Labda kama hujui nini maana ya siasa za upinzani, CHADEMA wanajenga nchi vizuri zaidi wanapokuwa kama chama cha upinzani kuliko kuwa CCM. Kuna mambo mengi mno ambayo kama siyo CHADEMA yasingefanywa; hata kuchaguliwa Magu kulitokana na ccm kuona maji yamefika shingoni wakaona ngoja wasifanye mchezo safari hii. Hoja zote na ufisadi mkubwa kama kashfa za Simbioni, Agreka, na makampuni mengine ya kuzalisha umeme; na ufisadi na wizi mkubwa kwenye madini viliibuliwa na upinzani ukiongozwa na CHADEMA.Tumeshudia Nchi mbalimbali zikifarakanishwa na tamaa ya madaraka kwa baadhi ya viongozi wa vyama na vikundi mballimbali na kusababisha matabaka hofu na uvunjifu wa amani. Kama tuna malengo mema kwa Nchi yetu basi tushirikiane na kuondoa chuki na siasa za kuharibu mambo mema yaliyopo hivyo kama ilivyokua kwa Angola Unita kuunga na serikali ikiyopo madarakani na Mozambique Frelimo kuungana na Renamo na kuleta matokeo chanya Basi ni vyema na sisi tukaiga kwa Chadema kujiunga rasmi na CCM wachape kazi kujenga Taifa letu...nawasilisha View attachment 1101332