihusisha na Bavicha. Hii ndio maana tunawahusisha Bavicha kama chimbuko la fikra na hoja za msingi. Maana ni kweli hata mimi tangu nianze kufuatilia shughuli za bunge miaka zaidi ya mitano iliyopita, vikao vya bunge vimekuwa vikianza Jumanne.
 
Siku nyingi nilikua najiuliza hilo swali, ngoja leo niangalie majibu
 
Asante sana,

Sasa hili bango la Bavicha limeingiaje hapa?
Halafu unamshukuru wakati hajakutajia no. na tawi lako la Bavicha lilipo.
Unajibu bila kujua huyo anakukebehi? Kila anayeulizia kitu kinachohusu hii nchi ni either Chadema au Bavicha. Nashangaa NCCR, CUF na vingine si upinzani? Hiyo ndo inakupa picha ni kwa jinsi gani chadema ni tishio.
 
jumatatu huwa ni siku ya registration ,kumbuka hata chuoni semester mpya ikianza hamuanzi masomo siku ya kwanza lazima kuwe na registration.so jtatu ndo ilitengwa kwa kazi hiyo
 
Back
Top Bottom