Powder
JF-Expert Member
- Jan 6, 2016
- 4,807
- 6,302
Mbona UKAWA wakifanya mambo yao kuna watu wanapata shida sana? Kama UKAWA wamesusa kila bunge likiendeshwa na Tulia, kwanini Tulia anapata shida? Kwanini asiendelee na vikao vya bunge kama kawaida? Akawaacha UKAWA wafanye yao na yeye afanye yake?
Majuzi wabunge wa CCM wakiomba miongozo kuhusu ama bunge kuwaadhibu Wabunge wanaosusa iwe kusimamishwa au kutolipwa posho, majibu ya Dr. Tulia yalisema hakuna kanuni ya bunge ilovunjwa, japo jana akaja na nyingine kuwa ameamua kuzuia posho kwa kucheki maamuzi ya Ma Spika walopita, (Inaonekana alikua anahangaika kutafuta hii) Ni nini hasa kinampa wakati mgumu mpaka kutangaza kuondoa posho za 300,000 za kikao?
Kwa posho ambazo wabunge wengi wa UKAWA wanataka zisiwepo,mbunge ambaye anapata zaidi ya Mil. 11 kwa mwezi, pesa ya mfuko wa jimbo, mikopo Bank na miradi mbalimbali, Posho ya Laki 3 kwa siku inaweza kubadilisha uamuzi wa UKAWA? Kwanini Tulia anapata shida na UKAWA kumsusia Bunge? Kwanini asiendelee na Bunge bila uwepo wa UKAWA? Kama akidi Bungeni inatosha, mijadala inaweza kuendelea, kwanini Dr. Tulia anahangaika na UKAWA kwanini asifunge vioo akaendelea kuendesha bunge?