zagarinojo
JF-Expert Member
- Jul 26, 2020
- 2,622
- 2,835
Jamani hiki kitu kimenishangaza nimeamua kushare na ninyi mnisaidie. Afrika ina nchii huru zaidi ya 50. Ikiwemo Nigeria. Ila najua hatuwezi kulingana nchi zote au hatuwezi kuwa sawa Ila kwanini Nigeria kila kitu wapewe au wawe nacho wao?
Naanza kama ifuatavyo:
1.Uchumi Wa Nigeria na Ujumla wake
Inasemekana katika bara Afrika Nigeria ndiyo nchi yenye uchumi mkubwa kwa kuzingatia kigezo cha Per Capita Income na Gross Domestic Product (GDP). Lakini ukiacha hivyo ndiyo nchi yenye matajiri wengi akiwemo Aliko Dangote tajiri wa Afrika. Lakini hata kwenye population Nigeria ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wengi Afrika nzima .
2.Burudani na Michezo.
Tukija kwenye upande wa Burudani na Michezo hapa tutakesha.
Tuanze na upande wa filamu. Nigeria ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza filamu zake kwa wingi Afrika lakini pia ughaibuni. Wasanii wa filamu nchini humo wamejizolea umaarufu katika filamu Zao pendwa.Nikitolea mfano filamu ya "Aki na Ukwa" au "Aki na Pawpaw"
Filamu ni moja kati ya vitu vinavyochangia kwa sehemu kubwa mapato ya nchi hiyo. Wakiwa wamiliki wa Kampuni ya Nollywood ambayo ni Moja ya makampuni bora ya kutengeneza movie Duniani
Tugeukie kwenye muziki hapa ndio usiseme kabisa. Najua huwezi pita kwenye club au disco na ukatoka bila kusikia wimbo kutoka Nigeria. Wasanii wao ni wenye majina makubwa na wenye umaarufu sana barani Afrika.Kwa mfano P-Square, Burna Boy, Davido, Yemi Alade, Wizkid, Tiwa Savage na wengineo.
Staili nyingi za kucheza zinabuniwa na wanaigeria na kupendwa Afrika nzima. Mfano Azonto, Zanku, Shaku, Sankoro, Soko, Antenna, Akwaba, Ngororo. Wasanii wao wameipa heshima kubwa nchi yao kwa kuchangia asilimia kubwa kwenye ukuaji wa uchumi.
Lakini pia katika michezo Nigeria imewahi kutoa wachezaji mahiri katika mpira wa miguu akiwemo Jay Jay Okocha.
Timu yao ya Taifa imekuwa ikishiriki mashindano makubwa ya soka e.g Kombe LA Dunia, Afcon na mengineyo.
N.B: Inasemekana hata kwenye uchawi Nigeria ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa wachawi na waganga hodari Afrika.