Kwanini CCM ni tofauti na vyama vingine? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini CCM ni tofauti na vyama vingine?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 27, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  CCM ni tofauti sana na vyama vingine vya siasa nchini ambavyo vina usajili kamili chini ya sheria ya Vyama. Sifa pekee za CCM zinajidhihirisha wazi wazi katika masuala mazito ya kitaifa yafuatayo:-
  (1) Azma ya kuhakikisha kwamba Muungano wa Tanzania “na Mapinduzi ya Zanzibar vinaheshimiwa, vinalindwa na vinaendelezwa wakati wote.”,

  (2) Azma ya kuhakikisha kwamba ardhi inaendelea kuwa rasilimali kuu ya Taifa na inayoendelezwa kwa maslahi ya wananchi wote.

  (3) Azma ya kutaka kuona kwamba Tanzania ni Taifa lenye Umoja, Amani, Utulivu na Mshikamano madhubuti wa kitaifa wakati wote;

  (4) Azma ya kuhakikisha kwamba Utawala wa Sheria na Utawala Bora vinalindwa na kuendelezwa wakati wote;

  (5) Azma ya kuhakikisha kwamba Watanzania tunajenga maadili na demokrasia ya vyama vingi katika mazingira ya amani, yanayokataa siasa za uchochezi, uzushi, kashfa, uzandiki, uongo, ubaguzi wa rangi, ukabila, umajimbo na udini, mambo ambayo ni kinyume cha Haki za Binadamu.
  Wananchi kuichagua CCM maana yake ni kujihakikishia wao wenyewe kwamba wataendelea kula hayo matunda ya uhuru kwa ukamilifu.

  (toka Kanuni za Uteuzi wa CCM)
   
 2. The Spit

  The Spit JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  hiyo azma ya tatu ni amani katika msingi ghani wanaozungumzia kwa vile mi nijuavyo ni kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambazo ziko katika safu mbaya sana ya suala zima la amani.
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Duu?? Labda nina tatizo la kunagalia kinume nyume, mbona mambo yote matano ulo yataja nayaona kinyume nyume jinsi yanavo tekelezwa?
  mfano:
  1)'Mapinduzi ya Zanzibar vinaheshimiwa, vinalindwa na vinaendelezwa wakati wote' Hivi kuendelezwa kwake ndo mabavu mabavu hadi mauaji ya raia wasio kuwa na hatia? rejea mauji ya Pemba

  2)'ardhi inaendelea kuwa rasilimali kuu ya Taifa na inayoendelezwa kwa maslahi ya wananchi wote' Hii sijui hata nisemeje? Anzia wae wananchi wa Ihefu, wale wa Bulyankulu, achilia mbali wale wa GGM, tusisahu wale wananchi wanao fukuzwa kule karibia na kiwanda cha wazohill pia kama mnakumbuka tulisha ona picha humu JF za askari akimtandika mboko mama mmoja mkazi wa huko wazo walipokuwa wakijaribu kuandama kupinga kunyanganywa ardhi yao apewe muwekezaji, na sijui wale wahadzabe waliishia wapi? kwa hili nawapongeza kwa kuhakikisha wanahakikisha ardhi inakuwa mali ya muwekezaji !

  3) 'kwamba Tanzania ni Taifa lenye Umoja, Amani, Utulivu na Mshikamano madhubuti wa kitaifa wakati wote' Kwa kisingizio hiki hiki wezi na wahujumu uchumi wanapeta mitaani, eti wakiguswa nchi itayumba na amnai itatoweka? kwa kisingizio hiki hiki sheria zimekuwa zikipindishwa na kuweka double standards! Sijui ni amani kweli ama ni woga! Kisingizio cha amani na utulivu tumeshuhudia vijana wetu vyuoni wakipigwa marungu na FFU bila sababu za msingi,vyuo vikigeuzwa makambi ya jeshi! tumeona watu kama Zito kabwe wakinyima haki yao ya msingi kutoa mada mbali mbali kwa intelectuals.. FFU wanamwagwa mitaani hovyo wanapiga watu eti wanalinda amani na utulivu! Siamini hiyo kama ni amani bali ni kujenga taifa la waoga!

  4)'Utawala wa Sheria na Utawala Bora vinalindwa na kuendelezwa wakati wote' Rejea hapo juu, kwa mafisadi sheria zinapindishwa, mashitaka yanapelekwa mepesi, mfano Yona pamoja na wizi wa kiwira, anashitakiwa kwa kakosa kadogo tu.. mengine yote yanafunikwa, mramba pamoja na ten percent zote na kutaka tule nyasi mashitaka malaiiiini, chenge, na Rashid, tunaona wanavo peta mtaani hata hawaguswi! Mpaka system ikuteme ndo sheria inaonekana, lakini kama wewe ni ndani ya system wala sheria haikugusi!

  5) 'Azma ya...vyama vingi katika mazingira ya amani, yanayokataa siasa za uchochezi, ubaguzi wa rangi, ukabila, umajimbo na udini,......' Sijui hili CCM wamelitekeleza wapi? rejea walivo kibatiza CUF chama cha kidini, walivo eneza CHADEMA chama cha kichaga, rejea kauli za Sumaye ukitaka mambo yako yawe safi rudi CCM, rejea kudorola kwa maendeleo kwa kisiwa cha pemba, rejea kauli za Makamba TARIME, chagueni CCM ndipo mtaletewa maendeleo kwani ndiyo yenye pesa!, Oh, God bila kusahu wale wahanga wa kiteto.. picha zao tuliona humu ama kweli mazingira ya amani ya vyma vingi ccm imeyajenga!

