Kwanini Dodoma na si Dar es Salaam?

Kwanini Dodoma na si Dar es Salaam?

Unaongelea budget gani mkuu?????. Ile budget ya wabunge wa CCM ni budget hewa. Mkuuu hana tabia ya kufata budget ya bunge. Yeye hufanya anacho amua hata kipind ni wazir pesa za wizara yake zilikuwa zikitumiwa tofaut na bunge lilivyopanga. Sasa kama ndyo amekua mkuu wa nchi ile budget ya CCM ni hewa yeye kila siku atakuwa anakuja na maamuz yake.
Hehehe kashike
UKUTA
 
Hivi wewe una akili kichwani?
Hivi mtihani wa darasa la nne ulifaulu kweli?
Hivi mji mkuu wa tanzania ni upi?
Ni kawaida ya mtu dhaifu kuficha ukweli badala ya kuufanyia kazi. Haya wewe uliyefaulu mtihani wa darasa la 4, hebu nikuhoji kidogo...wakati bwana mkubwa alipokuwa waziri wa 'lami' na yahusianayo, aliwahi kutaka kuvunja jengo la makao makuu ya TANESCO pale Ubungo kwa kuwa limejengwa kwenye hifadhi ya barabara? Niko sahihi?
 
Alishasema hii nchi ni tajiri..kwa nini hutaki ..yeye unajua hazina kuna shilingi ngapi...kama hutaki kwenda Dom acha kazi vijana wapo wengi sana mtaani wanahitaji ajira
Mkuu, suala si kuacha kazi au kutotaka kwenda Dodoma. Kilio ni vipaumbele. Kwenye michango ya harusi watu hukaa chini na kutambua budget kisha hupanga sherehe. Sisi tunashereheka lakini hatuna bajeti. Tujiulize, pesa za kwenda Dodoma zinatoka wapi? Wafanyakazi wangapi watahama? Waziri Mhagama anasema pesa za ujenzi wa majengo yaliyopaswa kufanyika Dar ziende Dodoma. Kumbe hata majengo hakuna lakini wiki ijayo watu wanahamia kule. Kwanini wasihame taratibu ili wasiyumbishe sekta nyingine. Sekta binafsi inayumba, sasa na serikali kutayumba. Si kila hutuba lazima iwe na tamko.
 
Hii ni laana ya kumfukuza matonya toka jijini Dar,sasa ni zamu yenu kufukuzwa town na kumfuata matonya kijijini.

Ila utawala huu,veeeeerrrrrrrryyyyy interesiting
 
Hivi wewe una akili kichwani?
Hivi mtihani wa darasa la nne ulifaulu kweli?
Hivi mji mkuu wa tanzania ni upi?
Asante ndugu. Bahati mbaya wakati nipo darasa la nne, mitihani ilifutwa. Kwahiyo sikufanya kabisa. Sijapinga kuhama ila hii namna ya kukurupuka. Yule mh kasema ndani ya miaka minne na ushehe. Wengine wanaibuka eti ndani ya wiki.
 
Jamaa wa Dar walizoea kuwaita watanzania wenzao kuwa ni wa mikoani sasa tuone wakifika Dodoma wagogo wakawaita wa mikozi watasemaje. Magufuri awagawaie watumishi viwanja pale Dodoma ili hela walizopiga zamani tuzione pale. Dodoma ikue na Dar Isinyae kidogo na Gesi izalishe umeme Mtwara ndio kilichokuwa kilio chetu. Hatukufurahi Dar kupora makao makuu ya nchi kwa muda wote huo. Kwa vile kuna polisi ila mapema tungeandamana kudai makao makuu Dodoma, Dar Mji gani wa kuamka saa 10 usiku. Watumishi wanaotoa maamuzi na kutengeneza sera wana usingizi ndio maana miaka hamsini ya Dar haikutusaidia.
Dar ina matatizo yake, hakuna shaka. Hapa kinachozungumzwa ni namna maamuzi makubwa yanavyopangwa hovyo hovyo. Hivi bajeti ya kuhamia Dodoma ni kiasi gani? hizo pesa zitatoka kwenye fungu lipi? Kwa haraka za wizara zote kukimbilia huko, Dodoma itaweza kubeba watu wote kwa muda mfupi kwa miundombinu iliyopo? Kwanini kama kuna ulazima tusihame taratibu? Nini athari kwa biashara? Je, uchumi wa nchi utapanda au kupungua?
 
