Hongereni kwa wana Ileje kuonesha shauku ya kupata Baraka na nasaha za viongozi wakuu wa CDM. Lakini la msingi ni watu gani mwawasimamisha kuwahimili wa vyama vingine? Mfano kuna watu wawili wa CCM huko inasemekana wanakubalika sana Godfrey Msongwe na Janet Mbene kwa Mbunge wa sasa Kibona inasemekana hana chake, Je, kwa makamanda walioonesha nia wapo vizuri kusimama kidete na hao? Ili hata ziara za wakubwa wa CDM ziwe na mantiki.