Kwanini CCM isifanyiwe reform ikiwa waasisi wake wana kubali imekosa maadili kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini CCM isifanyiwe reform ikiwa waasisi wake wana kubali imekosa maadili kitaifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Oct 27, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hali inayoendelea katika chaguzi za CCM ni ushahidi tosha kuwa sasa chama kimekosa dira na mwelekeo.Makada waaminifu kama mzee Kingunge amesema cha kimepoteza taswira na kuwa chama cha wenye pesa,Mh. Sumaye alisema chama hiki bila kutoa rushwa huwezi kupata uongozi na vijana nao wanatwangana viti na kutuhumiana kupokea rushwa.

  Kama madhumuni ya chama yamegeuka na chama kukubali kutumia nguvu kubwa ya kifedha ili kujikita kiuongozi tuna haja gani ya kuwa na chama kama hiki.Chama kimekuwa pango la wanyang'anyi kwa kupora rasilimali za taifa.

  Ukiangalia safu yake ya uongozi kuelekea uchaguzi wa 2015 napata wasiwasi kama lengo lao ni madaraka au kuna zaidi ya madaraka.Huwezi leo hii kumchagua mjumbe wa NEC ilihali kiongozi huyo na sifa za ujambazi kisha ukajinadi umejipanga kimkakati,wasiwasi wetu kama nchi inakabidhiwa kwa majambazi basi ujue wanyonge hawana pa kukimbilia.

  Kama kweli CCM inataka kusimama imara ni fursa muhimu kukifanyia reform ili kuwakimbiza wezi na mafisadi ambao wameifikisha nchi hapa tulipo.Hatuwezi kuwa na chama kinachowagawa Watanzania kwa misingi ya udini na ukabila tuka baki salama.Hta mwalimu aliwahi kusema dhambi hii ya ubaguzi tukiacha ikapita itatutafuna wote.CCM ya mwalimu ilijali maadili na heshima ya kuthamini utu wa mtu kinyume na CCM ya leo inayo uza utu wa mtu kwa kuwafukuza juu ya ardhi yao na kuwakabidhi wakoloni wa kigeni.

  Chama kinahitaji wa kina Kolimba ambao wanaweza kuwaeleza ukweli na kuwakosoa viongozi viwavi wa madaraka katika kutafuna keki ya taifa.Wananchi hatuwezi kufanya mbuzi wa kafara kila unapofika uchaguzi kwa kuhongwa ili kuuza utu na haki yetu kwa bei isiyotosha kununua hata pipi.Reformation kwa CCM ndiyo njia pekee ya kukinusuru angalu 2015 kiwekambi rasmi ya upinzani,vinginevyo kitapoteza hata hiyo nafasi ya upendeleo.
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kama unakumbuka Horace Kolimba ndiye aliyekuwa wa kwanza kusema hivyo hadharani kwenye mkutano wa Chama, labda unakumbuka vizuri kilichomkuta. Lakini unatakiwa kuangalia tena hali halisi ni nani wameshika hatamu na wanafanya kazi kwa ajili ya nani, anzia mjumbe wa nyumba 10, kwenda juu hadi ngazi ya taifa uone kama wanafanya kazini kwa ajili ya wakulima na wafanyakazi au kwa ajili yao wenyewe na maslahi yao. Ukiangalia hilo na muundo wa chama unaweza kuona kuwa kwa sasa mageuzi ndani ya CCM ni ndoto ya mchana. Kilichopo kama unataka kuwa kiongozi ni kujaribu kuogelea katika mazingira haya haya. 2015 kuna uwezekano kuwa CCM itaingia madarakani kuwa vyombo vyote vya usalama vitafanya kuhakikisha hilo hata CCM ikishindwa.
   
 3. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hawawezi kufanya reform kwa sababu wote wameoza,hakuna wa kumfunga mwenzie kengele,tutumie vizuri haki yetu kuwashikisha adabu. 2015
   
 4. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ukweli ndo huo,lakini Watanzania nao wafanye mabadiliko ya kweli kuliko kulalamika isipokuwa hatari nayoiona hapa kwa watawala hawa ni kwamba kuzidi kuwakanadamiza wananchi.Mfumo huu dume lazima wananchi wahakikishe wanauondoa na ikishindikana wakachachua na sisi ndiyo walalamikaji basi ni borfa kutumia nguvu ya umoja wetu wa kitaifa na kuingia barabarani.Tutakufa wachache kwa maslahi ya wengi.
   
 5. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  mkuu gamba limegomea kiunoni.
  2015 ndio watakuelewa
   
 6. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  WEWE ACHANENI NA UYO MSHAUR WA MAGAMBA, WATU AMEWAUDH NA WAMEMSUSA TANGU JANA POST 4 TU, AIBU, ILA NAKUJULISHA CCM ISHAKUFa HAKUNA REFORM APO, C UMEONA ATA JANA UVCCM WAKICHAPANA KWEUPe?
   
 7. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tatizo si kufa kwa CCM tatizo ni kufika 2015 tukiwa chini ya utawala ambao watanzania wanataabika bila kuwa na chembe ya unafuu wa maisha ndo maana tunahitaji dhamira ya kweli kuliko kusubiri wananchi waendelee kutaabika kisa tunaikosoa CCM
   
 8. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #8
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  The problem is....

  Who will bell the cat?
   
 9. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145

  wenye dhamira ya dhati ni wengi tatizo hakuna anayesikilizwa,maskini hawezi ongea mbele ya tajiri na chama kimekuwa cha matajiri
   
 10. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  tunasubiri masumbwi zaidi 2015
   
Loading...