Kwanini Dkt. Kalemani hakamatwi na Polisi kuhusiana na kushambuliwa kwa risasi kwa Tundu Lissu?

Zaidi ya mara tatu nimemsikia Lisu akisema jirani yake huko Dodoma Mh. Medard Kalemani ambaye ni mbunge wa Chato hadi leo hajahojiwa kuhusiana na jaribio la kuuwawa kwake.

Lisu na Kalemani nyumba zao zinapakana huko kwenye makaazi ya vingozi Dodoma.

Swali langu kwa nini Lisu anasisitiza sana Mh. Medard Kalemani (mbunge wa Chato) ahojiwe? Je anadhani kuna kitu anajua? Hasa ukitilia maanani cctv camera zilizokuwa kwenye nyumba yao hadi sasa hazijatolewa hadharani?
Duh! Hii kesi imetelekezwa kwa kuangalia kwa jicho la tatu....Sio kwa jicho la Kangi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Police wangeanza naye huyu Mbunge wa Chato
Hawawezi kumhoji bila ruhusa ya JIWE.

JIWE kamwachia JIMBO.

Akamteua kuwa NAIBU Waziri NISHATI na MADINI, huku anasikilizia upepo.

Halafu akamtumbua MUHONGO, ili mtu wake ABAKI WATAFUNE VIZURI "INJI"

- Hazina
- Madini
- Nishati

Lazima kachomeka watu wake.
 
Makamanda bwana! Kwani Dr. Medard Kalemani ndio alikuwa dereva wa gari ya Toto Tundu!?
 
Lkn alipaswa kuwa mtu wa kwanza kuhojiwa.
Nadhani polisi wana mamlaka ya kumhoji au kupata maelezo yake hata kiwa nje ya nchi, kuna balozi zetu na kuna maafisa ambao wanaweza ku hukua maelezo ya dereva au ya lissi sio lazima akaripoti

By the way mimi nadhani dereva akienda kuripoti watamweka ndani bila maelezo na hawatamtoa, kumbuka yule dereva ni mwana familia wa Lissu kwa hiyo ni lazima familia imlinde

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Very true

Kuna kila dalili kuwa hili tukio lilipangwa na vyombo vya dola na vinaendelea kulindwa na vyombo hivyo hivyo!
Hawakuwa na plan A and B Kitendo cha kulipotezea swala hili imewapa wadau kufikiri zaidi ''it has made people to think outside the box''
 
na wakumbuke kwamba mwaka kesho ni uchaguzi mkuu yatasemwa mengi,au uchaguzi utafanyika bila kufanya kampeni?mtasemwa tu,japo ampendi kuambiwa ukweli
 
Tulimsikia Godbless Lema, akitoa tuhuma nzito pale Bungeni, kuwa Waziri wa Nishati, Dr Merdard Kalemani, ndiye aliyehusika na kuzinyofoa CCTV camera, zilizokuwa zikiwaonyesha watu waliomshambulia kwa risasi, Mbunge wa Singida Mashariki, pale Dodoma, Septemba 7 mwaka Jana.

Tuhuma hizo ni nzito na zimetolewa takribani wiki 3 sasa, lakini cha kushangaza Dr Kalemani hajazijibu tuhuma hizo kukiri au kukataa kutenda kosa hilo

Hivi sasa ni takribani miezi 8 tokea Mheshimiwa Tundu Lissu, amiminiwe risasi zaidi ya 30 kwa nia ya kumuua, ambapo Jeshi hilo la Polisi halijawahi kumkamata hata mtu mmoja kuhusiana na tukio hilo!

Nakumbuka baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi lilitoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za watu waliotenda tukio hilo baya kabisa watoe taarifa Polisi ili Jeshi hilo lichukue hatua kwa watu hao waiiotenda unyama huo

Sasa Godbless Lema ametekeleza ombi lenu Polisi, sasa ninachojiuliza hivi Jeshi la Polisi linapata kigugumizi gani kumkamata Dr Kalemani ili aweze kuelezea ni wapi amezipeleka CCTV camera hizo, ambazo zimewaonyesha watu waliofanya tendo hilo ovu??

