Kwanini CHADEMA inapata nguvu haraka?

Umenikumbusha mbali, ilishawahi nitokea, kweli nilimpata demu wakati mapema alikuwa ananisimbua. Ila nami nikamtema baadaye.
 
Kwa nini wanakimbilia CHADEMA?
Watu wengi wanaanza kujiaminisha kitawaongoza kuelekea “Uhuru wa pili”. Kama wazee wetu walivyokimbilia TANU dhidi ya mkoloni leo wapo watu wanakimbilia CHADEMA kwa sababu wanaanza kuamini kuwa labda nayo itawaongoza katika kujijengea kujitegemea, kujiheshimu na kuthaminiwa.
Hata hivyo, naamini changamoto kubwa zaidi kwa CHADEMA si kufanya maandamano au kuvaa magwanda bali ni jinsi gani itaongoza watu kuanza kujiletea maendeleo.

Ni lini kwa mfano tutaona viongozi wake wakifanya kama alivyofanya Nyerere katika ziara
yake ya pili ya vijiji vya Tanzania mwanzoni mwa miaka ya sabini ambapo alishiriki kazi za ujenzi wa Taifa. Kwa mfano, lini tutaona vijana wa CHADEMA
wakihamasika kupaka rangi shule, kuleta matofali, kuziba mitaro au hata kujenga kliniki
au kuboresha kliniki. Je, inatosha kufanya maandamano na kuhamaisha watu kujivua
gamba kama kuvaa gwanda mwisho wake ni kujisikia raha tu lakini si kufanya kitu?
Kumbe Watanzania wanapokataa haya mengine kimsingi wanakubali jambo linalowezekana. Swali ni lipi litawezekana chini ya CHADEMA
sasa kabla ya 2015? Historia itaamua.

Vyovyote vile itakavyokuwa Watanzania hawatokubali tena kuonewa, kunyanyaswa,
kupuuzwa, kunyonywa na kwa hakika hawatokubali kudanganywa tena. Wanataka
vitendo vyenye kuonyesha kuwa watawala na wale wanaotaka kuja kutawala wanawapa
thamani wanayostahili, wanawajali na kuwaheshimu kama wananchi.
 
Swali kwako;

Miaka hiyo ya sabini Nyerere alikuwa anatawala ama anawania kutawala (sasa fananisha na Chadema)

Hayo yote unayoyasema usingeyasema kama kodi zetu na maliasiri zetu zingetumika ipasavyo, lakini kwa ufisadi uliopo ndio maana unawaza kwenda kupaka rangi shule wakati kodi yako inatakiwa kufanya hayo!

Wape Kura Chadema ili wasimamie maendeleo ya watanzania wote kwa kuleta utawala bora.
 
Kurunzi, ngoja nikupe msimo wangu, labda utasaidia kuwaelewa wengine wengi. Mie binafsi sipendi siasa, na wala si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa. Lakini ningependa sana Chadema wachukue nchi, si kwa kuwa nawaona kina Slaa, Mbowe na kina Kabwe ni bora sana zaidi ya viongozi wa CCM, bali kwa kuwa uongozi wa CCM umejisahau sana, na kuwachukulia Watanzania "for granted". Imefikia mahali ambapo unashindwa kuelewa kama viongozi wetu hata wanatumia common sense kufanya maamuzi, na kama kweli wapo kwa ajili ya nchi na wananchi wake. Hivyo kwangu Chadema inakuwa ni "wake up call" nzuri sana kwa CCM. In fact niliwahi kuandika kwamba katika mambo ambayo ningemheshimu sana JK ni kama angeendeleza nguvu ya upinzani badala ya kuwa na nia ya kuuua kama alivyokuwa Mkapa. Nataka tuwe na Raisi anayetambua kwamba Tanzania ni more than chama chake cha siasa, na sio the other way round.

Kwa msingi huo nisingependa CCM ife. Ningependa Chedema ichukue nchi lakini CCM ibaki na nguvu kuwapa changamoto Chadema watakapokuwa madarakani. In fact, ideally, ningependa kuona tuna vyama maximum vitatu vya siasa nchini. Yale yaliyotokea kwa KANU kule Kenya na UNIP kule Zambia yanasikitisha sana. Kufa kwa chama kikubwa cha siasa kunaletelea monopoly ya political powers katika nchi, na hii haifai hata kidogo. Angalia ANC wanavyojisahau kule South Africa kwa kuwa wana monopoly ya kisiasa, na jinsi inavyowaletea tatizo kwa sasa toka kwa wananchi na vyama vy wafanyakazi, kutia ndani hata na watoto wao ANCYL. Hii pia inaletelea kukikuza chama mpinzani mkubwa wa ANC kinachoitwa DA, japo mwanzoni kilionekana kama ni chama cha wazungu badala ya National Party kilichokuwa cha Makaburu enzi za apartheid.

Hivyo hata Chadema wakichukua nchi, nitasikitika sana ikiwa watakuwa na nia ya kuiua CCM kabisa. Hata wakifanya hivyo, eventually nao kama vile tu CCM wataafika mahali waanze kujisahau, na kosa lilie lile litakaloiondoa CCM madarakani litakuja kuwaondoa Chadema madarakani hapo baadaye. Usipokuwa na mpinzani makini utajisahau tu, na hutakuwa strategic kwa chama chako na katika kuiongoza nchi. Hiyo ni law ya nature. Hivyo chama makini kitataka kuwe na mpinzani makini, kama kweli kina nia thabiti ya kuendeleza nchi na sio kutaka uongozi kwa uroho tu wa madaraka na mali.
 