Hivi kuna ulazima gani wa kuhamia Dododma kwa sasa? je? ni gharama kiasi gani zitatumika kuhamisha ofisi hizi? je? Sisi wa lala hoi ambao tuliambiwa hii nchi ni yetu sote kuna tunacho faidi hapa kweli? Hii sii hali ya kuendelea kulewa misifa na kusahau kuwa wako wanaoteseka? Ni nini hasa hakiwezi fanyika kama serikali ikibaki Dar? Any way serikali iliwahi toa bei elekezi ya sukari kuwa shs 1800 lakini leo hii kilo ya sukari ni shs 2500-3000. usafi ulianza kwa mbwembwe lakin leo hii miji imejaa taka, Ilianza kwa kujidai kuwa elimu bure lakin taratiibu ikaanza kupigia watanzania magoti iwasaidie madawati, na mengine mengi. Sasa je hatuoni kuwa kukurupuka huku hakutufikishi popote?
 
Duh umenifurahisha, ni kweli hakuna sababu zaidi ya makabrasha ya kikao cha baraza la mawaziri cha mwaka 1973. Tunakwendaje huko kwa Matonya? Nauli iko wapi? Tunatengeneza unnecessary uncertainty to businesses and potential investment. It is very hard to script Dr Magufuli's thoughts. With no template, we cannot hold our leaders' accountable. Yaani hatujui mheshimiwa akiibuka atasema nini? Huenda akaamua kufuta flyovers zote. Maana nchi ndio inahama hivyo.
Hahaaa, na kwa sababu walishazoea kujiuzia na kuharibu sehemu za kihistoria katika nchi yetu, ikibidi pale jumba jeupe wavunje, tupafanye kuwa Coco beach ya pili iliyo wazi kwa kila mtu, itungwe sheria ya kupalinda isiyobadilika kama ya WAMEDI na WAAJEMI wa kale kuwa hakuna kubadilisha matumizi yake!

Kwanza jengo lenyewe inaelekea watu wakiingia mle, utu unawatoka, sijui lina mapepo tangu Mjerumani?! Bora pawe wazi tu tuwe tunaenda kuvuta uvundo wa soko la samaki tukijidai tuko beach....
 
Hii nchi inaendeshwa kwa matukio nnakumbuka iliwahi kuzungumzwa kuna baadhi ya mawaziri wametumia gharama kubwa kuzifanyia ukarabati mkubwa ofisi zao hiyo hasara iliyotumika itafidiwa vipi.
 
Hahaaa, na kwa sababu walishazoea kujiuzia na kuharibu sehemu za kihistoria katika nchi yetu, ikibidi pale jumba jeupe wavunje, tupafanye kuwa Coco beach ya pili iliyo wazi kwa kila mtu, itungwe sheria ya kupalinda isiyobadilika kama ya WAMEDI na WAAJEMI wa kale kuwa hakuna kubadilisha matumizi yake!

Kwanza jengo lenyewe inaelekea watu wakiingia mle, utu unawatoka, sijui lina mapepo tangu Mjerumani?! Bora pawe wazi tu tuwe tunaenda kuvuta uvundo wa soko la samaki tukijidai tuko beach....
Wazo lako zuri. Huenda tukapata pesa zetu kwa kufanya nyumbani kwa mheshimiwa ni sehemu ya utalii. Pia na pale Benki Kuu. Sijui kesho mwenye nchi atasema nini? Huyu kawagusa wananchi kuanzia kwenye sukari mpaka ajira. Ngoja tuone kwa Matonya.
 
Mkuu, suala si kuacha kazi au kutotaka kwenda Dodoma. Kilio ni vipaumbele. Kwenye michango ya harusi watu hukaa chini na kutambua budget kisha hupanga sherehe. Sisi tunashereheka lakini hatuna bajeti. Tujiulize, pesa za kwenda Dodoma zinatoka wapi? Wafanyakazi wangapi watahama? Waziri Mhagama anasema pesa za ujenzi wa majengo yaliyopaswa kufanyika Dar ziende Dodoma. Kumbe hata majengo hakuna lakini wiki ijayo watu wanahamia kule. Kwanini wasihame taratibu ili wasiyumbishe sekta nyingine. Sekta binafsi inayumba, sasa na serikali kutayumba. Si kila hutuba lazima iwe na tamko.
Suala la kuhamia Dodoma lilipitishwa tangu mwaka 1973 na Mwalimu lkn utekelezaji wake ulikwama kwa sababu ya hoja kama hizo zako. Sasa kama tukiendelea kuitaka serikali ijipange ndo ihamie Dodoma story itabaki kuwa ile ile. Me namuunga mkono Rais serikali iende Dodoma kama ni kujipanga watajipanga huko huko. Ambae hana nauli ya kwenda Dom basi na aache kazi vijana tupo wengi sana mtaani tunahonga pesa kibao tupate kazi na hatupati, tukisikia Dodoma kuna kazi tutaenda hata kwa malori ya mizigo.
 
wakati mwingine kudiriki kushindwa ni kujiingiza kwenye gharama zisizo za lazima. Nchi bado inachangamoto nyingi tu za msingi ;kama kiongozi anahitaji akumbukwe kwamba aliifanyia kitu flani Tanzania ni bora akafuata taratibu na kutokua na haraka ya utekelezaji wa mambo ya msingi anayotaka kuyafanya.

