Kwanini hizi ndio albums bora kwa muda wote?

Kwanini hizi ndio albums bora kwa muda wote?

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,664
Reaction score
8,285
Huu ni Kwa Mujibu wa Watu wa Industry Ya Music

- Impacts, album ya Prof Jay na Afande Sele ukiachana kuwa na mawe mazito pia zilileta ushawishi mkubwa kwenye Bongo Flava.

Kwa miaka hiyo Dansi na Taarabu zilikua juu, huku Bongo Flava ukionekana kama muziki wa kihuni.

Lakini baada ya hizo projects mbili ukurasa mpya ulianza, unaweza kuona ni kitu rahisi lakini hakuna kitu kigumu kwenye maisha kama kuhamisha mindsets za watu au kuunda new era.

Biashara, kama tungekuwa tuna utaratibu mzuri wa kutunza data basi naamini album ya Ng'e ya Ngwair ndio ingekuwa album iliyouza zaidi kwa muda wote.

Na Kwa kipindi hicho inasemekana iliuza mnoo, lakini data ziko wapi? Shida ipo hapo ila hata mimi naamini iliuza kweli sababu almost ngoma zote zilikua ni hit songs.

Kingine cha utofauti, hiyo album ndio ilileta mabadililo makubwa kwenye Rap na game nzima kwa ujumla upande wa biashara.

Kitu ambacho huko nyuma hakikua hivyo maana game ilikuwa inafanyika kwa mahaba zaidi na harakati.

Content, albums nyingi kwa kipindi hicho zilikua na content zilizoshiba lakini project ya Jay Mo ina kitu cha utofauti kidogo.

Ukiachana na content Mo' delivery na ubunifu ulikua mkubwa sana, unavyoiona delivery ya Dizasta Vina na ubunifu wa stories basi ndio Mo' kipindi hicho.

Ukiachana na yote lakini bado haikufanya vyema sokoni, kwa mujibu wake.

Mo' anasema albums zake hazikuuza kihivyo japo zilileta impact kubwa as Jay Mo lakini sio Cash kama ilivyokuwa kwa wasanii wengine chini ya Lebo ya Bongo Records.

Kitu kingine kuhusu hiyo album, ilikuwa na mawe mazito tena hit songs za kutosha lakini album bado ilikuwa underrated.

[emoji1241][emoji1241][emoji1241][emoji1241]⁩ nk nk
FB_IMG_1663199016813.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom