Kwanini binadamu tunaogopa KIFO?

Tuishi kwa amani,upendo na mshikamano tunapokuwepo hapa duniani;kifo ni hitimisho ya uwepo wako katika hii Dunia...tusidanganyike kwa kuamini ya kuwa tutazaliwa kwingine au tutaenda sehemu inayoitwa peponi...hiyo yote ni katika hali ya kujifariji ili kupunguza makali ya kifo.
 
Mkuu hata wanyama kifo wanakiogopa hivyo sidhani kama ni suala la kuogopa kwa ajiri ya dhambi.
 
Mimi binafsi sijawahi kuogopa kifo...ninachoogopa ni yale maumivu kabla ya kifo kutokea.
Namaanisha kuna vifo vinatokea baada ya kupata ajali, unakuta unavunjikavunjika, au unaungua au unakatika, au umekanyagwa au umeugua unateseka hadi kupelekea kifo kutokea.
Ingekuwa ndani ya mwili kuna batani ukipress unazima unajifia zako bila maumivu ingekuwa poa, tatizo la kifo mara nyingi kinaambatana na maumivu ndio kinatokea.
 
Katika jambo ambalo Mwenyezi Mungu ameliwekea sahau ni kifo. Hakisomesheki na hata ukieleweshwa utasahau tu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…