Kwanini Dodoma na si Dar es Salaam?

Kwanini Dodoma na si Dar es Salaam?

Waliosababisha yote haya ni UKAWA. Laiti Dar ingekuwa haiko chini ya himaya ya UKAWA zoezi hili lisingeibuka ghafla na kasi ya kustaajabisha ya kutaka Serikali kuhamia Dodoma.
 
Hakuna mashaka na definition ya makao makuu na commercial city. Hapa kinachuzungumzwa ni mipango ya kuamua kitu bila plan. Waulize hao wanaoenda wiki ijayo, wanastahiki zao zote? Kule sehemu ya kuishi et al pako vipi? Ukihama kwa pupa, utaongeza tija?
Kaka suala la kuhamia Dodoma lilikuwa linapigwa danadana miaka nenda miaka rudi. Wapo watu wengi tu ambao wanahamia kwenye nyumba zao wakati bado hazijakamilika, na zinakamilika wakiwa humo humo ndani. Suala la miundo mbinu na logistics ni la muda mfupi.
Serikali ihamie Dodoma, foleni zisizo na umuhimu zipungue jijini. Hakuna haja ya kuogopa changamoto maishani.
 
BAVICHA Tatizo Lao wanajua Sana Kukosoa.Awajui Kureason...Acha Serikali Iamie Dodoma

Serikali Aijakulupuka.

USHAURI.

TUPUNGUZE MIDOMO BAVICHA.TUFANYE KAZI TUKA INVEST DODOMA
 
Kaka hii ni golden chance tumeipata tusiipoteze, Magufuli akimaliza muda wake anaweza akaja raisi mwengine na mipango mengine kabisa, suala la Dodoma likatiwa kapuni kama walivyofanya maraisi waliotangulia. Tufanyeni fasta jamani ndani ya miaka hii mitano ya Magufuli serikali ihamie Dodoma. Kama ni soka nasema hii ni penati tumepewa dakika ya 90 tufunge tusonge mbele, tukizubaa Magu akiondoka hili suala litasubiri tena miaka mingine 50.
Unajua kitu kinakuwa golden chance kama kina faida. Hapo faida haieleweki. Kwanini Dodoma?
 
Kaka suala la kuhamia Dodoma lilikuwa linapigwa danadana miaka nenda miaka rudi. Wapo watu wengi tu ambao wanahamia kwenye nyumba zao wakati bado hazijakamilika, na zinakamilika wakiwa humo humo ndani. Suala la miundo mbinu na logistics ni la muda mfupi.
Serikali ihamie Dodoma, foleni zisizo na umuhimu zipungue jijini. Hakuna haja ya kuogopa changamoto maishani.
Serikali sio nyumba mkuu. Sina tatizo la kuhamia ila si kuhamia hovyo hovyo. Tatizo ni nini kutoa muelekeo wa Taifa? Kwani tukifanikiwa bila kukurupuka kuna tatizo?
 
Duh umenifurahisha, ni kweli hakuna sababu zaidi ya makabrasha ya kikao cha baraza la mawaziri cha mwaka 1973. Tunakwendaje huko kwa Matonya? Nauli iko wapi? Tunatengeneza unnecessary uncertainty to businesses and potential investment. It is very hard to script Dr Magufuli's thoughts. With no template, we cannot hold our leaders' accountable. Yaani hatujui mheshimiwa akiibuka atasema nini? Huenda akaamua kufuta flyovers zote. Maana nchi ndio inahama hivyo.

we jipange kwenda kufanya kazi kwa wananchi, Dodoma unaka enda kufanya nini? Nyie watu acheni utani Mh. Rais alishasema tujipange kwenda vijijini... ninyi mpo mnawaza umangi meza, white color jobs kwenye hili vumbi lilo jaa nchi nzima? Ndiyo maana utakuta watu wanvaa suti kwenye jua kali la Dar na ndivyo ilivyo tunataka kufunga tie kwenye umasikini huu wakati more than half ya population ipo kwenye umasikini uliotopoea, wanajishughulisha kivyaovyao huku wenye suti ndiyo wanaoitwa wataalumu na wote wamengang'ania Dar ambapo kwenye ukoloni ulikuwa ni mji wa kukusanya mali zote nchini zibebwe kwenye meli zipelekwe kwa wakoloni. The same set up tumetengeneza ndiyo maana kila mtu anatoa sababu ili aendelee kubaki hapo kwenye meli kubwa za nchi zilizoendelea waendelee kutajirisha nchi hizo kwa kununu suti zao na vyakula supermarket huku kule Dodoma wamejaa akina what you call 'matonya'....SHAME SHAME SHAME!

Vueni gloves zenu, ondoeni suti zenu na tie; kina Matonya ni matajiri wa resources ila ninyi akilini mmefungwa na kongwa la utumwa wa kutisha....Dodoma ina miundombinu yote ya serikali inayojitambua kuwa ni ya watu wanaohitaji msaada so whatever is available can be used only to reach out these Matonyas to give them the glory they deserve!
 
Acha kutoka povu basi...mi nimeshahamia Dodoma tayari nacheza na fursa

Word! Na wanaopiga mayowe ni hao hao waliozoea kuishi kwa damu za wenzao...wao kushika uchafu kwao mwiko ila wanapenda pesa inayozalishwa sehemu 'chafu' kwa kisingizo cha mshahara na marupurupu huku wenye nchi hawapati hata milo miwili......Magu hoyeeeeee!
 
Dah... Ndiyo hasa aina ya kiongozi tunayemtaka kwa wakati huu.... Miaka zaidi ya 50 ya pereteperete tupo palepale... Hebu tujaribu njia nyingine... "Karume Kenge aende shule"
Kwa kuwa ndiye mnayemtaka. ..subirini kidogo...asije mtu kubadili maneno hapa
 
Duh umenifurahisha, ni kweli hakuna sababu zaidi ya makabrasha ya kikao cha baraza la mawaziri cha mwaka 1973. Tunakwendaje huko kwa Matonya? Nauli iko wapi? Tunatengeneza unnecessary uncertainty to businesses and potential investment. It is very hard to script Dr Magufuli's thoughts. With no template, we cannot hold our leaders' accountable. Yaani hatujui mheshimiwa akiibuka atasema nini? Huenda akaamua kufuta flyovers zote. Maana nchi ndio inahama hivyo.
Nyie mnafikiria kipa umbele flyovers na wa mikoani wanafikiria afya, chakula, elimu na malazi
 
Jibu la kisiasa ni kwamba tunasogeza huduma kwa wananchi. Huduma zipi? Tunasogeza maendeleo kwa wananchi. Kwahiyo baada ya Dodoma tutahamia wapi?

Rais Magufuli anatamani nchi iwe ya asali kwa miezi kadhaa. Hivi karibuni kaanzisha mipango mingi saana yenye gharama kubwa.

Kuna flyovers (sijui zitasalimika maana watu wanahama), kuna mradi wa mwendo kazi Mbagala, ujenzi wa reli wa standard gauge (trillion 16 - budget yetu trillion 29), elimu bure kwa sekondari, kuna ule mradi wa barabara Dar mpaka Chalinze, kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu na miradi mingineyo.

Hili la Dodoma ni kuvuruga bajeti bila mpangilio. Mpango huu hata kama upo ukienda kwa taratibu tutapoteza nini? Wafanyakazi wanaambiwa wiki ijayo wawe Dodoma.

Hawa sio mbuzi kwamba hawahitaji kujipanga. Wanafamilia zao. Huu mpango ulivyo kuna ulazima gani wa kuikurupua serikali nzima kwa haraka? Kwanini tusipange. Hivi kipaumbele ni makao makuu au upatikanaji wa maji.
Wananchi wanashirikishwaje katika mipango inayowahusu.

Mheshimiwa mwenye nchi, mipango yenye kukurupuka huvuruga uchumi. Fikiria mwekezaji amekopa na anataka kuweka jengo la ofisi pale Posta. Ghafla unaibuka na mpango mkubwa kama huu.

Ni nani mwenye fikra timilifu atawekeza kwenye viwanda bila kufahamu mipango ya serikali. Nchi hujenga kwa mipango imara na yenye kueleweka.

Dira ya tunapoelekea lazima iwe wazi na ifahamike. Tumerithi mipango mingi saana kutoka tawala zilizopita.

Kuna mipango ya kijamaa ambayo tuliitia kapuni kimya kimya na mengineyo. Teknolojia imebadilika na kurahisisha kila jambo.

