Kwanini CCM inashinda sana vijijini kuliko mjini?

Kwanini CCM inashinda sana vijijini kuliko mjini?

1. Upinzani wameweka nguvu nyingi mijini huku wakisahau vijijini. Tena kule ndko kura zinapopigwa vizuri.

2. Elimu elimu elimu

3. Media coverage
Kuna vijiji hata magazeti hawayajui. Tv wanaangaliaga tbc pekee. Unategemea nn apo.

4. Umri. Vijijini kuna idadi kubwa ya wazee kuliko vijana. Wazee hawana habari na mabadliko coz hawana maisha marefu. Vijana hawana utamaduni wa kupiga kura.

5. Wizi wizi wizi wa kura
Tatizo la upinzani kushindwa kufika mjini ni la kibajeti, hivi vyama havina fedha za kutosha ndio maana wanabaki mjini tu. Kama CCM yetu ambayo ni kongwe na inauwezo kifedha ilifikia mahali inashindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake kwa kukosa pesa, je hali ya kifedha itakuwaje kwa vyama vya upinzani?
 
Kama huiungi mkono US, Uingereza, China au taifa lolote lililo endelea unaweza usipate msaada kutoka kwao.
Ndugu zetu wengi vijijini kulingana na mazingira ya kiuchumi wanategenea misaada kutoka mjini. Sasa ili kuwaelimisha ni kuwapunguzia misaada na hata kuwanyima. Wakiuliza sababu ni kuwaambia mnaichagua Ccm na hali inakuwa mbaya hivyo uwezo wa kuwasaidia umepungua na ubaelejea Keisha kabisa.
Ni juu yao kuchagua kupewa kofia na kuichagua Ccm huku wakikosa msaada wa matibabu, elimu nk au kuikataa misaada ya kofia na kupata hivyo vingine.
Wakati mwingine people should learn the hard way
 
Elimu,elimu,elimu inawanyima elimu huko vijijini ili iendelee kuwatawala CCM imewekeza katika ujinga ndio maana inaendelea kukubalika vijijini
 
kijijini ukijifanya mpinzania unanyimwa pesa za tasaf
 
mjini wapi...hebu wekeni na takwimu za mijini nchi nzima kati ya ccm na upinzani nani anaongoza.....naona tunaanza kuwatukana watu wa vijijin kama vile na sis hatutokei huko.....
 
Ushindi wa Juzi wa udiwani huko Dar es Salaam, ni vijijini? Kwa watu wanao ona mbali, Uchaguzi wa juzi yaweza kuwa dira ya tunakoelekea kwa vyama vyote. Mwenye macho na aone, mwenye masikio asikie, asiyekuwa na vyote ahisi.

For now the pilot has already announced 80 Knots, and there is no enough runway for us to stop. In fact the useless thing is the runway behind us. We will use it next time when we land there in 2020. For now we are looking at the cruse speed.
Exceptions huwa hazikosi, na haita tokea siku Wapinzani waka shinda sehemu zote za jiji ila sehemu kubwa wamechukua wao.
Hata NY city ni democrats lakin wana chaguaga wabunge wa Republican kwenye baadhi ya sehemu.
Ki ujumla wapinzania sehemu za mijini hupambana sana kuliko vijijini.
Niko sahihi kabisa
 
CCM inashinda vijijini kwa sababu watu wa vijijini ukiwapa tu sembe wanasahau kila kitu. Mfano Idodomya.
 
W
1. Upinzani wameweka nguvu nyingi mijini huku wakisahau vijijini. Tena kule ndko kura zinapopigwa vizuri.

2. Elimu elimu elimu

3. Media coverage
Kuna vijiji hata magazeti hawayajui. Tv wanaangaliaga tbc pekee. Unategemea nn apo.

4. Umri. Vijijini kuna idadi kubwa ya wazee kuliko vijana. Wazee hawana habari na mabadliko coz hawana maisha marefu. Vijana hawana utamaduni wa kupiga kura.

5. Wizi wizi wizi wa kura
well said
 
Wahenga walisema kuuliza sio ujinga,wahenga walishasema huwezi kujua kila kitu,kwa hiyo naomba kuuliza swali ,na swali lenyewe liko hivi,je kwanini chama cha mapinduzi ccm huwa kinashinda sana chaguzi nyingi za vijijini kuliko chaguzi za mijini?

