Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Katika historia ya ulimwengu, tumeshuhudia matendo makuu yasiyoelezeka kwa akili ya kibinadamu, kama vile wagonjwa kupona, viwete kutembea, mabubu kuongea, vipofu kuona, wafu kufufuka, na bahari kugawanyika. Jambo la kushangaza ni kwamba, ishara hizi kubwa zimefanywa tu na watu wanaoiamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu. Kwanini?
Mifano ya haraka:
Musa, aliyeiamini Torati, aliigawanya Bahari ya Shamu (Kutoka 14:21).
Elia, nabii wa Mungu, alileta moto kutoka mbinguni (1 Wafalme 18:38).
Mitume, waliohubiri Injili, walifanya ishara nyingi: Petro alimponya kiwete, Paulo alimfufua Eutiko (Matendo 3:6-8; 20:9-12).
Labda utasema hiyo miujiza ilifanywa zamani. Siku hizi hakuna miujiza! Mimi sio wa zamani. Sawasawa na andiko la Yohana 14:12, nimeshuhudia miujiza mikubwa maishani mwangu...
Nimepona makumi ya magonjwa kwa kuweka mkono tu sehemu inayouma na kukemea kwa Jina la Yesu. Mara nyingi, nimeyafukuza mapepo yaliyokuja kunishambulia.
Kwa Jina la Yesu, 'nimewapiga stop', si mara moja, majambazi waliojaribu kunidhuru, nk, nk, nk
Mambo haya mazito siyasikii au kuyaona nje ya watu wanaoiamini Biblia na Yesu mtenda miujiza. Kwanini?
Kama huo sio ushahidi kwamba Biblia ni Neno la Mungu, nitajie sababu yako wewe... Kwanini ishara, maajabu na miujiza mikubwa inafanywa na watu wanaoiamini Biblia tu?