Wananchi wanahitaji huduma na sio sura za viongozi wa serikali hapa Dodoma.
Wewe hujui unaloliongelea unaongea kwa nadharia tu. Usidhani watu wamekurupuka wanajua ni wapi watapata fedha kwa ajili ya kuhamishia makao makuu dodoma. Tatizo mmezoea kufanya kazi kwa mazoea. Tubadilike jamani tuwe na subira tuone kama itashindikana.
 
Ameona mambo magumu baada ya miaka 5 hatakuwa na cha kuwaeleza wapiga kura hivyo anataka japo aambulie kura za kanda ya kati kwa kuwaambia alihamishia serikali dodoma na kuwaletea maendeleo.
 
we jipange kwenda kufanya kazi kwa wananchi, Dodoma unaka enda kufanya nini? Nyie watu acheni utani Mh. Rais alishasema tujipange kwenda vijijini... ninyi mpo mnawaza umangi meza, white color jobs kwenye hili vumbi lilo jaa nchi nzima? Ndiyo maana utakuta watu wanvaa suti kwenye jua kali la Dar na ndivyo ilivyo tunataka kufunga tie kwenye umasikini huu wakati more than half ya population ipo kwenye umasikini uliotopoea, wanajishughulisha kivyaovyao huku wenye suti ndiyo wanaoitwa wataalumu na wote wamengang'ania Dar ambapo kwenye ukoloni ulikuwa ni mji wa kukusanya mali zote nchini zibebwe kwenye meli zipelekwe kwa wakoloni. The same set up tumetengeneza ndiyo maana kila mtu anatoa sababu ili aendelee kubaki hapo kwenye meli kubwa za nchi zilizoendelea waendelee kutajirisha nchi hizo kwa kununu suti zao na vyakula supermarket huku kule Dodoma wamejaa akina what you call 'matonya'....SHAME SHAME SHAME!

Vueni gloves zenu, ondoeni suti zenu na tie; kina Matonya ni matajiri wa resources ila ninyi akilini mmefungwa na kongwa la utumwa wa kutisha....Dodoma ina miundombinu yote ya serikali inayojitambua kuwa ni ya watu wanaohitaji msaada so whatever is available can be used only to reach out these Matonyas to give them the glory they deserve!
Kwahiyo Mkuu, Dodoma ndio kwenye vumbi na umasikini? Basi bora Tabora kabisa au mikoa mingine. Kifupi hujaeleza sababu za kwanini tuhamie Dodoma na huduma zipi zitasogezwa. Bajeti yake ni kiasi gani na tunapata wapi pesa hizo? Kipaumbele ni Dodoma sasa hivi au ilikuwa mwaka 1973 wakati hakuna barabara?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wewe hujui unaloliongelea unaongea kwa nadharia tu. Usidhani watu wamekurupuka wanajua ni wapi watapata fedha kwa ajili ya kuhamishia makao makuu dodoma. Tatizo mmezoea kufanya kazi kwa mazoea. Tubadilike jamani tuwe na subira tuone kama itashindikana.
Kwahiyo Mkuu ni marufuku kuhoji? Je, kuna vitabu vya bajeti viwili ambapo kingine ni marufuku wananchi kukisoma? Yaani wanajua watawala tu? Nchi ya Demokrasia ni nchi ya kuhoji kama kipaumbele ni Dodoma au huduma za jamii? Tunahitaji tuambiwe tunaelekea wapi.
 
Nyie mnafikiria kipa umbele flyovers na wa mikoani wanafikiria afya, chakula, elimu na malazi
Ungepata muda wa kupitia post nzima ungejua ninasisitiza vipaumbele na si Dodoma. Hapo nilizungumzia mipango mingi ambayo bado inapangwa Dar es Salaam wakati nchi inahama.
 
