Kwa sababu haiwezekani
Hili ni wazo ambalo ukifikiri kwa hali ya kushidwa kweli utaliona huwezi na ni ngumu pia kutokea.
hakuna jambo ambalo limefanikiwa hapa duniani kwa kukosa utajiri wa kuwaza na kutafakari. lazima uwe na utajiri wakuwaza ndio upate kitu kipya
kwa nini ishidikane kutegeneza mwili wa mtu, hata ambao hauko hai??
Nasema hivyo nikiwa na mawazo chanya kabisa kwamba unaweza ukafata na kutegeneza kifaa kinacholingana na mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa lengo la kupata sehemu zuri yakupatia kiumbe.
kifaa hicho kishategenezwa tunafaata taaratibu za virutubisho vinavyotakiwa kupewa ili mashine ili itegeneza kiumbe,
kwa kuanzia unaweza ukatoa kiumbe ambacho kimekufa lakin kiwe na nyama na mifupa baadaye tutatafuta namna ya kuweka uhai.
Akili ya Mungu ni kama ya binadam kwa sababu alituumba kwa mfano wake.
mh hizi bangi mnazovuta sijui zinalimwa wapi?? au ndo zinatoka mapango ya amboni?? noooo itakuwa ni visiwa vya tanganyika na zimbabwe
Katika maswala ya uumbaji wa binadamu jinsi anavyoelezwa kwenye vitabu vya Mungu kwamba binadam aliumbwa kwa udongo hii hoja ni kweli kabisa.
Hii hoja ni sahihi kwa sababu ya kwamba mwili wa binadamu ni udongo kutokana vyakula na Oksijeni anavyotumia katika maisha yake inatokana na mimea ambayo maisha yake kwa asilimia kubwa inategemea udongo.
Kwahiyo; Ng'ombe, kuku, na wanyama wote wanaoliwa nyama zao ni udongo.
Kwa hiyo mmea umesimama kama mashine ya kuchota kile kinachofaa kwenye udongo na kukitegeneza ili kiweze kujenga na kutegeneza mwili wa binadam kwa taratibu maalum.
Wadau na Wanasayansi wa JF, Hivi ni kweli hakuna uwezekano wa kutengeneza mwili wa binadamu kwa kutumia virutubisho muhumu vinavyopatikana kwenye vyakula tunavyokula.
Mungu alituumba kwa mfano wake, why tusiweze kuuumba na sisi mwili wa binadamu?
Nawasilisha.
Miongoni mwa maswali ya kwanini ambayo yanachekesha ni kama yafuatayo:
Kwanini binadamu ana miguu miwili
Kwanini Mungu aonekani
Kwanini Binadamu wanakufa
Kwanini Mungu aliumba wanaume na wanawake
Kwanini damu ni nyekundu n.k
Jingine la kuchekesha ni hili hapa:
Kwanini binadamu hawezi kuumba mtu,
Jamvi haliishi vituko, hivi unafikiri kuna mtu atakayeweza kujibu hilo swali unaloliuliza? Kajipange bwana mdogo wa Shinyanga.
Mwanaume na mwanamke wakijamiiana siku ya mwanamke kushika ujauzito basi hapo ndipo binadamu anakamilisha uumbaji wa mwanadamu mwingine. Wewe unataka mwanadamu aumbwe kama production ya magari au soda kiwandani? Kwa maneno mengine ni kwamba kiwanda kiko kati ya mwanaume na mwanamke, na hasa nadhani kiwanda kiko ndani ya mwanamke, yaani womb.
Je, unafahamu kuwa energy tunayoipata na muhimu kwa binadamu inatokana na Jua, rejea biology yako ya o-level topic ya food chain utapata majibu.
Binadam ndiye anayeumba mwingine baada ya Mungu kuumba yule wa kwanza. Mwanaume alipewa uwezo wa uumbaji.Mbegu za mwanaaume ndio zenye uhai.