  Nashangaa kwakweli kama sera zao ni nzuri namna hiyo ila wamejikita kuzitekeleza kinyume nyume, pengine ni mtazamo wangu lakini ndivyo niaonavyo, na laiti wangetekeleza haki bin haki ningekuwa wa kwanza kuipigia debe!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tofauti kubwa kati ya CCM na hivyo vyama vingine inajidhihirisha kwenye utekelezajiw a hayo malengo yao ambay yapo kanyaboya. Rwabugiri ameonyesha jinsi anavyoyaona malengo hayo kuwa yamekaa kinyumenyume, na hata mimi ninaamini hivyo.
  Hivi kuna watu wengi ambao hizo zilizoorodheshwa ndizo sababu zao za kuichagua CCM? Na ni kweli kuwa CCM inachaguliwa na watu wengi?
   
 5. J

  Jobo JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hivi mapinduzi ya Zanzibar ndo kitu gani? Kudanganyana kuwa Zanzibar haikuwa huru hadi Januari 12, 1964? Kwani wanadhani hatujui kuwa ASP kilishindwa kihalali katika uchaguzi halali na hivyo uhuru ukapatikana chini ya chama kingine? Kuenzi mapinduzi ni kama kuenzi jinsi Idd Amini alivyompindua Obote 1971!
   
 6. Giro

  Giro JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 360
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  No no no Mkuu,
  Nikijaribu kufikiria mambo hayo na CCM inavyo fanya kichwa kinaniuma.Nafikiri labda awameweka kama urembo tu kujifariji na kuwadanganya wadanganyika.
  Hiyo amani na mshikamano wanayo hubiri CCM ndio ile waliyoifanya kule Pemba/Unguja(2005),issue yao ya kumpakazia mwenzao(Salim Ahmed Salim) wameisahau,wanavyo vipakazia mbovu vyama vya CUF na Chadema? Makundi ndani ya chama chao hapo inakuwaje?.
  Hawa jamaa(CCM) ni wazushi,wababaishaji hawana sera zinazotekelezeka.
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  HIZO AZMA HAZIKO PRACTICAL JAMANI.unajua CCM inawezekana haikuwa mbaya BY THE TIME WANASET hizo azma,ila kwa sasa naona watendaji wakuu wa chama dio wanaoibua maswali mengi
   
 8. O

  Orkesumet Member

  #8
  Feb 27, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 75
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Ni ukweli usiopingika kabisa kwamba CCM imekuwa mstari wa mbele kueneza injili ya kuwa Tanzania inakuwa ni nchi ya amani na yenye kufuata utawala bora. Na hii imekuwa ikirithishwa kutoka awamu moja hadi nyingine. Ila ukifanya tafakari zaidi utaona kuwa nchi yetu ni amani kwa sababu za msingi tu zifuatazo (maoni yangu)
  1. watu walio wengi ambao wako kwenye kundi la rika lenye nguvu ya kufanya kazi hawajihusishi na siasa. Ni hili kundi lenye ufahamu mkubwa wa mwelekeo wa nchi kiuchumi, kijamii na kisiasa. Pia ni kundi ambalo lina uwezo wa kifedha
  2. ubinafsi v utaifa - walio wengi wametanguliza maslahi binafsi kabla ya maslahi ya taifa. Kuna mambo mengi tu ambayo yanahitaji nguvu ya umma lakini ni kawaida kusikia watu wakisema angalau watoto wangu wanapata mahitaji yao...au tumwachie amalize miaka kumi kisha tutachagua wengine
  3. chama v taifa - chama kweli kimeshika hatamu

  Kwa upande mwingine CCM imefanya vibaya kabisa katika utawala bora. Ni jambo lisilopingika kwamba "tone at the top" ya chama ndiyo chanzo cha uongozi mbovu katika nchi hii. Mambo ya utawala bora yamekuwa ni mambo ya kwenye karatasi na majukwaa ya kisiasa au kuridhisha wafadhili. Ni chama ambacho kimekuwa mstari wa mbele katika kugandamiza uhuru wa kutoa mawazo ndani ya chama. Sikushangaa pale BWM alipokosa tuzo ya utawala bora kwa viongozi wa afrika na si ajabu naye JMK akaikosa. Pia, tukiangalia upande wa vyama vingine, vingi kama si vyote vimekosa dira na vimeshindwa kufanya majukumu yake ya msingi ya kisiasa. Katika kufanikisha haya mambo mawili tuna safari ndefu!
   
 9. Giro

  Giro JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 360
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ukitaka AMANI siku zote kubali kudhulumiwa,na ukitaka UTULIVU siku zote kubali kuonewa hizo ndizo Formula.Otherwise patachimbika.
  Wa Tanzania tuna amani na utulivu kwa kuwa tu tumekubali hizo formula hapo juu kiasi kwamba tumekuwa wadanganyika kama sio majuha.Mfano mdogo tu Konda wa daladala jioni anakatisha ruti badala ya kwenda Mbezi naishia Ubungo rai wanakula kabunyau lazima amani na utulivu iwepo.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Je vyama vingine haviko hivyo au vina azma kinyume na hizo?
   
Loading...