Cammory,
Mtu hachukuliwa hatua za kisheria kwa tuhuma za kusadikika, unatakiwa uthibitisho, evidence.
Kuwa na fedha nyingi nje ya nchi sio kosa kisheria kama fedha hizo zimepatikana huko huko nje, kosa ni kama zimepatikana nyumbani, zikahamishwa isivyo halali.
Kwa mujibu wa sheria yetu, mshitaki ndie mwenye jukumu la kuthibitisha jinai, 'The burden of proof lies with the prosecution', sio jukumu la Chenge kuthibitisha uhalali wa fedha zake, anaweza kuwa amepewa sadaka na bilionea fulani na hawajibiki kumtaja wala kuthibitisha, bali kama serikali inadhani sio halali, inatakiwa ithibitishe ndipo imfikishe mahakamani.
Hii ndio Tanzania yetu, kama Kagoda kaomba bilioni 40 toka BOT kwa maandishi, fedha zikapitia account ya mtu anaeleweka humu humu nchini, zilipoingia, akazihamishia acount mbalimbali humu humu nchini na miongoni mwa accounts hizo ni za waheshimiwa zikiwemo za chama chetu kitukufu. Serikali inawajua wote tangu aliyeandika barua mpaka senti ya mwisho iliko fikia na bado ikashindwa kuchukua hatua yoyote, itakuwa vijisenti vya Chenge ambavyo serikali haina uwezo kujua vimetokea wapi, haina uwezo wa kuvizua na haina uwezo wa kumfanya chochote Mhe. Huyu.
Angalizo, pamoja na tuhuma zote hizi, Andrew Chenge ni mmoja wa wabunge wenye roho nzuri sana over the counter, kipindi chote cha Bunge, hukaa counter pale Dodoma Hotel, na wazee wengine akiwemo Mzee Mapesa, ukitokea kuwepo hapo, basi round zitakupitia haijalishi anakujua au la![/QUOTE]
Duh akiwa Dar kijiwe chake kipi niwe natembelea kipindi Mwezi ukiwa mchanga? Ila si anatembea na Silaha maana wengine after the 4th Chui aka Serengeti nabadilika na kuwa Tanzanian Chavez (nakua Patriotic) kuliko Dr. Slaa, sasa naweza kumkwaza Mzee Chenge akanirestisha in peace bure while watoto wangu ndio wanaanza chezea bunsen burner na test tubes.