Wanabodi,
Naomba kwa mwenye taarifa, kwa nini gharama za ulipiaji wa DSTV zimepanda ghafla tena kwa gharama kubwa?Kifurushi kilichokuwa 17,000 kwa sasa ni 23,500, kilichokuwa 34,000 kwa sasa ni 51,000 na kilichokuwa 56000 kwa sasa ni 84000 hadi 147000 ukiongeza Supersport 3 na 7. Tatizo ni nini? Wameleta mitambo mipya?
Mwenye taarifa, naombeni nijue.
Ambazo kama rand 14 ni sawa na US dollar 1, ina maana huku Tz twatakiwa tulipe Tshs.55000 kama 1US dollar ni Tshs 2200.Wanatuibia sana kama kura za.........
Mkuu sasa hiv DSTV premium unalipia 219,000, kutoka 199,000, 168,000, 147,000... Hizo gharama zilipanda ndani ya mwaka mmoja.. Kwa kweli Serikali iingilie kati.... hapa naona kuna watu wachache wanafaidi hela za watanzania...hasa wale top management...but hawa wachin wanalipwa kama matella wa bank...Mkuu mbona na wao rand haipo stable kwa dollar ilikua rand 7 kwa dollar moja ss ni rand 14 kwa dollar moja iyo rate ya leo..inakuaje South Africa malipo ni kidogo sana na ni nchi ambayo watu wanajiweza huku kwa masikini malipo mpaka laki na themanini kwa mwezi ? Na pia channel south zipo nyingi zaid kuriko huku tunakolipa ghali zaidi..huku imekua ni starehe wakati jozi sio starehe kwa kuwa wengi wanamudu kulipa dstv..
Katili mkapa anatuumiza pale.Mkuu sasa hiv DSTV premium unalipia 219,000, kutoka 199,000, 168,000, 147,000... Hizo gharama zilipanda ndani ya mwaka mmoja.. Kwa kweli Serikali iingilie kati.... hapa naona kuna watu wachache wanafaidi hela za watanzania...hasa wale top management...but hawa wachin wanalipwa kama matella wa bank...
Mambo yote ni bain sport kwanza ipo inaonekana kria, supersport wanajidai ni HD ila muonekano wao wala sio bora, na mabei yao rukuki.
Mnaotumia azam mngeweka bei za vifurushi ili watu wafanye maamuzi magumu. Na mnaotumia digitek mngethibitisha kama kweli hakuna malipo ya mwezi muone kama watu hawatasema Suu. Raha ya dstv kifurushi kiwe premium sasa kwa jinsi thamani ya shilingi ilivyo dola 100 kwa decorder sio wengi watakaoweza
Azam TV wako poa sana. Vifurushi vyao ni Azam Pure 24+ channels 12,000/= @ mwezi;, Azam Pure 50+ channels 20,000/- @ mwezi; Azam Play 80+ channels 25,000/- @ mwezi, na unaweza kuongezea Azam Sports channel 4: [1] Azam Sports HD, [2] Manchester United TV, [3] Liverpool FC TV na [4] Real Madrid TV) 15,000/-. Kama huja renew kifurushi, local channels utaendelea kuangalia free of charge!!
Samahani kama nimekosea naomba Azam au wanaojua zaidi wanisahihishe!