souljah meditater
JF-Expert Member
- Oct 15, 2012
- 2,146
- 2,104
IKIWA chumvi yote ya baharini ingetandazwa juu ya ardhi, ingefanyiza tabaka lenye unene wa meta zaidi ya 150, yaani, jengo lenye ghorofa 45 hivi!
Chumvi hiyo yote hutoka wapi, hasa tunapofikiria kwamba vijito na mito mingi sana humwaga maji yake yasiyo na chumvi baharini?
Wanasayansi wamegundua vyanzo kadhaa. Chanzo kimoja ni udongo na miamba.
Maji ya mvua yanapopenya kwenye udongo na miamba, hayo huyeyusha madini, kutia ndani chumvi na kemikali zake nyingine, na kuzimwaga baharini kupitia vijito na mito
(1). Bila shaka, kuna kiasi kidogo sana cha chumvi katika maji ya vijito na mito, kwa hiyo hatuwezi kuionja. Chanzo kingine ni madini yanayotokeza chumvi katika tabaka la juu la dunia lililo chini ya bahari. Maji hupenya kwenye mianya iliyo katika sakafu ya bahari, kisha yanapashwa joto kabisa, na kuja juu ya bahari yakiwa na madini yaliyoyeyuka. Matundu yanayotoa maji moto, ambayo mengine hufanyiza chemchemi za maji moto zilizo chini ya bahari, humwaga maji hayo yenye kemikali baharini
(2). Katika utaratibu mwingine unaofanana na huo, volkeno zilizo chini ya bahari hutokeza kiasi kikubwa cha miamba yenye moto baharini, na miamba hiyo hutokeza kemikali kwenye maji
(3). Chanzo kingine kinachotokeza madini ni upepo, ambao hupeperusha kemikali kutoka kwenye nchi kavu hadi baharini
(4). Mambo hayo yote hufanya maji ya baharini yawe na karibu madini yote yanayojulikana. Hata hivyo, kiasi kikubwa cha madini hayo ni sodiamu kloridi, yaani, chumvi ya kawaida. Chumvi hiyo hufanyiza asilimia 85 ya chumvi iliyoyeyushwa na hiyo ndiyo sababu maji ya baharini huwa na ladha ya chumvi.
Pia tunaweza kujiuliza kwa nini kiwango cha chumvi hakibadiliki? Ni wazi kuna chumvi nyingi baharini kwa sababu maji yanayovukizwa kutoka baharini ni safi. Madini hubaki baharini. Wakati huohuo, madini zaidi huendelea kuingia baharini; hata hivyo, kiwango cha chumvi hakibadiliki, kinabaki kikiwa asilimia 3.5 hivi.
Basi inaonekana kwamba chumvi na madini mengine huongezwa na kutolewa baharini kwa kiwango kilekile. Kwa hiyo swali linazuka, Chumvi hiyo huenda wapi? Chumvi nyingi hufyonzwa na viumbe hai.
Kwa mfano, chechevule wa tumbawe, moluska, na krasteshia hufyonza kalisi, ambayo ni sehemu fulani ya chumvi wanayotumia kujenga makombe na mifupa yao. Miani midogo sana inayoitwa diatoms hufyonza silika.
Bakteria na viumbe vingine hufyonza madini yaliyoyeyushwa na viumbe vingine. Viumbe hao wanapokufa au kuliwa, chumvi na madini yaliyo katika miili yao hatimaye hutua kwenye sakafu ya bahari kama mbolea au kinyesi
(5). Chumvi nyingi ambayo haiondolewi baharini kupitia njia zilizotajwa awali, huondolewa katika njia nyingine. Kwa mfano, huenda matope na vitu vingine kutoka nchi kavu, ambavyo hubebwa na mito, maji ya mvua, au majivu ya volkeno, vikashikamana na aina fulani za chumvi na kushuka kwenye sakafu ya bahari. Pia aina nyingine za chumvi hukwama kwenye miamba. Hivyo, kupitia njia mbalimbali, kiasi kikubwa cha chumvi huishia kwenye sakafu ya bahari
(6). Watafiti wengi wanaamini kwamba mzunguko huo wa chumvi na madini mengine kutoka nchi kavu hadi baharini na kurudi tena nchi kavu huchukua muda mrefu sana. Tabaka la juu la dunia limefanyizwa na miamba mikubwa sana. Baadhi ya miamba hiyo hukutana kwenye maeneo ya mshuko ambako mwamba mmoja huenda chini ya ule mwingine na kuzama kwenye tabaka la katikati lililo moto. K
wa kawaida, mwamba mzito zaidi huenda chini ya mwamba mwepesi, nao huzama pamoja na chumvi iliyo juu yake. Katika njia hiyo sehemu kubwa ya tabaka la juu la dunia hufanyizwa upya polepole
NB: Kama kuna mdau ana fact nyingine kuhusu bahari kuwa na chumvi anaweza akatujuza zaidi mshana jr Secret Star Heaven Sent