Kwanini Kenya wanalia mbona Uganda wamepigiwa mnada Ng'ombe 6000 hawalalakiki na Magufuli yupo Uganda saizi

Braza.. Huwezi kuvunja sheria za nchi jirani kwa kigezo cha Jumuiya.. haiwezekani na hicho hakijawahi tokea.. Tanzania sio shamba la bibi..
Siku ukisikia ugomvi kati ya wakulima na wafugaji wa nchi jirani mtakuja hapa kuiponda serikali kutosimamia sheria.

Narudia tena, huwezi kuvunja sheria za nchi jirani kwa kigezo kuwa mpo kwenye jumuiya.. hilo halipo mahali popote.
 
Ndo maana nakwambia. KUWAUZA sio SULUHISHO la tatizo. Mlimwambia Uhuru aongee na wananchi wake akashindwa kuwazuia?
Uhuru anakaa kimya. Kwa sababu mmeamua KUCHUKUA maamuzi wenyewe.
Mambo Kama haya ni ya viongozi kukaa chini. Kujadiliana. Cha kufanya.
Huu ndo ujirani mwema. Hii ndo Jumuiya inatakiwa iwe.
 
Kwa maelezo hayo inaonyesha dhahiri Kenya wanathamini watu wao, biashara zao mpaka na Mali zao.

Hongera sana na ndo maana wanatukimbiza karibia kila sekta
Dhamini kwanza sheria za nchi za watu huwezi kufanya mbinu za kihuni kupata kipato alafu usifiwe utasifiwa na wahuni wenzako
 
Museveni aliwahi kusema hadharani yeye sio mtumishi wa watu, anajipigania mwenyewe.

Unategemea kiongozi wa aina hiyo aumizwe na matatizo yanayowakumba watu wake?
 
Hahaha eti umemkosea yaani mtu akifuata sheria za nchi yake ni makosa? Niwape ushauri sababu mna akili finyu sana.

Nendeni mahakama ya Afrika Mashariki watawasikiliza
 
Braza.. hakunaga majadiliano kwenye suala la sheria nje ya mahakama, majadiliano yanakuwa mahakamani..

FYI Marais hawawezi kukaa chini kukubaliana suala la kisheria, wao hawako juu ya sheria.. zilitungwa na bunge sio wao na mtekelezaji ni mahakama.

Kipindi kile wahamiaji haramu kutoka Msumbiji walivyofukuzwa hukusikia Rais wa TZ amefanya majadiliano na Rais wa MZQ, walivunja sheria na ile ilikuwa stahili yao.

Na hata Rais alisisitiza, kuwa watendewe sawasawa na sheria za Msumbiji. Kwa sababu hakuna majadiliano kati ya marais linapokuja suala la utii wa sheria.

Hao waKenya walikuwa na nafasi ya kuja kununua mifugo yao kwenye mnada na kuirudisha kwao..

Sisi tunasimamia sheria zetu, kwa maslahi ya nchi yetu.. hapo huwa hakuna majadiliano.. ukitaka mjadala nenda mahakamani.
 
Sijakataa.
Tumefanya fanya mipango ya kujadiliana na wenzetu wa Kenya kuhusu ili tatizo?
Haya unasema tunafata sheria. Unakumbuka juzi tu. Nchi yetu imejitoa kwenye sheria ya kuendesha serikali kwa uwazi na uwajibikaji?
Lakini sheria ya kuuza mifugo ndo umeona ya kutekelezwa zaidi?
 
Ndo maana nikasema pale mwanzo.
ANGUKO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.
Tumeshindwa kujadiliana madogo
Makubwa hatutawezaa.
Ndo maana Jumuiya yenu IPO IPO..
Haina maendeleo wala Mipango.
SABABU YA UBINAFSI.
 
Irudishwe kwao.
Nimeuliza kuku wa jirani yako akiingia kwenye banda lako utamuuza au utamrudishia mwenyewe.?
Bawacha bana akili zenu zipo simple sana, hivi sio waziri Maghembe aliwataifisha ng'ombe zaidi ya 2000 waliovamia hifadhi?

Mbona hili povu hamkutoa kwa watanzania wenzenu umeolewa Kenya nini?
 
Kujitoa kwenye sheria yoyote ni kazi na jukumu letu, kama haina maslahi kwa nchi tuna uhuru huo.. zaidi sana hiyo sheria hatukutunga sisi, ilipopwaya tukaivua.

Hili tatizo la wafugaji wa Kenya kuingiza mifugo Tanzania halijaanza leo na wala sio tatizo la leo, huko nyuma tulimalizana kwa ujanja ujanja..

Kisheria hairuhusiwi kuingiza mifugo kwenye nchi jirani bila vibali.. full stop.

Sasa najiuliza hapa, kwa mfano una shamba lako pale mpakani unalima, halafu mtu wa nchi jirani akaingiza mifugo yake akala mazao yako, je utaenda kwenye mifumo ya sheria au mtamalizana?

Hiyo mifugo inasababisha uharibifu wa mazingira na vilevile inakula malisho ambayo ni halali ya wafugaji wa Tanzania.

Linapokuja suala la rasilimali zetu, je unafikiri ni halali kunufaisha majirani huku wa kwako wanateseka?

Nenda kaulize wafugaji wa Tanzania kama wanakubaliana na hilo swala?

Tumieni akili kidogo kwa mnachotetea..

Tukilegeza kwenye hili watakuja na kufanya mabaya zaidi..
 
yaani mkoloni katuwekea mipaka tumlindie ndo tunaitukuza kuliko kujenga mahusiano mema na jirani zetu ambao ni jamii moja na sisi, shame on us
Shame on yourself ardhi ni rasilimali kwa ujumla wake kama huoni hilo inawezekana ukiwa Rais wakenya wanaweza kuja kuchimba madini Tanzania na kuondoka nayo kisa upumbavu wa "mipaka ya kikoloni"
 
Bawacha bana akili zenu zipo simple sana, hivi sio waziri Maghembe aliwataifisha ng'ombe zaidi ya 2000 waliovamia hifadhi?

Mbona hili povu hamkutoa kwa watanzania wenzenu umeolewa Kenya nini?
Sawa. Ngoja wote tufuate sheria. Alafu tuone nini kitakachofatia.
 
Hizo sheria katunga Nani?
Na kuna sheria ngapi hamzitimizi?
 
Ndo maana nikasema pale mwanzo.
ANGUKO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.
Tumeshindwa kujadiliana madogo
Makubwa hatutawezaa.
Ndo maana Jumuiya yenu IPO IPO..
Haina maendeleo wala Mipango.
SABABU YA UBINAFSI.
Huwezi kwenda kufaidi rasilimali za nchi jirani kinyume cha sheria kwa kigezo cha kuwa kwenye jumuiya..

Ikiwa jumuiya inaruhusu uvunjifu wa sheria basi ni heri ikavunjika..

Jumuiya ya Afrika mashariki iliundwa kwa sheria maalumu.. na majadiliano yote yahusuyo jumuiya yatafanyika chini ya sheria.

So hakuna mahali ambapo kunasema kwa kuwa tupo kwenye jumuiya wananchi waruhusiwe kuvunja sheria halafu tujadiliane.. hamna kitu kama hicho.. unataka majadiliano unaenda mahakamani.

Na kama wanajumuiya hawaheshimu sheria za nchi zilizopo ndani ya jumuiya haina maana kwa jumuiya hiyo kuwepo..

Hapa sio suala la ubinafsi, tunalinda maslahi ya nchi yetu..

Malisho ya mifugo yaliyopo Tanzania ni kwa ajili ya watanzania tu..
 
Mleta mada ikitokea ukashikwa kalio alafu na rafiki yako naye akashikwa kalio na finger juu aka kaa kimya inamaana na wewe utakaa kimya sio?,inawezekana rafiki yako ndo michezo yake hyo kwahyo kakaa kimya sababu kafurahia
 
Sawa. Ngoja wote tufuate sheria. Alafu tuone nini kitakachofatia.
Acheni unafki kujiona mnazo akili sana kumbe zero tu, hiyo mifugo ingeingia kwenye mashamba ya watu na kuleta mauaji nyie mngekuja hapa kuishutumu serikali kuwa zembe, maliasili za taifa akili yako haizitambui yaani uko radhi hifadhi za taifa ziteketezwe tena na mifugo ya wakenya?

Sheria lazima ifuatwe huko kwao wanafuata sheria ndio maana polisi wa kenya walizipiga risasi zaidi ya ng'ombe 100 kwa kuingizwa kwenye shamba la mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…