kaijage kilembwe joshua
Member
- Oct 3, 2016
- 95
- 71
--------------------------------------
Kwa Mara ya Kwanza Vijana wa CCM Lumumba Wameungana na Vijana wenzao Makamanda wa Bilicanas kumtaka Kiongozi wa ACT WAZALENDO Zitto Kabwe ajitokeze hadharani kujibu upuuzi wa kinachoitwa tuhuma.
Vijana hawa hawafahamu kuwa Zitto ni Kiongozi Muadilifu na hawezi kujitokeza kujibu tuhuma zinazosukwa Lumumba na kuhaririwa Bilicanas zinazoongozwa na Chuki, wivu roho mbaya na kutojiamini? .
Vijana hawa pia wesahau kuwa Mafisadi wote wa taifa hili wanaotambuliwa na Dunia hii wamepatikana baada ya ripoti za uchunguzi zilizoasisiwa na taarifa ya CAG. ..
Kwa mifano michache
1. RICHMOND NA LOWASSA ilianzia na query kwa CAG then kamati ya Bunge ya Nishati Na Madini na baadae kamati ya mwakyembe kumwaga mambo hadharani.
2. ESCROW na kina Tibaijuka - uliibuliwa na CAG na baadae kamati ya PAC kumwaga mboga hadharani
3. Ufisadi wa EPA - ilianzia CAG iliyoipa kazi kampuni binafsi ya ukaguzi na baadae mambo yakawa hadharani.
4. Ufisadi wa KAGODA na DEEP GREEN - Imeanzia kwa CAG kama nyinginezo
4. Udisadi wa uuzwaji wa Mkataba tata wa shirika la UDA - halikadharika umeibuliwa na kwa CAG .
5. Kashfa ya iliyomng'oa waziri wa Fedha mkulo na wenzake nane 2012 ilianzia Kwa CAG.
Na nyingine nyingi waweza ongeza. ..
UNAJUA KWANINI?
Kwa sababu Ukaguzi wa mahesabu ni Taaluma sio kila mtu anaweza fanya.
Na Wataalam wa Dunia wamekubaliana kazi hiyo isimamiwe na taasisi huru ya CAG. ...
Na PAC aliyoiongoza Zitto hata hii ya Leo sio TAKUKURU wala POLISI wao wanakagua vitabu vya mahesabu vilivyokaguliwa tayari na CAG. ..
Leo Vijana mishipa ya shingo inawatoka wanataka Zitto awe fisadi. Eti alifumbia macho ufisadi wa NSSF alivyokuwa mwenyekiti PAC, hawajui hata kazi ya PAC wanaropoka tu.
Nani kawaambia PAC ni Mahakama?
Nawashauri tu Sasa kuwa hakuna haja ya kutengeneza Tuhuma Billicanas Kisha kuzihariri lumumba na kuzisambaza kwa nguvu kisa tu mnamchukia Zitto. ..
Kwa makamanda wa Billicana Inavyoonyesha mnatamani Sana kuirudia agenda ya kupambana na Ufisadi.
Bahati mbaya kamanda wa Anga aliipoteza alipokubali kumuuzia Chama FISADI ambaye ni mmoja Kati ya Mafisadi mashuhuli waliowahi andikwa na magazeti mnayoyatumia Leo kama reference, Magazeti ambayo Sasa hivi hayamuoni tena fisadi yanamsafisha . ..
Wekeni Ushahidi wa mamlaka zinazothibitisha Ufisadi wa Zitto Hadharani na mumkamate.
Na nyinyi CCM wenye polisi mnalalamika mitandaoni mnamuacha Fisadi Zitto anatembea barabarani? ?? Mkamateni mpelekeni mahakamani acheni kufanya cheap politics.
Kwenye hili Zitto mmemkosa mtafuteni kwengine
Ndimi
Habib Mchange