Mbona haya huku yasema? kama wewe siyo mnafki na mchakubimbi tena mbeyaaa sana tu. %^)&_&_- yako.
Majeruhi mwingine, Abdallah Hilali (39), aliyelazwa katika Hospitali ya Arusha Lutheran Center, amedai kuwa majeraha aliyopata miguuni yametokana na kupigwa risasi na polisi na kudondokewa na vipande vya bomu.
Alisema alikuwa nyuma ya jukwaa kuu akimsikiliza Mbowe na alipomaliza kuhutubia alishuka jukwaani kukusanya sadaka, ndipo alipoona mfuko wa mweusi mdogo wa plastiki ukipeperuka juu.
Nilidhani ni upepo unapeperusha kitu, lakini ghafla nilisikia kishindo na nikamsikia mama mmoja akipiga kelele kuwa aliyerusha mfuko anakimbia, nilipogeuka nikajikuta nipo chini, alisema Hilali.
Alisema alipokuwa anaangalia aliona kijana mmoja amekaribia kumfikia aliyerusha bomu lakini ghafla akapigwa risasi na kuanguka chini na aliyekuwa anafuatia kwa nyuma naye akapigwa risasi akaona anaruka na kudondoka chini huku damu zikivuja.
Lakini mwisho wa yote kijana aliyerusha hilo fuko aliingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi. Mimi nilikuwa chini, alisema Hilal mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alipotembelea majeruhi hospitalini hapo.
source Mwananchi : 6/18/2013