Kwanini hakuna Zoo ya kufuga Nyati?

Rufiji dam

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2020
Posts
4,449
Reaction score
10,761
Ukiwa Tabora kuna ZOO kama unaenda National kuna kila aina ya wanyama lakini huyu mwamba hayupo.

Kule sijui Arusha kuna shamba la kufuga wanyama na watu wanacheza mpaka na Simba, lakini hili dume Nyati halipo.

Nini shida mpaka huyu mtemi anaogopwa kufugwa.
 
Huyu Mwamba ni ng'ombe aliyechangamka. Hana lolote. Ni kitoweo tu kwa simba.
 
Nadhani kutunza jamaa yako ni kazi kweli kweli kiasi cha kuweza kutumia kuliko anachoweza kuzalisha. Si huyo tu. Iko wapi zoo ya twiga, tembo au fisi?
 
India Nyati wanafugwa kama ng'ombe tu na wafugaji wa kawaida tu vijijiji na huwatumia kulima mashambani na kukokota mikokoteni ya mizigo

Waweza pishana nao kibao wakichungwa na kijana mdogo tu kupelekwa malishoni

India hata tembo wanafugwa majumbani vijijini na hutumika kwa kazi mbalimbali za kilimo na kubeba mizigo na hata kuwatumia kama punda .mtu anapanda tembo anaenda aendako
 
Kwa hio nyati wa Serengeti ni species hio hio iliyoko kwa kanjibai?

brother una Jina Kubwa ila sasa dah...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…