Kwanini ishindikane kwa kila Mtanzania kuwa na bima ya Afya NHIF?

Kwanini ishindikane kwa kila Mtanzania kuwa na bima ya Afya NHIF?

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
2,691
Reaction score
2,303
Kwa kweli sioni na hamna sababu kabisa ya watanzania kushindwa kuwa na bima ya afya kwa wote au kupata matibabu bure kama ilivyo Zanzibar.

Hili ni jambo la msingi sana na linaweza kuokoa maisha ya watanzania wengi ambao wanakufa kwa kukosa matibabu.

Kama imewezekana kwa watumishi kulipia bima ya afya kwa kukatwa kwenye mishahara yao kwa mwezi kwa lazima kwanini wananchi nao wasiruhisiwe kulipia bima hiyo kwa kuchangia kila mwezi kwa lazima?

Mambo mengine serikali ikiwemo kulipa kodi inaweza kulazimisha wananchi kulipa kwa lazima hadi kukamata akaunti zao za benki iweje hili lishindikane?
 
Hili suala haliwezekani ,watanzania wengi uwalazimishe watoe mfano laki Kwa lazima utafunga nusu nchi.

Serikali ifanye mpango wa kupunguza gharama za matibabu Kila mtu achague bima au cash.
 
Mama ana roho nzuri ila kwa ndugu zake wazanzibari nyie machogo pambaneni na hali yenu. Labda 2030 akipenda rostam, mkapata raisi chogo mzalendo kama nyerere au magufuli au mkapa, tofauti na hapo namba tunaisoma.
 
Yaaani kweli watu wanapewa mav8 na hela za kampeni wakati watu wanakufa,kweli?
 
Inawezekana kabisa huduma za afya kuwa bure na bora kuanzia zahanati mpaka muhimbili.
 
Niliwahi kupiga hesabu kua kama serikali ikiamua katika 1500 ya luku inayolipa Kodi ya jengo,watoe 500 tsh wapeleke kwenye bima,na watoe tozo kwenye miamala but kila muamala wakate tsh 50 kwa ajili ya Bima kwa wote,. INAWEZEKANA
 
Hao watumishi wanaokatwa kwa lazima huduma wanazopata huko hospitalinj kwa sasa ni utapeli mtupu.

JK aliiheshimisha sana hii NHIF tofauti na ilivyokuwa enzi za Mkapa tulikuwa tunaificha ili tulipie kuepuka kubaguliwa na watoa husuma hospilini.

Watumishi wanakopeshana michango ya wanachama bila riba ilhali kuna taasis maelfu za kutoa mikopo nchini,unategemea nini?

Hali ni ngumu mno mtaani mtu kumudu hivyo vifurushi ni heri afungwe akale na kutibiwa bure.
 
Binafsi baadala ya hiyo bima wanipe hela nijipambanie mwenyewe
 
Back
Top Bottom