Asilimia kubwa ya watanzania wanaishi vijijini, asilimia kubwa ya watanzania ambao ni masikini wanaishi vijijini, asilimia kubwa ya watanzania wasiojua kusoma na kuandika wanaishi vijijini, asilimia kubwa ya watanzania wenye viwango vya chini vya elimu wanaishi vijijini, asilimia kubwa ya watanzania wasio kuwa na access na vyombo vya habari hasa national ones na internet wanaishi vijijini, asilimia kubwa ya watanzania wasio access national electric grid wanaishi vijijini.

Sources: Household budget surveys, National Panel surveys, national 2012 census reports, national health and demographic surveys tembelea www.nbs.go.tz

Mtazamo wangu 1. yawezekana wengi wa watanzania tegemezi wanaishi vijijini na kudhani kuwa wanaowategemea walio mijini ni matunda ya CCM hivyo ili waendelee kunufaika na utegemezi huo basi njia ya mkato ni kuendelea kuichagua CCM (rural-urban migration excluding factors such as education and marriage). 2. wapinzani wanapoongea kwenye public wanakuwa wanafoka au wenye hasira kali (kasoro Lowassa na Sumaye) hivyo watu hawapendi vurugu ndio maana wanaona bora zimwi likujuwalo kuliko lile lenye mwelekeo wa hatari kwa mitazamo yao.

Haya yote yanachangia watanzania wengi wa vijijini wasipate mwanga wa kuona njia sahihi ya kupata maisha bora.
 
Tuki weka pembeni sijui rushwa, tukiweka pembeni masuala ya umasikini au vijiji kutofikika tatizo kubwa ni

Kuna disconnection kati ya watu wa mjini na vijijini, yaani unakuta mtu wa kibaha mjini yuko connected zaid na mtu wa Dar au Mbeya au Iringa mjini lakini hajui kinacho endelea msoga. Vyama vya siasa navyo vinakosea hapo, angalia mwaka juzi kuna watu eti wana jiita wana chadema walikuwa wanasema hawajui nani kampigia kura magufuli, ndugu wapenda maendeleo na wapinzani nendeni vijijini, nendeni mka wasikilize wakati wa uchaguzi wana hitaji nini simamisheni wagombea wanao toka humo humo vijijini mkiweza, mwenye ndugu ukienda krismas sio unakula kuku tu, wasikilize wanakijiji wanapenda nini shida zao ni nini, ukienda kijijini ukawaambia tu elim elim elim siajabu hata hawatakuelewa ila ukitoa ahadi zinazonendana na mazingira uta weza, sasa jimbo la Isimani la Iringa eti una msimamisha Ole Sosopi ashindane na Lukuvi!!, shida ni kuwa makao makuu ya vyama yaliyoko mijini hayajui watu wa vjijini wana taka nini, na wana nchi walioko mijini hawako connected na wenzao wa vijijini kusikia wana shida gani na wa vijijini hawasikii ndugu zao wa mijini wana shida gani.
Tujirekebishe mabadiliko huanza na sisi

Napenda wanaosema ukweli.Unaumiza lakini ndiyo ukweli.Hongera.Vijijini pia hawaamui kwa kungalia mitandaoni mnaandika nini? hawana muda na maumivu wana muda wa kuvuna wanachopanda.Hawasubiri msaada wa Trump kuamua nani kashinda wanadhibiti wenyewe nani ashinde,
 
Asilimia kubwa ya watanzania wanaishi vijijini, asilimia kubwa ya watanzania ambao ni masikini wanaishi vijijini, asilimia kubwa ya watanzania wasiojua kusoma na kuandika wanaishi vijijini, asilimia kubwa ya watanzania wenye viwango vya chini vya elimu wanaishi vijijini, asilimia kubwa ya watanzania wasio kuwa na access na vyombo vya habari hasa national ones na internet wanaishi vijijini, asilimia kubwa ya watanzania wasio access national electric grid wanaishi vijijini.

