TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 15,266
- 25,555
Wiki chache zimepita Tanzania imemaliza kufanya uchaguzi wake mkuu ambao umegubikwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za wananchi kuumizwa na wengine kuuwawa kutokana na madhira ya kampeni zilizolindima kwa miezi kadhaa hapo nyuma.
Tulishuhudia vikosi vya ulinzi wa mipaka ya nchi vikipita mitaani kwenye mikoa kadhaa ili kama si kuwatisha wananchi basi ilikuwa kuweka ulinzi na usalama kwa wananchi, kuelekea siku ya kupiga kura.
Inajulikana wazi vikosi vya ulinzi kama jeshi, polisi nk kila kimoja kina jukumu lake kwenye ardhi ya nchi iliyopo kwa wakati huo, kama hapa Tanzania jeshi la wananchi ni kulinda mipaka ya nchi nk, jeshi la polisi wananchi na mali zao nk, sasa ukija kukuta jeshi linaingia sehemu isiyo na madhara kwa nchi na kikosi kingine hakijaomba msaada au kuzidiwa basi lazima ujiulize kulikoni?
Uganda ni nchi jirani na Tanzania, ni wiki inaisha sasa nchi hiyo imeingia kwenye kampeni za uchaguzi wa kumtafuta kiongozi mwingine wa taifa hilo, ambapo mpaka sasa Rais Museveni bado anataka kuendelea kuongoza kwa kipindi kingine huku akiruhusu katiba kumpa kipaumbele.
Mpinzani mkubwa wa museveni ni Robert Kyagulanyi a.k.a Bobi Wine mwanamuziki kijana anayeonyesha kuwa na nia thabiti kupambana na Museveni mwenye mamlaka makubwa kiutawala nchini humo.
Takribani wiki imeisha baada ya Tume ya uchaguzi nchini Uganda kumpitisha Bobi Wine ambaye amekuwa mbunge wa Kyadondo na amewakikisha vyema, mgombea huyo wa kiti cha urais amekuwa anapata vitisho na kuandamwa na majeshi ya polisi na usalama nchini humo kwa kasi sana.
Nimekuwa nafuatilia kampeni za nchi hiyo mpaka unajiuliza hivi hii ni vita au ni nini?
👇
Wanajeshi wamevaa kivita wakiwa na magari ya kivita ya delaya wakizunguka mitaani, hii maana yake ni nini?
Kuna sehemu wanamzuia asifanye kampeni enei fulani kwa kisingizio kuna mgombea mwenzake anaendelea na kampeni wakati ratiba inamruhusu kuwepo eneo hilo.
Siasa hii ya kutumia vyombo vya usalama kama jeshi kwa wananchi wake hasa kwa nchi za ukanda wa maziwa makuu imetoka wapi na inaelekea wapi?
Hapa chini 👇 raia akiadhibiwa barabara na kikosi cha jeshi.