Kwanini Dodoma na si Dar es Salaam?

Hakuna mtu aliyepinga kwenda Dodoma tatizo ni mipango.
 
Huu ni uswahili unaofanya ndio maana hatukuendelea muda mrefu kwa kuwa serikali ilijaa watu wenye mawazo ksma yako.Ukiyasoma na kumweleza mtu ni kama yana hekima fulani lakini ni pepo zito la umaskini ndilo linaweza kukyongoza kusema hivyo.Ndio maana mwingine anaoa hana hata kitanda lakini miaka kadhaa baadae anamiliki jumba la kifahari wakati mwingine anajipanga kabla ya kuoa lakini maisha yake yanabaki ya kawaida hadi anazeeka.Haya mambo ya kung'ang'ania Dar ni kuumiza watu wengi wanao fuata huduma Dar wakati watu wale wale wachache wanazidi kufaidika na pesa tunazowapelekea katika mahoteli nk.Bora kundi lingine la watu lianze kufaidi hicho wanachofaidi watu wa Dar.
 
Mkuu nchi haijaribiwi. Ni lazima tupange. Tutakwama. Ile budget yenyewe hatujui itatoka wapi. Tumehama kwenye viwanda, tunahamia uwekezaji wa majengo Dodoma.
Nchi haiwezi kukwama.Na kama kuna mtu anadhani atakwamisha ajue atakwama yeye
 
Kwahiyo hoja ni kugawana kufaidi? Niliuliza swali la msingi, Huduma gani watu wanafuata Dar wakati wa utandawazi?
 
Nchi haiwezi kukwama.Na kama kuna mtu anadhani atakwamisha ajue atakwama yeye
Unadhani nchi kukwama ni kama gari litakavyoonekana? Zile purukushani za wiki hii tunahamia, na mie mwezi ujao. Ziko wapi? Huo ndio mkwamo.
 
Sioni sababu ya kubashiri kukwama,mpango wa kuhamia Dodoma upo tangu enzi za mwalimu utekelezaji tu ulikuwa haujafanyika kwa sababu ya mawazo ya kiswahili swahili-tunajipanga,tupo kwenye mchakato,tunafanya upembuzi yakinifu,pole pole ndio mwendo,haraka haraka haina baraka nk!Hayo mambo kwenye hii dunia hayafai hata tu kutamkwa licha ya kuyafanyia kazi.
 
Kwahiyo hoja ni kugawana kufaidi? Niliuliza swali la msingi, Huduma gani watu wanafuata Dar wakati wa utandawazi?
Kazi nyingi za serikali hazifanyiki kwenye mitandao mkuu hili lazima ulijue
Unadhani nchi kukwama ni kama gari litakavyoonekana? Zile purukushani za wiki hii tunahamia, na mie mwezi ujao. Ziko wapi? Huo ndio mkwamo.
 
Kazi nyingi za serikali hazifanyiki kwenye mitandao mkuu hili lazima ulijue
Transformation nyingi zinazofanyika sasa hivi zinategemea teknolojia. Tungewekeza kwenye hili, hayo mengine yangekuwa historia. Yaani mtu kusafiri na kupeleka barua inatakiwa habari hii ifike mwisho. Mfano tenda na maombi ya kazi hufanywa online. Tujiimarishe kwenye maeneo mengine pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…