Au ndiyo tuseme Jeshi la Polisi linajaribu kuwalinda watu hao waliotenda unyama wa hali ya juu kwa Mbunge wetu wa Singida Mashariki, Mheshimiwa Tundu Lissu??

Mungu ibariki Tanzania
Hata balozi Masilingi juzi alipohijiwa, alisema camera zile ni za Kalemani binafsi. Lakini hadi leo hajaulizwa. Au ni kwasababu wanafahamu zina ushahidi.
 
Nchi ya ajabu kwelikweli! Kumbe polisi wana pa kuanzia sasa. Iweje wasitimize wajibu wao? Hili suala linaharibu taswira ya kupendeza ya nchi yetu iliyojengwa 50+ years ago! Siyo sahihi hata kidogo kuichafua taswira hiyo ya amani, upendo na mshikamano kwa namna yoyote ile iwayo. Sauti hizi zinazosikika ni sehemu ndogo tu ya sauti zisizosikika waziwazi ambazo humjengea mtu ujasiri wa kufanya lolote ili kulipiza kisasi. Tusifike huko bali tutimize wajibu wetu kila mmoja kwenye nafasi yake.
 
Ili umkamate mtu YEYOTE Lazima uwe na inputs za kwenda kumuhoji... Namaanisha kuwa kama LEMA anao ushahidi huo sehemu ya kwenda kuutoa ni POLISI na wala siyo Viwanja vya Bunge.. Akiutoa Polisi ina maana ataeleza jinsi alivyofahamu kuwa aliyezitoa CCTV ni Dr Kalemani.. Ataeleza mmiliki wa hizo cctv ni nani..ataeleza anajuaje kuwa zilikuwa zinafanya kazi ama mbovu... Ili akiitwa Dr Kalemani Polisi tayari wawe na taarifa pana za kutosha kumuhoji kupata ukweli

Sasa tatizo la LEMA Taarifa NZURI NA NZITO kama hizo anatoa Ndani ya Bunge na kwenye media anaishia hapo

POLISI WALISEMA MWENYE TAARIFA AWAPELEKEE.. HAWAKUSEMA MWENYE TAARIFA AWAAMBIE WAANDISHI WA HABARI AMA AZITOE NDANI YA BUNGE

ndo Maana wenye uelewa tunafahamu kwamba LEMA ANATAFUTA POLITICAL MILEAGE.. ANATUMIA TUKIO HILO KUTAFUTA SIFA NA MVUTO WA KUHURUMIWA NA WANANCHI

Maana akiulizwa jibu atakalosema ni kwamba NA YEYE AMESIKIA HIVYO.. AMEAMBIWA HIVYO.. akiambiwa kumleta aliyemwambia utasikia kuwa WANATAKA KUTUBAMBIKIA KESI... upuuuuziii tu

Sorry Mkuu kama Nimekuwa kinyume na wewe
New #335
Mm nna swali mkuu. Mfano kukatokea na wavamizi/magaidi wakaua watu/raia maeneo ya mkusanyiko au kwingineko kokote. Halafu akatokea mbunge tu yeyte akasema bungeni kua anawajua hao watu...ila tu hajaenda kutoa taarifa polisi. Je Polisi watafanya nn kumhoji huyo mbunge na ikumbujwe kua ana kinga ya kuongea chochote bungeni?
 
Hili likijibiwa pia tutajifunza mengi.
utasubiri sana majibu
Instagram media - Bt2Krycj3b7.jpg
 
Na wewe usiwe kama lema mwenye shule ndogo! Cctv ni zangu Wala si za mtu mwingine nikiamua kuziondosha si naziondosha? Try to think young man! Hao Polisi watatumia kifungu kipi? Unajua watu humu wanawaogopa kuwaeleza ukweli kutokana na mitusi yenu ya kilejaleja wengine hatujali
Comments Kama hizi ndio zinafanya wengine tupigwe ban.
 
Back
Top Bottom