Kwanini CCM Inatumia Matusi Sana Kwenye Kampeni Arumeru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini CCM Inatumia Matusi Sana Kwenye Kampeni Arumeru?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by MgungaMiba, Mar 15, 2012.

 1. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Tulizoea kuambiwa wapinzani hawana sera kazi yao ni kupinga kila kitu na kutukana, lakini safari hii inashangaza kuona CCM na umahiri wake wote imekuwa ndio kinara wa matusi! Mfano, uzinduzi wa Chadema tumemsikia Cmgn Manager Vincent Nyerere, Mgombea J Nassari, Mgeni Rasmi wakiongea kwa ufasaha mkubwa kiasi waliotoka uwanjani walikuwa wakijadili yaliyosemwa, lakini ilipofika zamu ya CCM kuzindua, do salalaa!

  Pandora Box la mitusi likafunguliwa, wapinzani wakaitwa Wapumbavu, wajinga, mabunzi, Vidubwana, hawana adabu, Mzee Mkapa na heshima zote alizonazo akajishusha hadhi, badala ya kumnadi mgombea, alitumia 80% ya hotuba yake kujitetea yeye, utadhani alikuwa mgombea, na kumtusi Vincent bila sababu.

  Hawakuishia hapo, huko vijijini ilikuwa balaa tupu, kwa mfano kule Msitu wa Mbogo, Mbuguni, yule Chalii Lusinde, Mzee Ole Sendeka nao wakafuata Nyayo za Mwigulu, walizungumzia nywele ziotazo sehemu za siri, huku wakishika maeneo yaotayo M*v*zi hayo na kufananisha na wapinzani, kinamama na watoto waliokuwepo walitaharuki na kujisikia vibaya, wakawaambia watu kuwa wasipoichagua CCM basi watatiwa Mimba, kwa ujumla hali ya hewa ilichafuka kwa matusi.

  Mgombea Bw Sioi nae akatoa yake, ingawa hakuongea kitu zaidi ya kusalimia tu, lakini hata kwenye hizo salaam pia alichemsha, kwani ingawa alikuwa kwenye kijiji cha Msitu wa Mbogo kilichopo kata ya Mbuguni, yeye alpaita kuwa ni Makiba! Watu walicheka sana kwani Makiba ni kata nyingine!

  Kwanini CCM inatumia matusi kiasi hiki wakati inayo mengi mazuri inayoweza kuyaelezea? Mbona kwenye kampeni ya Chadema na mgombea wake watu wanaongea vizuri, wanaelezea mtizamo na dhamira yao katika kuwania kiti hicho?
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ccm wamegundua dawa ya moto ni moto
   
 3. r

  rwazi JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama baba yao muuaji wa mwalimu domo limejaa matyusi wengine wafanyeje,laana ya mwalimu itawamaliza.
   
 4. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wana jf waswahili walisema debe tupu haliachi kuvuma , hao sisiem wameishiwa jamani hamlijui hilo , watawacheka.
   
 5. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Dawa ya moto upi?
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Bila shaka wanafata nyayo za mwingulu za ubakaji
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kuongea maneno hayo mbele ya watu wazima na watoto wa jinsia tofauti ni sawa na kuwavua nguo, wana Arumeru mfanyieni sioi kama warombo walivyomfanyia mramba
   
 8. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Jibu ni rahisi mtoa mada, hawana jipya la kuwavutia wananchi. Wanadhani kuchafuana ndio mtaji. Wewe huwaoni watetezi wao humu jukwaani wanavyotoka povu kwa kupaka matope. Badala ya kuzungumzia hoja za walipokuwa madarakani katika jimbo wamefanya nini, wamekwama wapi na wana mipango gani kuleta ufanisi zaidi wa hiyo mipango yao. Wao mtaji wao ni matusi tu. Wameathirika na "Zomeazomea syndrome"
   
 9. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwa hakika sasa nauona mwisho wa chama cha Mapinduzi, maana viongozi wake wamekosa uadilifu na busara kiasi cha kuanza kutoa matusi bila kujali kama kuna hadi watoto ambao wapo katika mikutano yao na wanasikiliza.
   
