Kwanini jamii inatudharau tulioacha shule?

Concord

Member
Joined
May 11, 2016
Posts
34
Reaction score
30
Wakuu,

Kwanza salamu ziwafikie,Mimi ni si mwenyeji humu JF nimekuwa nikitumia kama guest kwa muda kidogo.

Wakuu jambo linalonshangaza nimekuwa gumzo hapa mtaa kwetu baada ya kuamua kuachana na shule (secondary level) kwa kuwa sina mpango wa kuajiriwa na ni kama miaka sita au saba hadi kumaliza elimu yangu ukiangalia umri unaenda na nataka kuwa free na mishe zangu na skuli inabana sana muda.

So huku mtaa kila nikipita lecture hazishi mara oh utajutia, mara elimu haina mwisho n.k

Hivi wakuu kwanini hisia zetu zisiheshimiwe sisi tulioacha shule?
 
Elimu inamchango mkubwa sana hata katika maisha yako ya kila siku na si lazima uje kuajiriwa..Labda ukose hiyo fursa kwa bahati mbaya lakin kama kulikuwa na fursa ya kupiga book ukaacha tena katika ngazi ya Sekondary hata mimi nazidi kukushangaa kwa maamuzi hayo..
 
Unajishughulisha na nini kwa sasa?
 
Na kwann uache shule ndio mnao kuja kusumbua mtaani Mungu amekupa NEEMA ya kusoma kwa nn usisome? Kuna watu wana tafuta japo kubeba madaftari tuu..n hawapati eboo..
 
Mkuu asante kwa ushauri lakini najua kuna elimu tofauti na shule.
 
Mkuu asante kwa ushauri lakini najua kuna elimu tofauti na shule.
 
Siku zote akiangalia watu au kuwasikiliza mafanikio utasubir sana cha msing ni wakushauri then wewe mwenyewe ndo ujifanyie maamuzi yako binafsi
 
Mtu akiacha shule kibongobongo hapa olvl mi siamini mafanikio yyt juu yake hyo anajitaftia shida2 maana hata sklls ya kusoma kitabu na kukielewa atakua hana kwa hyo kijana nakushaur piga2 shule mwanang si wengn imetutoa japo sio sana ila tuna maisha yetu kifupi vijana tupende shule hakuna namna kwa Nchi zetu hz masikini
 
Hama mtaa! Ukienda mtaa mpya hakuna atakaye jua kuwa uliacha shule...
 
Kama mkuu alivyosema hapo juu. Kwa vile umeamua kufanya business, then hakuna shaka kuwa itakubidi utafute mbinu za kubobea katika hiyo kazi yako. Nasema hivyo ili ujipange vizuri uwe na business endelevu. Soma hivyo vitabu vya business, fuatilia watu waliofanikiwa katika biashara na usijaribu kufanya illegal business.
 
Mkuu ukitaka kujua umuhimu wa shule waulize matajiri ambao hawakusoma watakwambia, ila wanajuta sana kutokusoma na ndio wanaongoza kwa kuwa na uchungu juu ya elimu ya watoto wao.
 
Mkuu ukitaka kujua umuhimu wa shule waulize matajiri ambao hawakusoma watakwambia, ila wanajuta sana kutokusoma na ndio wanaongoza kwa kuwa na uchungu juu ya elimu ya watoto wao.
Mkuu nlichofata shule nshakipata na nimeshafanya utafiti juu ya hasara na faida ndo nimeamua hivyo.
 
Mkuu kuhusu hilo ucjali japo nmeacha shule ila sijaacha kutafuta elimu zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…