Uku tukiwa bado tunalaumu Sera ya elimu bure kuonekana chanzo cha Sera ya kubana matumizi;linaibuka tena jingine la kuhamia Dodoma. Tunapokwenda hatupafahamu ukweli ndo huo.
Wewe ndio haupafahamu unapo kwenda...
 
Suala la kuhamia Dodoma lilipitishwa tangu mwaka 1973 na Mwalimu lkn utekelezaji wake ulikwama kwa sababu ya hoja kama hizo zako. Sasa kama tukiendelea kuitaka serikali ijipange ndo ihamie Dodoma story itabaki kuwa ile ile. Me namuunga mkono Rais serikali iende Dodoma kama ni kujipanga watajipanga huko huko. Ambae hana nauli ya kwenda Dom basi na aache kazi vijana tupo wengi sana mtaani tunahonga pesa kibao tupate kazi na hatupati, tukisikia Dodoma kuna kazi tutaenda hata kwa malori ya mizigo.
Mwalimu alipitisha mengi saana. Kama tunaweza tuanze na azimio la Arusha, la Musoma na mengineyo. Turudishe vile vijiji vya ujamaa. Taifa lihodhi kila kitu. Kwahiyo ndugu, si kila jambo la wakati ule linafaa kwa sasa. Wakati ule kusafiri kutoka Dar kwenda Mwanza ni siku 3. Njia ya mawasiliano ni barua na telegram kwa wananchi wa kawaida. Kama kweli tumeamua, tuamue kama Taifa na si kukurupuka. Kwani tukihama kwa wizara chache chache bila kuharibu mipango mingine ya nchi kuna tatizo gani. Tuhame kwenye hiyo miaka 5 si kwenye wiki moja.
 
Duh umenifurahisha, ni kweli hakuna sababu zaidi ya makabrasha ya kikao cha baraza la mawaziri cha mwaka 1973. Tunakwendaje huko kwa Matonya? Nauli iko wapi? Tunatengeneza unnecessary uncertainty to businesses and potential investment. It is very hard to script Dr Magufuli's thoughts. With no template, we cannot hold our leaders' accountable. Yaani hatujui mheshimiwa akiibuka atasema nini? Huenda akaamua kufuta flyovers zote. Maana nchi ndio inahama hivyo.
Kwa taarifa yako Dar ni commercial city na Dodoma ni Capital City. Kuahirishwa kwa uamiaji wa serikali kuelekea Dodoma, kumekuwepo kwa muda mrefu. Na huu ni wakati muafaka wa kuhamia, ngoja ngoja utakuta mtoto sio wako, wanasema waswahili.
 
Mwalimu alipitisha mengi saana. Kama tunaweza tuanze na azimio la Arusha, la Musoma na mengineyo. Turudishe vile vijiji vya ujamaa. Taifa lihodhi kila kitu. Kwahiyo ndugu, si kila jambo la wakati ule linafaa kwa sasa. Wakati ule kusafiri kutoka Dar kwenda Mwanza ni siku 3. Njia ya mawasiliano ni barua na telegram kwa wananchi wa kawaida. Kama kweli tumeamua, tuamue kama Taifa na si kukurupuka. Kwani tukihama kwa wizara chache chache bila kuharibu mipango mingine ya nchi kuna tatizo gani. Tuhame kwenye hiyo miaka 5 si kwenye wiki moja.
Kaka hii ni golden chance tumeipata tusiipoteze, Magufuli akimaliza muda wake anaweza akaja raisi mwengine na mipango mengine kabisa, suala la Dodoma likatiwa kapuni kama walivyofanya maraisi waliotangulia. Tufanyeni fasta jamani ndani ya miaka hii mitano ya Magufuli serikali ihamie Dodoma. Kama ni soka nasema hii ni penati tumepewa dakika ya 90 tufunge tusonge mbele, tukizubaa Magu akiondoka hili suala litasubiri tena miaka mingine 50.
 
Kwa taarifa yako Dar ni commercial city na Dodoma ni Capital City. Kuahirishwa kwa uamiaji wa serikali kuelekea Dodoma, kumekuwepo kwa muda mrefu. Na huu ni wakati muafaka wa kuhamia, ngoja ngoja utakuta mtoto sio wako, wanasema waswahili.
Hakuna mashaka na definition ya makao makuu na commercial city. Hapa kinachuzungumzwa ni mipango ya kuamua kitu bila plan. Waulize hao wanaoenda wiki ijayo, wanastahiki zao zote? Kule sehemu ya kuishi et al pako vipi? Ukihama kwa pupa, utaongeza tija?
 
Vipaumbele na kero za wananchi vimeisha sasa wana focus kwenye mambo yasiyo na maana kuhamia dodoma!!
 
Back
Top Bottom