Kwanini binadamu anabadilika tabia?

Kwanini binadamu anabadilika tabia?

D_ullah

Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
43
Reaction score
62
Matokeo ya mwanadamu kubadilika tabia yanachagizwa sana na kitu gani?

Je ni anasikiliza na kuruhusu sana hisia zimtawale kutokana na matukio yanayompelekea abadili mtindo wake wa maisha (Tabia) kuliko kutumia akili katika kuchanganua yanamkabili?

Au

Ni matokeo ya uvumilivu na subira tunazoambiwa kuwa navyo pamoja na utulivu katika kila matukio iwe furaha au huzuni(maumivu)?

Ni nini kinachomfanya mtu fulani asibadilike na mwingine abadilike!? Hata wakipitia tukio moja?
 
Sijui sababu ila nadhan mazingira na circumstances zinazomzunguka.

Mwenyewe hapa nadhan niko katika mchakato wa kubadilika maana sio kwa kiminyo hiki cha maisha..

Kubadilika kuendea kuwa imara ili kufanikiwa au kutoka wema kwenye ubaya?
 
Tabia ya mwanadamu huchangiwa na sababu za kimazingira na kiikolojia. Sababu za kimazingira hutokana na aina ya makuzi aliyoambatana nayo katika maisha ya awali, hizi hujumuisha masuala ya imani za kidini, mila, desturi n.k.

Lakini sababu za kiikolojia huja baadaye baada mtu kusoma ama kuingia katika mikataba. Hizi humbadilisha kutokana na viapo, weledi, maarifa, maadili, n.k.
 
Kwa mtazamo wangu mimi, tabia nyingi watu wamerithi kwa wazazi yani ziko ndani ya damu, pia tabia za mtu zinatokana na mtu amesikia nini, ameona nini na anafanya au kufanyiwa nn mara kwa mara.. na kunatabia ziko ndani yamtu zimepooa sana uwezi zijua ila kuna hali au mazingira au vitu vinaweza kuboost hizo tabia zikaonekana kwahyo unaweza zani mtu kabadili tabia kumbe ilikua huko ndani imelala...
 
Tabia wanarithi kumbe...?
 
Back
Top Bottom