CosaNostra
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 382
- 139
casaNostra, nivema ungeweka hayo uyasemayo kwa ujazo ili nami nipate kujifunza kutoka kwa yale utakayo yaleta jamvini.
Ingependeza zaidi iwapo utatufafanulia hicho unacho mipango ya kuangusha serikali 1983 kama unalivyo ahinisha.
Jaribio/ Njama/ Uasi wa Jeshi, yote hayo yalimlenga Mwalimu.
Na sitaki kuamini kwamba haya yalitokea pasipo sababu, na hapa ndipo napata kuamini kwamba Jk ndie aliekua sababu mpaka kupelekea haya kutokea.
Kingine naona ume mention matukio haya mwaka 1983 na 1964. Je, hapakuwahi tokea tukio kama hilo au lakufanana na hayo katika wakati tofauti na 1983, 1964?
Nikirudi kwenye lengo kuu la kuleta Uzi huu hapa ni:-
Kwanini matukio haya hayakuwekwa kwenye vitabu vya historia?
Kwanini hatukufundishwa mashuleni walau tupate kujua yalio tokea kwenye historia ya nchi yetu?
Kwanini kama sio kweli serikali haujawahi kukanusha?
Kwanini matukio haya yalifichwa?
Mambo mengi ya kudhalilisha taifa huwa hayafundishwi popote pale, iwe marekani, Ulaya au wapi. chukua mfano wa vita ya ndani ya marekani, inafundishwaga? Tazama Biafra Nigeria, inafundishwa? hapa Kenya tu kina Ochuka (marehemu) walipofanya jaribio kumpindua Moi yanasemwa? jifunze hayo!! Mambo kama hayo ni wewe kutafuta mwenyewe, si kuwekwa katika silabasi. Mbona vitabu vinavyoelezea vipo? Kumbuka kesi ya uhaini ilikuwa ikichapishwa gazetini miaka ya 80s. Pia vitabu kama KwaHeri Ukoloni, Kwa Heri Uhuru cha Harith Ghassany vinaelezea kasoro za watawala wetu n.k.
Shida ni kuwa hatutafuti habari, zipo hotuba kibao za Nyerere kuhusu hayo. Hata mitandaoni taarifa mbona zipo?
Ebu soma ndugu yangu, tafuta habari, rejea hotuba za Mwl.
Kumbuka mwaka 1964 sababu ilikuwa wanajeshi kudai Uafrika uwekwe haraka jeshini sio kuendelea na maofisa wazungu.
Mwaka 1983 hali mbaya ya uchumi, na kwa mujibu wa NY Times baadhi ya Wahaya waliungana na wengine kula njama ya kuangusha serikali. Pia wakati huo kulikuwa na mapinduzi ktk nchi nyingi tu za Afrika.