Kwanini CCM wanatuita SACCOS?

Kwanini CCM wanatuita SACCOS?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
Pamoja na kuwa ukweli ni mchungu ni lazima usemwe.

Ukweli huogofya na ndiyo maana wale wanaosubiri matunda bila ya kutaka kuwa sehemu ya kuyatafuta, hao ruksa kuingia mitini na hata kutoa povu kabisa.

Ukweli ni mchungu ndiyo maana walio waoga na wasio tayari kuzilipa gharama chungu za ukombozi, ni sahihi kuwahimiza kwa bidii kabisa, kukaa pembeni kwani kwa hakika hata mawazo yao hayahitajiki.

Ni heri kuwa na watu wachache waliodhamiria, kuliko kuwa na watu wengi mizigo.

Tafakari za kina za tulikotoka, tulipo na tunakokwenda haziwezi kuepukwa katika kufikia malengo ya wazi yaliyopo.

Kuna hili la kuitwa SACCOS. Hili si la kufumbia macho. Kuona kukosolewa kwake kwa marefu na mapana yake kunaweza kutuvusha.

Chama kinachopigania katiba ya wananchi kama agenda yake kuu ya sasa, hakiwezi kuwa baridi namna hii tangia Mbowe kushikiliwa.

Chama kinachopigania haki, uhuru na usawa hakiwezi kuwa baina ya vyama ambavyo havijatoa kauli yoyote hadharani ya mshikamano na askofu Mwingira.

Chama kinachopigania haki, uhuru, usawa na demokrasia hakiwezi kuwa hakijatoa kauli yoyote rasmi na hadharani ya mshikamano na mzee wa upako, askofu Shoo na hata Polepole.

Mbowe akiwa kizuizini na Lissu akiwa nje ya nchi ni wazi sasa kuwa kwa mustakabala wa harakati kuendelea, chama kinabidi kujitathmini kwa kina.

Siasa za ukombozi zina tija zaidi "on the ground" kuliko mitandaoni.

Wako wapi kina Heche, Kigaila, na kina Lwaitama?

Wako wapi kina Mdude?

Ziko wapi busara za kina Bagonza, Ulimwengu, Niwemugizi, Ponda, Mwamakula na wenzao?

Ifahamike, ukombozi hauwezi kuwa wito kwa kila mtu. Yaani hata J4?

__________
Uanaharakati ndiyo njia pekee ya kuipata katiba ya wananchi
 
Nchi hii wapinza wana matusi chama tawala nao vile vile tu tuna shida mahali na siasa zetu mambo yenye ayana maana yoyote upendwa sana kwenye hii nchi angalia mambo ya milinda nyeusi yame trend kuliko katiba mpya.
 
Shida CHADEMA inaongozwa zaidi na mtu binafsi badala ya taasisi.

Laiti ingekuwa ni taasisi hata in absence ya Mbowe na Lissu bado chama kingeongoza harakati ya kudai katiba mpya kwa ari ileile.

Na ndio maana Mbowe hataki kuachia Uenyekiti, maana the moment anaachia uongozi... That will mark the beginning of the end for CHADEMA.

Hurting truth.
 
Nchi hii wapinza wana matusi chama tawala nao vile vile tu tuna shida mahali na siasa zetu mambo yenye ayana maana yoyote upendwa sana kwenye hii nchi angalia mambo ya milinda nyeusi yame trend kuliko katiba mpya.

Ninakubaliana na wewe kwenye hili la kujikita kwenye hoja zisizokuwa na maana.

Uanaharakati ndiyo njia pekee ya kuipata katiba ya wananchi

Mengine ni mambo kama haya:

1. Minyukano ndani ya CCM haitusaidii kwenye madai yetu ya katiba mpya.
2. Mwendazake hayupo tena, makando kando yake tuhangaike nayo kwenye "haki na maridhiano" baada ya katiba mpya.
3. Agenda yetu ni ya kudumu si marafiki.
 
Kuna ukweli mchungu kwenye maoni yako.

Hata hivyo, ninadhani Chadema inapaswa kujiangalia na kurejea haraka kwenye reli:

Uanaharakati ndiyo njia pekee ya kuipata katiba ya wananchi

Tunataka katiba mpya na Chadema ndiyo iliyo katika nafasi zaidi ya kufanikisha hilo. Hata hivyo ni muhimu kutambua:

1. Minyukano ndani ya CCM haitusaidii kwenye madai yetu ya katiba mpya.
2. Mwendazake hayupo tena, makando kando yake tuhangaike nayo kwenye "haki na maridhiano" baada ya katiba mpya.
3. Agenda yetu ni ya kudumu si marafiki.
 
Katiba Mpya, Uongozi wa Kitasisi na Demokrasia ya kweli inapaswa kuanzia ndani ya CDM kabla ya kuhangaika na nchi.

Katiba mpya ya nchi ndiyo hitaji la msingi zaidi:

1. Kuna wasio na ajira kwenye katiba mpya tungependa ajira ziwe za muda usiozidi miaka 5 kote.

2. Kuna mambo ya uwazi angalia sasa hivi tozo za simu na miamala mrejesho uko wapi?

3. Dawa hospitali tunaambiwa matrilioni ya pesa yanalipwa lakini hakuna dawa mahospilalini.

4. Mihimili ya utawala kutokuwa huru kumeondoa imani ya kutegemea lolote la maana kwa mujibu wa sheria.

5. Kwamba hatuko sawa mbele ya sheria ni hatari mno kwa mustakabala wetu kama binadamu nk.

6. Msururu ni mrefu.
 
Yes IAM dude, so what's the fuckin problem you stupid dude?

Tuna haja kubwa na katiba mpya mkuu. Mengine ni kama ya Mirinda nyeusi tu mkuu, hayatusaidii.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Siku wakiubali huu ukweli watafanikiwa ila ndio hivyo tena🚶‍♂️

Tunakubali Chadema imepoa baada ya Mbowe kukamatwa.

Tunakubali bila kuwa na Mbowe pale juu labda ya TLP, NCCR na CUF yangeshajiri. Mola amjalie wepesi na maisha marefu Mh. Mbowe.

Tunaitisha kujitathmini kwa lengo la kurejea haraka sana kwenye reli:

Uanaharakati ndiyo njia pekee ya kuipata katiba ya wananchi

Tunataka katiba mpya.

Kama ilivyo kwa hoja za akina Mirinda nyeusi, tuna haya pia ya kuepuka:

1. Minyukano ndani ya CCM haitusaidii kwenye madai yetu ya katiba mpya.
2. Mwendazake hayupo tena, makando kando yake tuhangaike nayo kwenye "haki na maridhiano" baada ya katiba mpya.

Agenda yetu ni ya kudumu si marafiki.

Hadi hapo unasema bi dada? Bado hatuko pamoja kwenye kuijenga nchi yetu tukiwa kifua mbere?
 
Back
Top Bottom