Jibu la kisiasa ni kwamba tunasogeza huduma kwa wananchi. Huduma zipi? Tunasogeza maendeleo kwa wananchi. Kwahiyo baada ya Dodoma tutahamia wapi?
Rais Magufuli anatamani nchi iwe ya asali kwa miezi kadhaa. Hivi karibuni kaanzisha mipango mingi saana yenye gharama kubwa.
Kuna flyovers (sijui zitasalimika maana watu wanahama), kuna mradi wa mwendo kazi Mbagala, ujenzi wa reli wa standard gauge (trillion 16 - budget yetu trillion 29), elimu bure kwa sekondari, kuna ule mradi wa barabara Dar mpaka Chalinze, kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu na miradi mingineyo.
Hili la Dodoma ni kuvuruga bajeti bila mpangilio. Mpango huu hata kama upo ukienda kwa taratibu tutapoteza nini? Wafanyakazi wanaambiwa wiki ijayo wawe Dodoma.
Hawa sio mbuzi kwamba hawahitaji kujipanga. Wanafamilia zao. Huu mpango ulivyo kuna ulazima gani wa kuikurupua serikali nzima kwa haraka? Kwanini tusipange. Hivi kipaumbele ni makao makuu au upatikanaji wa maji.
Wananchi wanashirikishwaje katika mipango inayowahusu.
Mheshimiwa mwenye nchi, mipango yenye kukurupuka huvuruga uchumi. Fikiria mwekezaji amekopa na anataka kuweka jengo la ofisi pale Posta. Ghafla unaibuka na mpango mkubwa kama huu.
Ni nani mwenye fikra timilifu atawekeza kwenye viwanda bila kufahamu mipango ya serikali. Nchi hujenga kwa mipango imara na yenye kueleweka.
Dira ya tunapoelekea lazima iwe wazi na ifahamike. Tumerithi mipango mingi saana kutoka tawala zilizopita.
Kuna mipango ya kijamaa ambayo tuliitia kapuni kimya kimya na mengineyo. Teknolojia imebadilika na kurahisisha kila jambo.
Wananchi wanahitaji huduma na sio sura za viongozi wa serikali hapa Dodoma.