Kwanini hujihusishi na Siasa?

Kwanini hujihusishi na Siasa?

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
289
Reaction score
489
"Siasa ni mfumo ambao baadhi ya watu huwatawala wengine," nukuu iliyo kwenye kitabu cha mwandishi kutoka nchini Canada, Glenn Tinder.

Katika maandishi yake Tinder anasema, kisiasa kila mtu ni sawa ingawaje kiuhalisia katika nchi nyingi duniani ikiwemo Canada ushawishi wa kisiasa hauna usawa.

Anaendelea kubainisha kuwa wenye mali na uchumi mzuri wanaonekana kuwa na sauti na kuwa na haki katika kufanya maamuzi.

Familia, jamii na vyombo vya habari vinatajwa kuwa vichocheo muhimu kuelekea hamasa ya uelewa wa watu kuhusu siasa.

Licha ya changamoto zilizopo katika mfumo wa siasa duniani, kuonekana wa kibaguzi hasa wakati wa kufanya maamuzi bado kuna umuhimu mkubwa wa watu kushiriki katika siasa katika maeneo yao ili kukuza ustawi wa jamii.

Tinder anamaliza kwa kusema siasa haihusishi madaraka tu kama watu wengi wanavyoamini bali inajumuisha masuala mengine muhimu kama maamuzi, mifumo ya elimu, haki jamii na maendeleo kiujumla.

Picha kwa hisani ya Rose Mayemba
Photo_1679335540596.jpg
 
siasa haihusishi madaraka tu kama watu wengi wanavyoamini bali inajumuisha masuala mengine muhimu Kama maamuzi, mifumo ya elimu, haki jamii na maendeleo kiujumla.
Siasa ni kila kitu katika maisha. Na ilianza tangu kale. Tofauti na zama za leo ni namna baadhi ya wanasiasa wanavyogeuza siasa kuwa mchezo mchafu.
 
Politics is who get what when and how-conversinal wisdom,Aristotle "affairs of state" na lasswell anasema "authoritative allocation of value"

Politics is all about social, political and ecenomical in broader sense kwamba siasa ni itikadi na mfumo wa maisha ya kila mtu..je unajua dini ni siasa??

Uislamu
Kristo
Budhha

Zote ni itikadi na pia siasa hivyo siasa ni maisha yanayoishi why useme sijihusishi na siasa?
 
Dini sio siasa
 
Back
Top Bottom