Kwanini Dr. Slaa anawasifia polisi?

Naounga mkono hoja. Dr ni mtu makini sana. naomba atuongoze japo miaka mitano wakati anasindikiza uzee wake ili aache amewafunga wezi wa mali zetu. daima tutamkumbuka kwa kuingoza nchi akiwa nje ya ikulu. hata pinda amekili kuwa hapati usingizi sababu ya CHADEMA anayoiongza DR. Heko Dr Slaa Baba mdogo wa Taifa letu.
 
Kwa mtu ambae una ndugu yako polisi unaweza kuelewa nini anachomaanisha Dr. Slaa

Polisi ni wafuata order na unapokuwa nao sehemu tofauti na "order" utawagundua ni binadamu sawia na wenye kuumia pale wanapolazimika kutekeleza order

Kwa taarifa nilizonazo kwa watu Arusha, wako Polisi wengine ambao waliwasaidia vijana wengi tu wa CHADEMA "kutokea" kwenye njia na pande ambazo hawawezi kukutana na polisi ambao wako chini ya "makamanda watoa order"
Ni kweli Police nao ni binadamu,wanamoyo ilio hai kama wa kiumbe kingine chochote.Wanafanya hayo kwa kutekeleza order za wakubwa wachache wenye maslahi binafsi na kujipendekeza Rais ili wateuliwe kwenye position za juu.Kumbuka aliyofanyiwa A.Mrema kule Kilimanjaro na maeneo mengine.
 
Dr. Slaa, ni mtu mstaarabu na mtu wa haki. Kutokana na picha zilizoonenkana kwenye TV juzi, wakati anashuka kutoka kenye lori la polisi akipelekwa mahakamani kufunguliwa mashitaka, niliona askari akimsaidia kushuka kutoka kwenye lori. Nilimuona yule polisi alionyesha adabu na kukiri tofauti za umri wao.

Hata juzi kwenye mtadao huu kuna watu waliotoa ushuhuda wakusaidiwa na polisi wasikamatwe! Nao wameonyesha kushangaa utu wa askari wetu. Ukweli ni kwamba nao ni watanzania na wapata maumivu kama tunayoyapata watanzania wengine, kwa nini wasibadilike?
Ningemshangaa Dr. Slaa kama asinge tambua utu wa askari wetu.
 
Acha justification zako za kitoto katika mambo serious. Huwezi kukusanyika NMC kuilazimisha mahakama kumuachia huru mtuhumiwa aliyekataa dhamana yeye mwenyewe. Hata kama Lema alikubali kutoka nje kwa dhamana, mahakama zina mamlaka zake na mamlaka hizo haziwezi kuvurugwa na mikusanyiko na mikesha ya NMC. Na wala mkusanyiko huo haukuwa na lengo hilo la longitudinal research unayoizungumzia wewe.

kifupi ni kuwa huwezi kuyaona hayo. Siasa sio sheria ndugu
 
Naounga mkono hoja. Dr ni mtu makini sana. naomba atuongoze japo miaka mitano wakati anasindikiza uzee wake ili aache amewafunga wezi wa mali zetu. daima tutamkumbuka kwa kuingoza nchi akiwa nje ya ikulu. hata pinda amekili kuwa hapati usingizi sababu ya CHADEMA anayoiongza DR. Heko Dr Slaa Baba mdogo wa Taifa letu.

umenena,naunga mkono hoja.mwenye kutaka mwongozo akuone.
 
Hawa Polisi wadogo nao ni watanzania jamani, unafikiri wanfurahia kupiga watu? Lakini tatizo ni nidhamu ya kijeshi ndiyo inayowaponza. Ukiambiwa piga unatakiwa kupiga kwanza kabla ya kuuliza kwa nini.

Wenye shida na matatizo ni akina Mwema, Chagonja, Sillo, na huyu jamaa wa kanda maalum ya Dar. Hawa wanajitahidi kumpendeza mkuu wa kaya. Lakini wajue iko siku hawa wanaowatuma kupiga raia watageuza hizo bunduki kwao, na hapo ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno.

wamepewa toyota brand new,unategemea nini?ni lazima wambebe alowabeba.
 
Sikiliza, kuna wakati wanaweza wakawa hawapigi changa la macho halafu watu wabishi kama nyie mkang'ang'ania tu ubishi wenu mkawa "gadafized" shauri yenu.
 
Nimeshangazwa na kitendo cha Dr.slaa kulisifia jeshi la polisi kuwa limeanza kuelewa maana ya majukumu yake kwa kutenda haki na kutowapiga wanachadema waliokamatwa kwenye sakata la viwanja vya Arusha. Mimi binafsi naona jeshi ili bado linaendesha ukatili kwa wanchama wa vyama vya upinzani kinyume na usemi wa katibu mkuu wa Chadema.


source:twitter akaunti ya Dr slaa

twitter@drwilbroadslaa
Nilishasema humu kwamba CDMA wanawalisha sumu wanachama wao. Lolote linalosemwa na kiongozi wa CDMA kuhusu mazuri yanayofanywa na serikali ni kosa, basi mvukuzeni uanachama Dr. SLAA kwa sababu tayari ameshawasaliti katika yale mliokubaliana kupinga kila jambo. SLAA ameshatambua kuwa kuwasingizia polisi ili kujiimarisha kisiasa hakuna maana yoyote na hasa pale anapoona wanaofaidika na siasa za maji taka hizo ni wachache ambao hata yeye anaonekana kukosa nafasi. Tusubiri mengi yatagundulika tu kadri siku zinavyokwenda.
 