Sources: Household budget surveys, National Panel surveys, national 2012 census reports, national health and demographic surveys tembelea www.nbs.go.tz

Mtazamo wangu 1. yawezekana wengi wa watanzania tegemezi wanaishi vijijini na kudhani kuwa wanaowategemea walio mijini ni matunda ya CCM hivyo ili waendelee kunufaika na utegemezi huo basi njia ya mkato ni kuendelea kuichagua CCM (rural-urban migration excluding factors such as education and marriage). 2. wapinzani wanapoongea kwenye public wanakuwa wanafoka au wenye hasira kali (kasoro Lowassa na Sumaye) hivyo watu hawapendi vurugu ndio maana wanaona bora zimwi likujuwalo kuliko lile lenye mwelekeo wa hatari kwa mitazamo yao.

Haya yote yanachangia watanzania wengi wa vijijini wasipate mwanga wa kuona njia sahihi ya kupata maisha bora.

Napishana na wewe uelewa kaika baadhi ya maeneo.Wasio jua kusoma na kuandika wengi wapo mjini si vijijini.Wasioweza kujitegemea bali kutegemea wengi wapo mijini,
Vijijini huchagua wanaye muamini hawachagui fedha za mtu.
 
Napenda wanaosema ukweli.Unaumiza lakini ndiyo ukweli.Hongera.Vijijini pia hawaamui kwa kungalia mitandaoni mnaandika nini? hawana muda na maumivu wana muda wa kuvuna wanachopanda.Hawasubiri msaada wa Trump kuamua nani kashinda wanadhibiti wenyewe nani ashinde,
Hahaha
Hii disconnection ipo dunua nzima
Hata USA watu wa mijini na vijijin huchagua vyama tofauti
 
Mfumo wa uchumi wa Tanzania uliwapoka wananchi vijijini nguvu zao kiuchumi tangu enzi ya chama kimoja kwa kisingizio cha kuweka "madaraka mikoani" kumbe ni janja ya chama kujitanua na kuwa na sauti ya mwisho hadi vijijini. Vyama vyao vya ushirika navyo vikajumuishwa kwenye mfumo wa chama kimoja; makada wakipewa uongozi. Kilichobakia ni wananchi wengi kuishi kwa kutegemea maamuzi na fadhila za viongozi wa kisiasa. Kuanzia uzalishaji wa kilimo, uamuzi kuhusu walimeje, mazao ya aina gani, wapateje pembejeo, wauzeje mazao yao, wapi na kwa bei ipi ni uamuzi wa makada wa kisiasa.

Wakulima waliojaribu kujitutumua kuongeza uzalishaji, hata kuchukua mikopo na kuajiri vibarua waliitwa makabaila wakadhibitiwa. Ukiongezea na kudumazwa kwa huduma za kijamii kama elimu, afya, maji safi, n.k. uwezo wa wananchi vijijini na kujiamini kulipotea kuliko mijini. Kwa kiingereza tunaweza sema wamekuwa "emasculated". Wanachojua ni mustakabali wao kutegemea serikali ya chama kilicho madarakani. Na chama hicho ni kimoja tu. Kuna utani wa kuwepo kwa wazee wanaofikiri hicho chama bado ni cha Nyerere. Ukiacha vijiji vichache vyenye wananchi wengi waliofanikiwa kujiendeleza zaidi kiuchumi, vingi mustakabali wao umeshikiliwa na chama. Wakijaribu kujitenga nacho mambo yanawaendea ovyo. Hivyo inabidi waendelee kukichagua angalau kuambulia chochote - TASAF, mbolea ya ruzuku, n.k.
 
Vijijini hakuna mafuriko-Wapinazni wanapenda mafuriko ya watu kwenye mikutano yao,ili wajipe moyo wanashinda.Kijijini huwezi kupata mafuriko ndio maana hawapendi kwenda.
Chopper hairuki kijiji kwa kijiji-Chopper zinazotumiwa na wapinzani zinatua wilayani tu,ambako watu wengi wanakuja kupata bahati ya kuona"hedikopta" na kuigusa,wakimaliza wanaacha kila kitu hipo.
Upinzani unahitaji kufanya maamuzi magumu sana ili kura zitoshe,sio kwa wasanii hawa tulionao
 
