Kwanini CHADEMA mnatutenga Ileje?

Katika kumbukumbu zangu hii ni thread ya pili kudai uongozi wa CHADEMA Taifa kwenda Ileje.

Hoja hii isichukuliwe powa, kuna mdau kasema hapo juu kuwa majani yamekauka yanasubiri kiberiti tu.

Naona ameachiwa Gwamaka na wenzake ambao nao wameanza mwaka huu kwakuwa ni wa uchaguzi. Tumaini Makene fikisha hizi taarifa makao makuu.

Ileje pamwanya ngani
 
Last edited by a moderator:
Jamani kila siku tunasikia mkutano wa CHADEMA kila kona ya nchi. Mbona sioni mikutano kama hiyo jimbo ya Ileje?.

Nipo hapa Isongole watu tunazidi kutamani kuwaona viongozi wa kitaifa wakihutubia mikutano ya hadhara.

Tunaomba msitusahau katika ukombozi wa taifa letu na sisi ni watanzania kama Tunduma walivyo.

Kwa ujumbe huu naomba mtukumbuke kwa ziara.

@Mbuzimtu NAOMBA TAFADHARI TUTAFUTANE KWA MSG.....ISONGOLE NI NYUMBANI NA KILA NIKITAKA KUANZISHA UZI HUU SHETANI ANAINGILIA KATI..............AHSANTE KWA KUWEKA UZI HUU HAPA........


SHAUKU ILIYOPO ISONGOLE, ITUMBA JUU YA CHADEMA NI KUBWA MNO PLZ AND PLZ TUNAWAHITAJI VIONGOZI WA JUU WA CHADEMA MJE HUKU.......

cc.richard kabungo mpiganaji mpambanaji kuwaletea democrasia ya kweli isongole.......
 
Heshima yako Mbuzimtu, pia nikupe pole kwa kilio ulichokitoa cha kukosa kuona ziara za viongozi wetu CDM kitaifa.

Ni ukweli usiopingika, ujio wa viongozi wa kitaifa ni faraja kubwa kwa wapiga kura hawa watarajiwa ktk kuchagua diwani, mbunge na rais kupitia UKAWA.

Niungane na wewe kuwaomba viongozi wa kitaifa kufika majimbo haya: Ileje na Rungwe Mashariki (BUSOKELO). Kilio cha wananchi hawa kutopata ziara ya viongozi wakuu kitaifa kimekuwa sugu. Na ni majimbo ambayo wananchi wake wako tayari sana kwa mabadiliko km ilivyo Kyela, Mbeya Mjini n.k

Mwisho nishauri, wabunge wa CDM ni aseti kubwa kwa chama wajitahidi kutoka na kufanya ziara kwa kushambulia. Majimbo mengi tutayachukua uchaguzi ujao lakini jitihada iongezeke kidogo, japo changamoto inaweza kuwa fedha hata hvyo wananchi wako tayari kuchanga kuwezesha ziara za waheshimiwa wabunge na viongozi wakuu wa chama. Kikubwa ni utayari tu makamanda.
 
Nimekaa Ileje hapo Itumba miaka kadhaa.... ni kweli CDM mnahitaji kufanya mikutano sana tena sana....sijawahi ona/sikia kiongozi wa kitaifa akiwasili Itumba au Isongole au popote pale kufanya mkutano na wananchi. watu wanaipenda sana CDM ileje hasa ikumbilo na isongole lakini elimu na ushawishi vinatakiwa vifanywe na viongozi wa wilaya kwa kusaidiwa na wa kitaifa. imagine lami ya kutoka mpemba-isongole itumba haizidi km 60 lakini tangu uhuru watu wanadanganywa....... CDM komaeni. CCM mtaji wao mkubwa ni woga na kukosa elimu kwa watu wa Ileje
 
Chonde chonde cdm! Tafadhali kati ya viongozi wa juu wanaokubalika sana huko Ileje aende bila kukawia, muda ndo huu ikiwezakana hata katibu mkuu akipige ziara ya siku kadhaa huko au fanyen operation maalum kande hiyo!
 
Ileje kuna makamnda machachari sana.

1. Gwamaka Mbughi aliyekuwa mwenyekiti wa Chaso UDSM ameshatangaza nia.... Uwezo wake wa kujenga hoja ni kama Kafulila.

1. Aliyekuwa ofisa habari Chaso mkoa wa Dar es Salaam Daniel Ezekiel naye anafanya mikutano. Yeye anagombea udiwani, akimuunga mkono swahiba wake Gwamaka.
 
Jamani gwakisa yule jamaa wa duce enzi hzo yukwapi ck hz? Je anaendelea na siasa? Kama ndiyo mbona kapotea sana? Ilikuwa ni kichwa moja matata na enzi kutokana na nguvu zake watu walijua ni mwanafunzi wa udsm main campus.
 
Jamani kila siku tunasikia mkutano wa CHADEMA kila kona ya nchi. Mbona sioni mikutano kama hiyo jimbo ya Ileje?.

Nipo hapa Isongole watu tunazidi kutamani kuwaona viongozi wa kitaifa wakihutubia mikutano ya hadhara.

Tunaomba msitusahau katika ukombozi wa taifa letu na sisi ni watanzania kama Tunduma walivyo.

Kwa ujumbe huu naomba mtukumbuke kwa ziara.

umempa za uzo kavukavu harudii tena kukukejeli, tatizo humu watu wanachukulia poa tu kwa sababu wamejificha nyuma ya keyboard zao
 
sijawahi kuona ccm ikiombwa kuhutubia mahali , haya yanayoitokea cdm hakika yana baraka za Mungu .
 
Back
Top Bottom