Dude lao
Nakushangaa mkuu, kama kweli hauoni umuhimu wa vizazi kuelezwa au kufundishwa kuhusu ukweli wa yaliojiri. Na pengine nikurekebishe ulipoteleza, hapo nikimaanisha jaribio la kupinduliwa kwa serikali ya Mwl. Nyerere, tena mara tatu katika miaka tofauti tofauti.
Asante
Alexism. Haya ndio mambo niyapendayo mkuu, napenda sana kufunyua ukweli uliofichwa.
Dude lao
Japo historia haisemi wazi juu ya mambo mengi sana Tanganyika na Tanzania ya leo, lakini Mwalimu Nyerere tangu awe kiongozi wa nchi hii amenusurika mapinduzi MATATU.
Moja ni la mwaka 1964, la pili ni la mwaka 1970 na la mwisho ni la mwaka 1982.
Jaribio la kwanza ndilo lilipelekea kuundwa kwa JWTZ na lilizimwa kwa msaada wa Malkia wa Uingereza aliyetuma makomandoo maalumu na wakafanikiwa. Jaribio la pili ndilo lililopelekea kuundwa kwa usalama wa Taifa na kikosi maalumu cha ulinzi wa rais. Na jaribio la mwisho ndio lilipelekea kubadili sera ya usalama wa Taifa kwa kuwapandikiza kila kwenye sekta na kuwa kila mtu ni mlinzi wa nchi hii (usalama)
Leo nitazungumzia jaribio/ uasi wa 20 Januari 1964 na nini hasa ilikuwa chanzo cha uasi ule:
Kuasi kule kwa wanajeshi Januari 20 1964 (Tanganyika Rifles) wala sio jambo la zamani sana kiasi cha kusema kwamba historia ile imetupwa na hakuna anayesema ukweli, nilikuwa nahisi viongozi kama Mwalimu, Kawawa na Kambona wangeyaweka katika maandishi mambo yale muhimu katika historia ya nchi yetu kabla hawajatutoka. Hakuna mahali mambo haya yameandikwa na ndio maana vijana wanaotaka kujua historia ya nchi yao wanakuja na hizi hearsay.
Askari wale wa Tanganyika Rifles waliasi... Miongoni mwa mambo waliyokuwa wanadai ni hali nzuri ya maisha ya askari Mtanganyika, mshahara ulikuwa mdogo, hawakupandishwa vyeo na hakukuwa na Watanganyika katika vyeo vya juu ndani ya Jeshi lile.
Askari waliasi na kuingia mjini, na wengine walikwenda kwenye makazi ya maafisa wa Kiingereza (raia) na kuwashikilia. Waziri wa ulinzi wakati huo alikuwa Oscar Kambona. Mwalimu na Mzee Kawawa kwa usalama wao walitoroshwa na kwenda kujificha. Inasemekana maficho yao yalikuwa Kigamboni. Waziri wa ulinzi (Kambona) alijaribu kupita katika barracks na kuwaomba askari watulie bila mafanikio.
Hali ile iliendelea kuwa mbaya na Mwalimu kwa ushauri wa Kambona na Kawawa akaomba msaada kwa Uingereza ili waje waokoe hali ile ambayo ilikuwa inaelekea kuwa mbaya,kufuatia kuasi kwa askari wetu, askari wa Kenya na Uganda nao waliasi kwa sababu sawa kabisa na za uasi wa Tanganyika Rifles.
Malkia alituma kikosi maalumu cha askari wa Uingereza ambao walikuwepo katika ghuba ya Aden, askari hao walikuja na meli kubwa ya kivita HMS Centaur ambayo ilikuwa na makomandoo (45 RM),askari na helikopta. Walifanikiwa kutuliza maasi yale, na Mwalimu na Kawawa wakatoka mafichoni na kuonekana hadharani wakiwa na waziri wa ulinzi, ambaye alifanya kazi kubwa bila mafanikio kuwaomba askari (Waliokuwa wananuheshimu sana) waache uasi na madai yao yatafanyiwa kazi.