Mfumo wa uchumi wa Tanzania uliwapoka wananchi vijijini nguvu zao kiuchumi tangu enzi ya chama kimoja kwa kisingizio cha kuweka "madaraka mikoani" kumbe ni janja ya chama kujitanua na kuwa na sauti ya mwisho hadi vijijini. Vyama vyao vya ushirika navyo vikajumuishwa kwenye mfumo wa chama kimoja; makada wakipewa uongozi. Kilichobakia ni wananchi wengi kuishi kwa kutegemea maamuzi na fadhila za viongozi wa kisiasa. Kuanzia uzalishaji wa kilimo, uamuzi kuhusu walimeje, mazao ya aina gani, wapateje pembejeo, wauzeje mazao yao, wapi na kwa bei ipi ni uamuzi wa makada wa kisiasa.

Wakulima waliojaribu kujitutumua kuongeza uzalishaji, hata kuchukua mikopo na kuajiri vibarua waliitwa makabaila wakadhibitiwa. Ukiongezea na kudumazwa kwa huduma za kijamii kama elimu, afya, maji safi, n.k. uwezo wa wananchi vijijini na kujiamini kulipotea kuliko mijini. Kwa kiingereza tunaweza sema wamekuwa "emasculated". Wanachojua ni mustakabali wao kutegemea serikali ya chama kilicho madarakani. Na chama hicho ni kimoja tu. Kuna utani wa kuwepo kwa wazee wanaofikiri hicho chama bado ni cha Nyerere. Ukiacha vijiji vichache vyenye wananchi wengi waliofanikiwa kujiendeleza zaidi kiuchumi, vingi mustakabali wao umeshikiliwa na chama. Wakijaribu kujitenga nacho mambo yanawaendea ovyo. Hivyo inabidi waendelee kukichagua angalau kuambulia chochote - TASAF, mbolea ya ruzuku, n.k.

Wasomi wengi ninaowafahamu ni zao la kijijini.Wakifika mijini hujifanya vijijini hakuwahusu,huwalea watoto wao kimjinimjini.Watoto wa aina hii wakikosa ajira kama baba zao huanza kulalamika hatuna ajira. Wanalalamika kwa kuwa hawajafundishwa kufanya chochote nje ya ajira.Huamini kuwa jukumu la kuwafundisha cha kufanya nje ya Jira ni la serikali.Huamua kwa hisia siyo akili.Watoto wa kiume ( wengi wao) wa mijini huvaa heleni,milegezo huimba nyimbo za wageni wakidhani ni maendeleo.Wanapokutana na wa vijijini hushangaana.

Ukifika uchaguzi kuna Vyama hupeleka wa mjini ili wachaguliwe na vijijini,hukataliwa.Wanaanza kushangaa,"washamba hawa wamenikataaje"?Vijijni hutumia akili zao hawaigi ya wengine tu.Wasipokuamini hawakuchagui.Tunaochangia humu kwetu wapi? Baba yako na mama yako wamezaliwa na kukulia wapi? babu zako je?

Tembelea eneo lolote la Dar es salaam angalia maeneo wanayokula.Kagua maandalizi na aina ya vyakula,fuatilia vinywaji vyao na maeneo wanayokunywa.Sikiliza mazungumzo yao na aina ya lugha wanazozitumia.Fanya hivyo hivyo vijijini njoo na maoni yako utajua nani kaelimika.Kuna tofauti kati ya kusoma na kuelimika.
 
Napishana na wewe uelewa kaika baadhi ya maeneo.Wasio jua kusoma na kuandika wengi wapo mjini si vijijini.Wasioweza kujitegemea bali kutegemea wengi wapo mijini,
Vijijini huchagua wanaye muamini hawachagui fedha za mtu.

Lakini nimeweka sources, labda kama zina walakini kwa mtazamo wako.
 
Wahenga walisema kuuliza sio ujinga,wahenga walishasema huwezi kujua kila kitu,kwa hiyo naomba kuuliza swali ,na swali lenyewe liko hivi,je kwanini chama cha mapinduzi ccm huwa kinashinda sana chaguzi nyingi za vijijini kuliko chaguzi za mijini?
Huko hawashindi bali ndipo wanapoibia kura,vijijini hakuna vijana vijana wamekimbilia mijini.Hao wapiga kura wanatoka wapi?wazew idadi yao in ndogo
 
Back
Top Bottom