Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,251
- 44,586
Aloo unapaswa kutuheshimu sisi wa miji mingine ha wa vijijini. Siyo uungwana kutuita watu wa porini. Sasa ninyi wa mjini mna faida gani kama mmelala usingizi wa pono. Tumia maneno ya staha bana.Kweli una hoja, mimi kwa uzooefu wangu nadhani haya yanachangia
1. Wakazi wa Dar wakipato cha chini pengine na upungufu wa elimu huuza hata kura zao kwa 20,000 [mtumikie kafiri]
2. Benki kuu na benki zote kubwa zipo hapa Dar, fikiria! hapa si Polisi wala wakala wa uchaguzi anaweza nunuliwa tu.
3. Tume Nec,msajili wapo hapa, sasa watamuudhi mzee kweli! si unakumbuka 1995, boksi la kura kufika magomeni saa 9 mchana.
4. Seriakli[ccm] kuvuruga, si unajua vyuo vikuu vimefungwa hadi baada ya uchaguzi, hii ni kuzuia Dar kutekwa na wasomi.
5. Wapinzani wamekata tamaa, hawajiamini na hukimbilia maporini.
Aloo unapaswa kutuheshimu sisi wa miji mingine ha wa vijijini. Siyo uungwana kutuita watu wa porini. Sasa ninyi wa mjini mna faida gani kama mmelala usingizi wa pono. Tumia maneno ya staha bana.
Kwa hiyo kumbe madai ya kwamba wananchi hawana elimu (ya uraia) ya kutosha ni bogus!! Maana wakazi wa Dar wana access na mambo mengi sana kuwafanya wawe sophisticated kuliko wale wa vijijini. Mweeeeee
Kwanza kabisa pengine nisikubaliane nawe kusema Dar siyo ngome ya upinzani. Unamaananisha wa chama kimoja? Au upinzani kwa ujumla? Kama ni wa chama kimoja nadhani ni sahihi usemavyo, lakini kama ni kwa ujumla, inawezekana Dar ni ngome ya upinzani. Kukubalika kwa sasa kwa Chadema na ufuasi mkubwa wa CUF (ambao sidhani kama umeyeyuka sana sasa hivi) nadhani kwa pamoja ni zaidi wa ule CCM.
Iliszemekana wakati ule Watu wapatao laki 9 walikuwa wamejiandikisha hapa Dar na iliaminika kwamba Mrema angezoa zaidi ya laki 6. Kuvurugwa kwa uchaguzi mkoa wa Dar (ambao baadaye uliahirishwa kwa wiki tatu hivi) kulilenga kuisaidia CCM kuondokana na uwezekano wa run-off kwani idea ilikuwa ni kutizama kwanza Mkapa ana-fare vipi kutokana na matokeo ya kura za urais mikoani.
Kuahirishwa uchaguzi kuliiathiri sana NCCR kwani wapiga kura wengi walipandwa na hasira na kuchana shahada zao za kupigia kura – na NEC ilichelewa na pia haikupanga utaratibu mzuri wa watu kujiandikisha tena (wale walizozirarua shahada).
Hali kadhalika mgogoro uliozuka baina ya viongozi wa juu wa NCCR kuhusu ushiriki au la wa marudio ya uchaguzi, na pia kutokana na kushindwa kwa kesi iliyopelekwa Mahakama Kuu iliyotaka kufuta uchaguzi nchi nzima na kurudia wote upya.
Hivyo siku ya kupiga kura ilipofika, ni watu takriban laki nne na uchee ndiyo waliopiga kura. Ni dhahiri wafuasi wengi wa NCCR hawakupiga kura na hiyo iliwezesha
CCM kuzoa majority of the votes na viti sita kati ya saba vya ubunge mkoani Dar.
Kwa hiyo utaona kwamba ngome ya upinzani iko hapa Dar sema tu CCM ilianza kuifinya kwa mabavu tangu uchaguzi wa mwanzo.
muwawamko wa kisiasa uko zanzibar... watu wa Dar es salaam wanahitaji kuwaigiza watu wa zanzibar.Kwa hiyo, tunaweza kutabiri vizuri kama ilivyotokea kwenye kura za maoni vijijini kuwa mwamko wa kisiasa kwa kweli uko vijijini kuliko mijini!? Angalia ni wapi wabunge wengi wa CCM wameanguka?