Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Migogoro yote itokanayo na tafsiri za mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni miliki ya EAST AFRICAN COURT OF JUSTICE.
Chadema hili wanalielewafika lakini mapingamizi yao juu ya utaratibu wa kuwachagua wabunge wao wawili ndani ya Bunge la Afrika Mashariki wanakimbilia High Court ambayo haina mamlaka.
Swali la kujiuliza ni kwa nini High Court ina mvuto na EACJ ni shubiri kwao?
Nionavyo Chadema wanakwazwa na uamuzi wa Komu wa EACJ (supra) ulioamua Bunge ndilo lenye mamlaka ya kujipangia utaratibu ionao unafaa katika kuwapata wabunge wa kuliwakilisha taifa kwenye EALA.
Bunge limeamua Chadema ongezeni majina yawe angalau mawili kwa kila nafasi hivyo kuliwezesha Bunge kufanya uchaguzi huku wanamagwanda wakiheshimu uwiano wa kijinsia.
Chadema wanataka kuligeuza Bunge kuwa ni "rubber stamp" jambo ambalo linakinzana na East African Treaty ambayo inaelekeza Bunge lifanye uchaguzi na kupeleka jina moja kwa kila nafasi ni dhahiri kukiuka maudhui yote yaliyoainishwa na TREATY.
Kwa kujua, wakienda EACJ watabwagwa wanaenda High Court ambao hawawezi kuingilia EACJ au Bunge kama ilivyoamuliwa na hukumu ya Komu(supra).
NIONAVYO:-
Waswahili wako sahihi walipolonga "mgema ukimsifia tembo hulitia maji" ndiyo hii kamati kuu ya cdm na wanasheria wake.
Hivi kweli Bunge litachaguaje wakati umelipa jina moja tu kwa kila nafasi? Kazi ya Bunge ni kuchagua siyo kupitisha matakwa ya vyama vya siasa.
Hivi, Chadema wana ajenda ipi kutoweka hata mwanamke mmoja au Mzenji katika mapendekezo yao ya hizo nafasi mbili za uwakilishi au chama chao sasa ni kama cha sisiemu wanaokazana kutaka kuwang'oa kwa kuzijenga koo za wanasiasa waliowahi kushika nyadhifa serikalini au ndani ya chama?