 10. k

  kitimtim JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Kimsing hawana tena la kuwaeleza watanzania wakawaelewa, mkapa kazindua kwa matusi, oooho vicent nyerere sio ndugu na nyerere..hivi kweli mtu mzima kama yule..akaongee maneno ya taarabu kiasi kile. Halafu ikimbukwe kwamba yeye mkapa ndio rais aliyefanya biashara binafsi kubwa pale ikulu;
  mkapa ndio alibinafsisha mashirika ya umma kwa mgongo wa nyuma; mtibwa sugar ana hisa nyingi balaa na shamba kubwa la miwa akajiuzia na kuleta taflani isiyo isha pale mtimbwa kati ya wakulima wa nje(yani watanzania wanaobangaiza na hilo shamba).

  Hela za epa pale benki kuu ya watanzania(bot)..hizi hela zilikuwepo miaka mingi tangu enzi za nyerere,mwinyi, ila kipndi cha huyu bwana kukalia kiti tu... Da..ndio zimesombwa hadi basi... Raia walipostukia ishu..balali(gavana) akapotezwa kwanza..halafu akina kagonda tukaambiwa wamiliki wake hawajulikani.

  Alivyo hana aibu mgodi wa kiwila ndio akajitwalia bila hiyana.....bila wabunge kukomaa.....na busara za pinda kuwaomba wabunge wasiendelee na inshu ya kiwira ya kwamba serikali imeambua kuutaifisha na kuurudisha...angekuwa pabaya sana huyu mzee

  alifanya madudu mzee huyu.... Basi tu...ilifikia mahali kikwete alipoingia tu madarakani...aliahidi kupitia mikataba yote aliyoingia huyu mzee.
  Sasa nashangaa sana badala ya kupumzika.....anaendelea kutukejeli na kutu enjoy wananchi...eti kuzindua kampeni..au kuzindua wizi mwingine
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mimi sioni ajabu kwa sababu, CCM hawana tena chakuwaambia wananchi uongo wote wamemaliza kilichobaki matusi. Viongozi ndio vinara wa matusi hukumsikia Nape akiwaambia wana Mwanza kuwa atawashikisha ukuta unafikiri hayo ni maneno mazuri, hukumsikia Mkapa juzi alivyoporomosha matusi.

  Wame waambukiza hadi mashabiki wao humu hoja za wafuasi wao ni za kulazimisha wakishindwa kwa hoja kutetea ufisadi na mafisadi wao wanakimbilia matusi au kubadili mada ni aibu tupu kweli. Lakini kadri siku zinavyokwenda ndivyo wananchi wanavyowaelewa vizuri kama hao kinamama sidhani kama wataendelea kuwa heshimu tena watu wa aina hiyo.
   
 12. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwa sababu ni watoto wa mbwa
   
 13. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hakuna sababu ya kuendelea kujadili matusi ya ccm. Kila mmoja aendelee kutoa elimu ili iwe rahisi kuwafungua watz kutoka katika vifungo vya ufisadi, wizi na ukandamizaji.

  Kuijadili ccm ni kuipa 'promo' isiyostahili.
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,775
  Trophy Points: 280
  Ukiona mtu anazungumza maswala yasiyohusu hoja husika ujue amezidiwa hoja.
  CCM wamepanic sasa matokeo yake wanaacha hoja za msingi na kuattack personality za watoa hoja.
  Kushinda kunapokaribia kushindwa wahusika hutamani ardhi ipasuke.
  Kuitetea CCM inahitaji uwe na akili ya maiti.
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hivi unapozindua kampeni kwa kuongea kuhusu meneja wa kampeni wa Chama pinzani maana Yale nini??
   
 16. m

  mang'ang'a JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Niliuliza asubuhi uzi wangu ukatoweka, kwa kuwa mkapa alifanya kazi na JK ORIGINAL muda mrefu na akawafahamu familia nzima, naamini alifanya kazi kwa muda mrefu na Mramba, Je? ashatambulishwa watoto wake wote??
   
 17. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  matusi kwenye kampeni hizo ni dalili za kufulia.kuhusu sioi kukosea hilo hana kosa sababu siyo mwenyeji wa huko na hiyo ni mara ya kwanza yeye anafika huko.wameru huu ni wakati wa kufanya maamuzi ya busara zaidi ya miaka 25 mmekuwa kwenye dimbwi la shida anzia kwa marehemu prof,major ndosi,marehemu sumari...semeni imetosha.kumbukeni lowasa aliukana umeru na akawatenda akiwa waziri wa maji
   
 18. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #18
  Mar 15, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  kumbe chadema ni moto eee!
   
Loading...