Habari yako dada Naureeen!Nataka nikwambie jambo ambalo litakusaidia,Mara nyingi sisi wanaume kabla hatujatongoza huwa tunatamani kwanza kulingana na muonekano wa nje wa mwanamke!na kwa kawaida mwanamke ameumbwa maringo kwanza, hakubali kirahisi hata siku moja! Wakati mwanaume anaendelea kumfuatilia demu anaongeza mapozi na kujifanya hataki mara aku-bomu hela, nitumie salio na vitu ka izo! Sasa siku anapokuja mwanaume kugundua mapungufu yake,historia yake anakuta mwanamke huyo ameshakuwa na mahusiano na zaidi ya wanaume 5 kama wewe mwenyewe ulivyosema! Ki-ukweli mwanamke anaweza kumtafuta mchawi kumbe tatizo ni la kwako mwenyewe! Mara nyingi wanaume tunakata tamaa baada ya kumfuatilia demu mda mrefu kumbe alikuwa anaku-ectia tu! Mf unamwambia naomba leo jioni tuonane ninamaongezi! Anakujibu usiku huwa sitoki! Wakati huo huo ww umeshagundua kuwa anaweza kutoka vizuri tu na pengine yeye mwenyewe anajichanganya jambo kumbe alivyokwambia mwanzo sivyo! Jaribuni kujichunguza ninyi wenyewe kabla hamjatupa lawama! wewe mwenyewe hebu fikiria umeachana na wanaume watano af wote wapo hivyo hivyo, hujiulizi? Wewe ndo unamatatizo unapaswa kubadilika dada! NB:hayo ni mawazo yangu you can have your own!