Nilishasema humu kwamba CDMA wanawalisha sumu wanachama wao. Lolote linalosemwa na kiongozi wa CDMA kuhusu mazuri yanayofanywa na serikali ni kosa, basi mvukuzeni uanachama Dr. SLAA kwa sababu tayari ameshawasaliti katika yale mliokubaliana kupinga kila jambo. SLAA ameshatambua kuwa kuwasingizia polisi ili kujiimarisha kisiasa hakuna maana yoyote na hasa pale anapoona wanaofaidika na siasa za maji taka hizo ni wachache ambao hata yeye anaonekana kukosa nafasi. Tusubiri mengi yatagundulika tu kadri siku zinavyokwenda.


Dr. slaa ni kati ya magwiji wa siasa na mtu aliyeleta mageuzi makubwa katika siasa taifa letu na kila mpenda maendeleo anatambua awe wa CCM au wa chama chochote kile , kwani juhudi zake kwenye kuleta mabadiliko kupingana na ufisadi
 
Hongereni polisi wa Arusha kwa kuanza kuwa na utu aliouona DR.Slaa lakini bado kazi ipo!!! Mnakaribia kuitwa polisi wa Tanzania.
 
Ni kweli kabisa Kamanda Siro ni kamanda bora kabisa katika jeshi la polisi hilo halina ubishi, hata Mwema hawezi kumfikia Siro katika uwezo wa kupambanua mambo na kusimamia haki za raia.
Hili nalisema toka moyoni kabisa kwa jinsi nilivyoweza kumfahamu kamanda Siro hata kupitia polisi walio wengi. mimi binafsi nimewahi kuonana uso kwa uso na kamanda Siro na kumsikiliza katika masuala mbalimbali, kwakweli nilikuja kusema Siro alipaswa kuwa IGP. Ni kamanda anae amini sana katika weledi kutatua mambo ndani ya jeshi la polisi kuliko kutumia nguvu. Ni msomi, mwelewa sana, ana busara sana. Nasema kama mwanza kipindi cha uchaguzi mwakajana isingekuwa na Siro leo hii tungekuwa tunakumbuka umwagaji damu jiji la mwanza.

Polisi wanahitaji kubadilika sana, kuachana na matumizi ya nguvu nyingi watumie busara zaidi hiyo ndo polisi jamii, lakini tukipata polisi wa aina ya kamanda wa wilaya arusha mjini hakika umwagaji damu Tanzania hauko mbali na chanzo kitakuwa polisi. pengine ni kutokana na kutumiwa sana na chama tawala.

Changamoto pia kwa Mwema, kwa maoni yangu anapaswa kubadilika sana katika kusimamia mambo ndani ya polisi, akiacha mambo ya jeshi la polisi kutumiwa na CCM watabaki salama. Kule Dodoma katika mgogoro wa ardhi eneo la Jedengwa inasadikiwa polisi wawili walipoteza maisha mmoja kuchomwa kisu tumboni na mwingine mshale wa sumu kisa kulinda eneo la tajiri Maimu.

Polisi please change!
 
Kuhusu Kamanda Siro ni kweli kabisa naweza kusema ni kamanda bora kabisa kuliko makanda wengi tanzania akiwamo Mwema mwenyewe. Ni mtu ambae anaamini sana kutatua tatizo kwa busara, mazungumzo na utulivu. Ni mtu anapenda kuheshimu haki na utu wa mwadamu. sio kama polisi wanaotumiwa hovyohovyo tu na chama tawala. Nilikuwa namsikia tu Siro akisifiwa hata na baadhi ya polisi wa kada za chini, siku moja nilipata kuzungumza nae uso kwa uso, hakika niliamini kabisa kuwa Siro alipaswaa kuwa IGP kuliko huyu tulie nae kwa sasa ambae ninashaka sana na uwezo wake kumudu majukumu yake ukizingatia sera yao ya '' POLISI JAMII''.

Siro ni msomi, mwelewa, ana busara, ana subira, ana jua maana ya majukumu yake n.k big up kamanda Simon Siro.

Ndugu wanajamii namsifu kamanda Siro kwasababu uchaguzi wa mwanza mwakajana isingekuwa Siro leo tungekuwa tunakumbuka umwagaji daamu wa mwanza, wengi mnakumbuka hali ilivyo kuwa lakini ni Siro aliyefanya uchaguzi na matokeo yabaki salama, lakini tungekuwa na kamanda wa wilaya Arusha mjini na kada mkongwe wa ccm, mambo yangeharibika.

Siro keep it up
 
​nadhani mbeya poilisi walifika wakati wakamwambia mkuu wa mkoa tafuna namna nyingine ya kutatua tatizo kutumia nguvu tutasababisha madhara makubwa......mwombe sugu atulize wananchi wake
 
Back
Top Bottom