Ndugu zangu Watanzania,habari zenu?natumai wote hamjambo na bila shaka mna ndoto ya kuendelea kusubiri kauli ya CCM ya maisha bora kwa kila Mtanzania itimie!Tuyaache hayo,hebu leo tuangalie ni kwa nini watu wengi wanaipenda CHADEMA?Binafsi nimekua nikiona nyota ya CDM ikipaa na kung'aa kila iitwapo leo!Hebu kwa pamoja tujadili ni kwanini watu wanaipenda CDM,hii itasaidia kuwafanya watu kuwa na sababu kadhaa za kuipenda CDM na hata wengine wenye mioyo ya dhati kwa CCM kuendelea kukipenda na kukijenga chama chao kama sababu za wana CDM zitakuwa dhaifu.Naomba kuwasilisha.
 
M nilikuwa naipenda sana ccm lakin ufisad ukawazid nikahamia Cdm kwasababu wana mtazamo mzuri na sera zenye kuleta maendeleo kwa taifa hapo baadae mis u (cdm)
 
Ndugu zangu Watanzania,habari zenu?natumai wote hamjambo na bila shaka mna ndoto ya kuendelea kusubiri kauli ya CCM ya maisha bora kwa kila Mtanzania itimie!Tuyaache hayo,hebu leo tuangalie ni kwa nini watu wengi wanaipenda CHADEMA?Binafsi nimekua nikiona nyota ya CDM ikipaa na kung'aa kila iitwapo leo!Hebu kwa pamoja tujadili ni kwanini watu wanaipenda CDM,hii itasaidia kuwafanya watu kuwa na sababu kadhaa za kuipenda CDM na hata wengine wenye mioyo ya dhati kwa CCM kuendelea kukipenda na kukijenga chama chao kama sababu za wana CDM zitakuwa dhaifu.Naomba kuwasilisha.

Mada nyingine bana aaaah !
 
watu wanaipenda cdm si kwa sababu ni nzuri sana au wasafi sana bali wamechoshwa na ccm na wanaona cdm kama njia mbadala. Ccm imeshindwa kabisa kuleta maisha bora kwa watanzania kwa miakka 50 waliyotawala. Hatuwezi kuendelea kutegemea majibu tofauti kwa kufanya jambo kwa njia ile ile ambayo ilishindwa.
 
try and error lzm itumike!naichukia nyinyiem coz ya ufisadi,na kushindwa kusimamia sera zao!bora cdm ichukue,ikishidwa nayo tutaitoa!
 
Pamoja na hayo,kwanini vyama vingine havipati umaarufu na havipendwi na watu?
 
Sababu ni moja tu....ni kushindwa kwa serekali ya ccm kutatua matatizo ya wananchi wake fullstop
 
1. Ugumu wa maisha.
2. Ukosefu wa ajira kwa vijana.
3. Matumizi makubwa na ya anasa kwa viongozi.
4. Kupeana nafasi za uongozi kishkaji.
5. Ongezeko la wasomi wengi wasio na ajira.
6. Kuchoshwa na Serikali ya kimazoea.

KAMA SERIKALI INGEYAFANYA HAYA:

1. kutoa ajira kwa vijana.
2. Kudhibiti mfumuko wa bei....

CHADEMA INGEKUWA KAMA VYAMA VINGINE VYA KWAIDA SANA..

LAKINI PAMOJA NA KUSHABIKIA CHADEMA JE , WANACHAMA WAKE WANAJUA CHAMA CHAO KITAWAFIKISHAJE PALE WANAPOTAKA??

CDM IMEJIANDAA KWA HAYA; 1.uwajibikaji 2.umakini 3.kupunguza matumizi ya serikali eg.magari na furniture kila mwaka 4.kupunguza gharama za maisha kwa umma 5.kupunguza utegemezi wa bajeti kwa kutumia maliasili za taifa kikamilifu na umakini mkubwa 6.kurudisha dhamira ya umoja na usawa miongoni mwa watanzania pasi kujali matajiri au maskini katika kunufaika na fursa za taifa
 
1. Ugumu wa maisha.
2. Ukosefu wa ajira kwa vijana.
3. Matumizi makubwa na ya anasa kwa viongozi.
4. Kupeana nafasi za uongozi kishkaji.
5. Ongezeko la wasomi wengi wasio na ajira.
6. Kuchoshwa na Serikali ya kimazoea.

KAMA SERIKALI INGEYAFANYA HAYA:

1. kutoa ajira kwa vijana.
2. Kudhibiti mfumuko wa bei....

CHADEMA INGEKUWA KAMA VYAMA VINGINE VYA KWAIDA SANA..

LAKINI PAMOJA NA KUSHABIKIA CHADEMA JE , WANACHAMA WAKE WANAJUA CHAMA CHAO KITAWAFIKISHAJE PALE WANAPOTAKA??

Tunajua na tunaamini watatukomboa'
 
Back
Top Bottom