Mbona kipindi cha bunge serikali yote inakuwa dodoma ?, mimi sijaona tatizo bado. Pili watu wengi uhamia kwenye nyumba zao kabla ya kukamilika na wakaendelea na ujenzi wakiwa ndani.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
we jipange kwenda kufanya kazi kwa wananchi, Dodoma unaka enda kufanya nini? Nyie watu acheni utani Mh. Rais alishasema tujipange kwenda vijijini... ninyi mpo mnawaza umangi meza, white color jobs kwenye hili vumbi lilo jaa nchi nzima? Ndiyo maana utakuta watu wanvaa suti kwenye jua kali la Dar na ndivyo ilivyo tunataka kufunga tie kwenye umasikini huu wakati more than half ya population ipo kwenye umasikini uliotopoea, wanajishughulisha kivyaovyao huku wenye suti ndiyo wanaoitwa wataalumu na wote wamengang'ania Dar ambapo kwenye ukoloni ulikuwa ni mji wa kukusanya mali zote nchini zibebwe kwenye meli zipelekwe kwa wakoloni. The same set up tumetengeneza ndiyo maana kila mtu anatoa sababu ili aendelee kubaki hapo kwenye meli kubwa za nchi zilizoendelea waendelee kutajirisha nchi hizo kwa kununu suti zao na vyakula supermarket huku kule Dodoma wamejaa akina what you call 'matonya'....SHAME SHAME SHAME!

Vueni gloves zenu, ondoeni suti zenu na tie; kina Matonya ni matajiri wa resources ila ninyi akilini mmefungwa na kongwa la utumwa wa kutisha....Dodoma ina miundombinu yote ya serikali inayojitambua kuwa ni ya watu wanaohitaji msaada so whatever is available can be used only to reach out these Matonyas to give them the glory they deserve!
Rudi utetee hoja yako. Suala la Dodoma si lele maana watu tuliona haiwezekani kwa haraka zile. Hata hii approach ya mawaziri na makatibu wakuu bado tata.
 
Mgonjwa huwa tumaini ndilo linalompa nguvu...ujiandaye kwenda kijijini...safari ya Dodoma ni lazima ila wale wanaohusika tu...wewe tafuta fursa ya kuwasaidia masikini kule kijijini..

Hoja yangu haihitaji kutetewa inasimama yenyewe...inakumulika kila siku kama ambavyo huwezi kukwepa mwale wa jua either unampenda au unamchukia Mungu!
 
Jibu la kisiasa ni kwamba tunasogeza huduma kwa wananchi. Huduma zipi? Tunasogeza maendeleo kwa wananchi. Kwahiyo baada ya Dodoma tutahamia wapi?

Rais Magufuli anatamani nchi iwe ya asali kwa miezi kadhaa. Hivi karibuni kaanzisha mipango mingi saana yenye gharama kubwa.

Kuna flyovers (sijui zitasalimika maana watu wanahama), kuna mradi wa mwendo kazi Mbagala, ujenzi wa reli wa standard gauge (trillion 16 - budget yetu trillion 29), elimu bure kwa sekondari, kuna ule mradi wa barabara Dar mpaka Chalinze, kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu na miradi mingineyo.

Hili la Dodoma ni kuvuruga bajeti bila mpangilio. Mpango huu hata kama upo ukienda kwa taratibu tutapoteza nini? Wafanyakazi wanaambiwa wiki ijayo wawe Dodoma.

Hawa sio mbuzi kwamba hawahitaji kujipanga. Wanafamilia zao. Huu mpango ulivyo kuna ulazima gani wa kuikurupua serikali nzima kwa haraka? Kwanini tusipange. Hivi kipaumbele ni makao makuu au upatikanaji wa maji.
Wananchi wanashirikishwaje katika mipango inayowahusu.

Mheshimiwa mwenye nchi, mipango yenye kukurupuka huvuruga uchumi. Fikiria mwekezaji amekopa na anataka kuweka jengo la ofisi pale Posta. Ghafla unaibuka na mpango mkubwa kama huu.

Ni nani mwenye fikra timilifu atawekeza kwenye viwanda bila kufahamu mipango ya serikali. Nchi hujenga kwa mipango imara na yenye kueleweka.

Dira ya tunapoelekea lazima iwe wazi na ifahamike. Tumerithi mipango mingi saana kutoka tawala zilizopita.

Kuna mipango ya kijamaa ambayo tuliitia kapuni kimya kimya na mengineyo. Teknolojia imebadilika na kurahisisha kila jambo.

Wananchi wanahitaji huduma na sio sura za viongozi wa serikali hapa Dodoma.
Umesahau daraja la busisi
 
Back
Top Bottom