Kwanini Biashara Nyingi Zinakufa?

Kwanini Biashara Nyingi Zinakufa?

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,638
Reaction score
3,641
1*X73XAAvD0reuicB3ckc1tQ.png

hata ukiwa na bidhaa bora, biashara nyingi hufa mapema kwa sababu ya changamoto chache zinazojirudia mara kwa mara.
Changamoto hizi zimeua biashara nyingi Tanzania. Zinafanya watu wakate tamaa, wauze mali zao, na wengine hata waache kabisa ndoto zao za ujasiriamali. Hapa chini nimekuletea changamoto kuu tano na mbinu za kuzishinda ili usiishie kwenye orodha ya waliokufa kibiashara.

1. Mzunguko wa Fedha (Cash Flow)​

Fedha kwenye biashara yako ni kama damu kwenye mwili, ikikwama, maisha ya biashara yako nayo yanakwama. Wafanyabiashara wengi huchanganya matumizi binafsi na ya biashara, wanatoa fedha bila mpangilio, na mwisho wake mtaji unapotea kimya kimya.

Suluhisho:

  • Jilipe mshahara badala ya kuchukua pesa kiholela.
  • Hakikisha kila shilingi inayotoka inaleta nyingine kurudi.
  • Andaa bajeti na uifuate kwa nidhamu — discipline ya kifedha ndio msingi wa survival.

2. Masoko na Upatikanaji wa Wateja (Marketing & Customer Reach)​

Wengi huingia kwenye biashara kwa sababu “inasemekana inalipa.” Wanakimbilia kilimo au biashara ya bidhaa fulani bila kufanya market research. Matokeo? Wanavuna bidhaa nyingi lakini soko halipo — bei inaporomoka, hasara inakula mtaji.

Suluhisho:

  • Fanya utafiti wa soko kabla ya kuingia kwenye biashara yoyote.
  • Tambua ukubwa wa soko, wateja wako wapo wapi, na njia bora ya kuwafikia.
  • Usisite kubadilisha mbinu zako kadri hali ya soko inavyobadilika.

3. Huduma Mbovu kwa Wateja (Poor Customer Service)​

Biashara nyingi zinawekeza kwenye matangazo lakini zinasahau huduma bora. Mteja anapoingia, anakutana na usoni mkunje, majibu ya hasira, au huduma ya kusuasua — na hapo ndipo unapompoteza milele. Katika soko lenye ushindani mkubwa, customer experience ndiyo silaha kubwa ya ushindi.

Suluhisho:

  • Wekeza kwenye customer care training kwa wafanyakazi wako.
  • Hakikisha kila mfanyakazi anaelewa lengo kuu ni kutoa huduma bora.
  • Mteja aliyeridhika anakuwa balozi wako wa bure — atakuletea wengine bila kulipwa.

4. Ushindani (Competition)​

Kama huna ushindani, inawezekana biashara yako haina faida. Lakini tatizo ni hili: watu wengi wanashindwa kudumu kwa sababu ya price wars — kushusha bei kila mtu anavyoshusha hadi faida inakufa.

Suluhisho:

  • Usishindane kwa bei pekee — ongeza thamani (value proposition) inayokutofautisha.
  • Tafuta unique selling point (USP): kitu cha pekee kinachofanya biashara yako isimame tofauti na wengine.
  • Badala ya kuangalia washindani wako, lenga kuboresha biashara yako kila siku.

5. Wafanyakazi/Wasaidizi Wasiokuwa na Uaminifu (Unreliable Employees)​

Wafanyakazi ndio injini ya biashara. Bila wao, hutoweza kufanikisha mauzo, huduma, au uzalishaji. Changamoto kubwa mbili ni:

  • Kukosa commitment na bidii ya kazi.
  • Kukosa uaminifu — kuiba biashara au wateja.
Suluhisho:

  • Ajiri watu wanaopenda kile wanachofanya na wanaothamini ukuaji wa biashara.
  • Wape motisha na mafunzo ili waone thamani yao kwenye biashara.
  • Chunguza tabia za mfanyakazi kabla na baada ya kuajiri; ondoa changamoto mapema kabla haijaathiri biashara.
Changamoto hizi tano ndizo zilizozamisha ndoto za wajasiriamali wengi. Lakini sasa unazo silaha za kuzipiga vita: nidhamu ya kifedha, utafiti wa soko, huduma bora, ubunifu wa kipekee, na wafanyakazi waaminifu. Ukizimudu, biashara yako haitaishi tu bali itastawi na kukua.

Usiruhusu changamoto hizi zikumalize! Mimi na timu yangu tunaweza kukusaidia:

  • Kuchambua biashara yako (Business Audit)
  • Kukupa strategies za masoko na mauzo zinazofanya kazi
  • Kukuongoza kwenye management ya fedha na wafanyakazi
  • Kuongeza wateja kwenye biashara yako
Tuma WhatsApp sasa hivi 👉 +255693880325
 
  • Kuongeza wateja k
 
Back
Top Bottom