Kwanini hatuna mijadala/debate za wazi?

Kwanini hatuna mijadala/debate za wazi?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,293
Reaction score
13,958
Tanzania tumekuwa nchi ambayo mijadala ya kimaendeleo inafanyika kwenye mitandao tu.

Je tunaogopa nini? Hii mijadala sio ya kisiasa pekee inawezekana mijadala ya mfumo bora wa elimu ya sekondari kwa kizazi hiki, mijadala ya sheria bora na ardhi yetu, mijadala ya ajira.

Uzuri wa demokrasia ni mijadala ya kimaendeleo. Tumekuwa tukibishana sana kwenye makutano, bar, vijiweni na kwenye mitandao lakini sijaona mabishano na mijadala ya wazi ukiacha wakati ule wa katiba mpya popote.

Waandishi wa habari niwape tu mawazo.

Anzisheni kipindi cha TV cha mahojiano mfano unaweza kusema unaalika watu wawili halafu kwa saa moja, unawahoji kama wenyewe wangekuwa na madaraka wangefanya nini kusadia nchi.

Yaani viongozi wanachaguliwa bila hata kujua wenyewe watafanya nini imekuwa ni chama tu!
 
..kabla ya Obama kuchaguliwa kuwa mgombea wa democrats alishiriki na wagombea wenzake ktk midahalo isiyopungua mitatu.

..pia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wagombea Uraisi na Makamu Uraisi wa Marekani hufanya midahalo baina yao.
 
..Tangu mwaka 1995 hatujawahi kuwa na mdahalo wa wagombea Uraisi.
 
Itv huwa kuna mjadala mzuri sana

Wakati wa Kikwete vituo vya TV ikiwemo hiyo ITV walikuwa na mijadala mizito tena iliyo balanced. Ila baada ya kuingia Magufuli hakuna mijadala huru bali iliyojaa hofu na kusifia tu. Na hata kama itakuwa ina ukali basi ni ya kuwakashifu wapinzani. Tumerudi nyuma kisa rais tu hawezi kuvumilia hoja kinzani. Hivyo tatizo hasa la mijadala huru ni udhaifu binafsi wa rais.
 
..Tangu mwaka 1995 hatujawahi kuwa na mdahalo wa wagombea Uraisi.

Hapana Mkuu, 2010 pia kulikuwa na mdahalo wa urais japo mgombea wa ccm ambaye ni Kikwete alikimbia mdahalo wa wagombea kwa pamoja na kuwa na mdahalo wake binafsi uliokuwa funika kombe. Hata 2015 haukuwepo maana wagombea wa ccm huwa hawapendi midahalo ama hawawezi. Kumbuka uchaguzi wa 2015 ulikuwa ni wa wagombea wawili wa ccm baina ya Magufuli na Lowassa, hawa wote hawawezi midahalo.
 
Yani unakuta kuna Kamanda lissu na Magu mjadala huo hata ufanyike usiku wa manane nipo macho nasema
 
Back
Top Bottom