Kwanini jamii inatudharau tulioacha shule?

Si asomee tu kozi za biashara vitabu aaa!Sina hakika kama atapata maarifa.
 
Usiogope usiogopex777 usiogope
Katika vitu ambavyo havihitaji kuomba ushauri
1.kuacha shule
2. Kuacha Mke/Mme
3. Kujinyonga
Elewa kwamba upo sahihi Kwa ulichokichagua
Siwezi kukaa kimya hapo namba tatu!.Upo ushahidi humuhumu JF watu walikuwa wako mbioni na wakaokolewa.
 
Ni kwel mkuu if your career depends on schooling you dont have a choice but only school,as for me that is very deffer what i need now is to put more effort to archieve my dreams its the right time now.
 
Kusoma shule siyo mpaka ukae darasani, ufundishwe na mwalimu na kufuata utaratibu wa taasis fulani. Watu wengi saana waliofanikiwa katika maisha hawakufuata mashinikizo ya watu wengine bali misimamo yao. Soma saana vitabu utapata mafanikio kuliko hata hao ambao wamefuata mfumo rasmi wa elimu.
 
Mimi naona uko sawa kabisa.Wakati mwingine akili inahitajia mambo mapya na unakuta huyapati darasani.

Hili ni funzo kwa walimu,serikali na wadau wa elimu kuboresha mazingira na namna za ufundishaji ili kumvutia mwanafunzi na kukidhi malengo yake.
 
Tatizo la elimu ya darasani haimfundishi mtu kutafuta SULUHISHO la matatizo bali inamlazimisha KUTOFANYA MAKOSA. Mtu mwenye akili ni yule anayepata A, lakini mtu huyohuyo ukimtoa nje anashindwa kupambana na maisha.

Kuna jamaa kamoja kana master's degree ya uchumi lakini nikimuuliza maswali mepesi tu anahangaika kutoa majibu utafikiri kaishia la saba.
 
kila MTU ana mlango wake wa mafanikio au kuendesha maisha yake n sawasawa na mapacha wanazaliwa Pa1 lakini kufa n tofauti

ushauri wangu : ulichokiamua Fanya kwa nguvu zako na kujituma, wekeza akili zako hapo, Toa sadaka, Fanya ibada jaribu kuwa mbunifu ktk hicho unachokifanya na kuwa makini sana Fanya akili yako ijue hapo ndo mafanikio yako yalipo, furahia hicho unachokifanya .....

.........God bless you......
 
Mkuu kwa hili sikuungi mkono hata kidogo, nachelea kusema shule ina mchango mkubwa sana katika maisha ya MTU yeyote.

Fanya research ndogo tu tena ya muda mfupi, kaa na mfanyabiashara msomi, sikiliza maono (focus) yake ya mbeleni, angalia capital alionayo kwa wakati huo, muulize alipoanzia na pia ni vipi ana-overcome challenges.

Pia mfuate mfanyabiashara mkubwa lakini hakusoma, muulize alipoanzia,vision yake na ni vipi ana-overcome challenges.

Naamini majibu utayapata. Kwasisi tunaofanya biashara na Wakinga, Wabena tunajua ukweli. Huezi mlinganisha Mchaga na Mkinga kibiashara.
Mkuu asante kwa ushauri lakini najua kuna elimu tofauti na shule.
 
Ha ha haaa. Wee jamaa dah. Umenifanya niamke. Ngoja niende tu kanisani sasa
Usiogope usiogopex777 usiogope
Katika vitu ambavyo havihitaji kuomba ushauri
1.kuacha shule
2. Kuacha Mke/Mme
3. Kujinyonga
Elewa kwamba upo sahihi Kwa ulichokichagua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…