Kwanini hakuna picha ya mwanamke katika noti, Kuna siri gani?

Kwanini hakuna picha ya mwanamke katika noti, Kuna siri gani?

Afro-Arabica

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,107
Reaction score
493
Tuulizane vipi noti za nchi nyingi kuna picha za wanaume tu! Vipi hakuna picha za wanawake maarufu au mashuja?!

Tafadhali mwenye kulielewa hili atujuze.
AAbY5nz.img

Wanataka kuweka mwanamke kwenye dola mpya ya kumi

Proposal ni kumweka mwanamke mweusi ambaye aliweza kuwatorosha weusi wengi wa kusini marekani na kuwapeleka kaskazini kwenye uhuru (nimemsahau jina - Harriet Tubman?)

Ama kwa British Pounds za denomination zote zina picha ya Malkia. Na Waingereza walikataa kujiunga na Euro kwa sababu walitaka lazima moja ya noti iwe na picha ya Malkia na mataifa mengine yalikataa.
 
sisi TZ jee....? tuweke picha !!!
 
Zipo mkuu, ila ni chache!

Mfumo kandamizi kwa mwanamke ndio umesababisha haya... Fikiria hata nafasi ya mwanamke kwenye dini zenu za kuiga. Ukristoni kuna Mungu Baba, ambaye ana mtoto wa kiume kisha kuna Roho mtakatifu ambae hana jinsia, huoni nafasi ya mwanamke ilivyouwawa hapo?

Kwenye Uislamu hawajadili sana ya jinsia ya Mungu na miungu, lakini wanaume wameahidiwa mabikira 72 watakapofika peponi, ila wanawake hawajaahidiwa chochote cha kufanana na hicho.

Pengine kosa lilianza kwenye jamii, lakini dini za kulazimishiwa ndio zikahalalisha mwanamke kuwa katika nafasi aliyonayo sasa hivi.

Hadi pale mtazamo wa jamii kuhusu wanawake utakapobadilika utaona mengi ya kushangaza.

Wasalaam!
 
Utaratibu ulizoeleka ni kuweka picha za wakuu wa nchi, ila tunaweza kubadilisha ikawekwa hata yako kwani nini bana! Kama vipi anzisha kampeni ya kuweka picha ya wanawake kwenye noti.
wapo Mashuja wakike wengi.. wapo walio shiriki ktk kuleta mapinduzi,maendeleo,nk,nk...!!
 
Ha ha ha

Hivi kuna mwanamke mkuu wa majeshi duniani hapa ?
 
Back
Top Bottom