Kwanini iwe Nigeria kila Kitu? Why Is It Nigeria. Wamewezaje?

Yaani ndo kitu kingine nisichopenda kwa wanaigeria wako biased sana ukikuta kwenye Tuzo za Kinijeria wapo wasanii wengine wa Afrika atashinda mnijeria tu.

Afrimma na tuzo zao zingine zina upendeleo sana
Wako vizuri lazima washinde wanaojituma sasa kina Diamond wanawa copy utegemee washinde
 
Jamani hiki kitu kimenishangaza nimeamua kushare na ninyi mnisaidie. Afrika ina nchii huru zaidi ya 50. Ikiwemo Nigeria. Ila najua hatuwezi kulingana nchi zote au hatuwezi kuwa sawa Ila kwanini Nigeria kila kitu wapewe au wawe nacho wao?

Naanza kama ifuatavyo:

1.Uchumi Wa Nigeria na Ujumla wake
Inasemekana katika bara Afrika Nigeria ndiyo nchi yenye uchumi mkubwa kwa kuzingatia kigezo cha Per Capita Income na Gross Domestic Product (GDP). Lakini ukiacha hivyo ndiyo nchi yenye matajiri wengi akiwemo Aliko Dangote tajiri wa Afrika. Lakini hata kwenye population Nigeria ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wengi Afrika nzima .

2.Burudani na Michezo.
Tukija kwenye upande wa Burudani na Michezo hapa tutakesha.

Tuanze na upande wa filamu. Nigeria ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza filamu zake kwa wingi Afrika lakini pia ughaibuni. Wasanii wa filamu nchini humo wamejizolea umaarufu katika filamu Zao pendwa.Nikitolea mfano filamu ya "Aki na Ukwa" au "Aki na Pawpaw"

Filamu ni moja kati ya vitu vinavyochangia kwa sehemu kubwa mapato ya nchi hiyo. Wakiwa wamiliki wa Kampuni ya Nollywood ambayo ni Moja ya makampuni bora ya kutengeneza movie Duniani

Tugeukie kwenye muziki hapa ndio usiseme kabisa. Najua huwezi pita kwenye club au disco na ukatoka bila kusikia wimbo kutoka Nigeria. Wasanii wao ni wenye majina makubwa na wenye umaarufu sana barani Afrika.Kwa mfano P-Square, Burna Boy, Davido, Yemi Alade, Wizkid, Tiwa Savage na wengineo.

Staili nyingi za kucheza zinabuniwa na wanaigeria na kupendwa Afrika nzima. Mfano Azonto, Zanku, Shaku, Sankoro, Soko, Antenna, Akwaba, Ngororo. Wasanii wao wameipa heshima kubwa nchi yao kwa kuchangia asilimia kubwa kwenye ukuaji wa uchumi.

Lakini pia katika michezo Nigeria imewahi kutoa wachezaji mahiri katika mpira wa miguu akiwemo Jay Jay Okocha.
Timu yao ya Taifa imekuwa ikishiriki mashindano makubwa ya soka e.g Kombe LA Dunia, Afcon na mengineyo.

N.B: Inasemekana hata kwenye uchawi Nigeria ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa wachawi na waganga hodari Afrika.
Unakumbuka kauli ya raisi wetu
idadi kubwa ya watu ndio kigezo cha kufanya watu wengi kuzaliwa wenye vipaji vya ajabu vya kustaajabisha [NGUVU KAZI] NA USHAWISHI
chukulia nchi kama china na india

Naijeria inatabiriwa mwaka 2100 itakuwa na idadi ya watu milioni 750 na inategemewa ndio nchi itakayo kuwa na idadi ya vijana na chanzo kwa soko la nguvu kazi ajira duniani

ASANTE WANAWAKE WA KINAIJERIA MNAJUA SABABU YA MOLA KUWALETA DUNIANI
 
Mi wanaijeria nwmawakubali sana,wale jamaa kwa hapa afrika wana uwezo wa juu kiasi halafu ni fighters ile mbaya,ukienda kwao vijana hawarembi yan ni kazi tu mwanzo mwisho,hawana aibu sio kama sisi vijana wa kibongo ukimshikisha mtumba auze eti anaona noma...

Halafu ni miongoni mwa nchi chache africa zilizoruhusu kuchezwa kwa ponography( xxx)..ili kutengeneza ajira
 
elimu elimu elimu
hilo suala hapo juu wenzetu walilipata mapema sana na wakaweza kuitumia japo kwa uchache
 
Kila mtu na mtazamo wake jinsi anavoli perceive jambo, na kulipokea to me wako vizuri, to you hawako vizuri that's okay it's just a matter of opinions and not a league

Kuna ukweli na story mimi naongea nilichokiona sio wewe unatoa story ukizozisikia...
 
Kuna ukweli na story mimi naongea nilichokiona sio wewe unatoa story ukizozisikia...
Kila mtu na Jambo analolitazama kwa mtazamo waake that's all hayo ya kuona au kutokuona doesn't make sense it's a matter of perceptions na sio mashindano JF
 
Hakuna kitu kizuri kama Serikali ya nchi ikiitambua industry ya muziki na filamu kama chanzo cha mapato kisheria na kutoa ushirikiano katika shughuli zote za sanaa. Sisi hapa thamani ya wasanii inaonekana kwenye kampeni tu baaas ila shida zao, hakimiliki, mapato hivyo vitu hutasikia wakiongelea kabisa. Hata kuanzisha tuzo za kutoa appreciation kutoka kwa serikali inashindikana. Ila utasikia tu "Kesho Kuna Jambo".

Wenzetu wana access hata ya kutumia mahakama na jela kuigizia tu.

Hao jamaa isingekua ushirikiano wa serikali yao na wao basi wasingekua hapo walipo.

Wanaofuata ni bondeni kwa Madiba.
 
Naona kama film industry ya South africa ni advanced kuzidi ya Nigeria
 
Nigeria na eneo kubwa la West Africa wameanza kujanjaruka kitambo saaana, yaani kuna vitu sie tunafanya saivi wao walifanya 90's hukoo...East Africa haswa Tanzania Ushamba ni mwingi mnooo na ujuaji wenye Giza mbele.
 
Hakuna kitu kizuri kama Serikali ya nchi ikiitambua industry ya muziki na filamu kama chanzo cha mapato kisheria na kutoa ushirikiano katika shughuli zote za sanaa. Sisi hapa thamani ya wasanii inaonekana kwenye kampeni tu baaas ila shida zao, hakimiliki, mapato hivyo vitu hutasikia wakiongelea kabisa. Hata kuanzisha tuzo za kutoa appreciation kutoka kwa serikali inashindikana. Ila utasikia tu "Kesho Kuna Jambo".

Wenzetu wana access hata ya kutumia mahakama na jela kuigizia tu.

Hao jamaa isingekua ushirikiano wa serikali yao na wao basi wasingekua hapo walipo.

Wanaofuata ni bondeni kwa Madiba.
Ni hawahawa waliojazana huko kwenye makampen au kuna wengne?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom