Kwanini bado mawaziri wapo ofisini ilhali bunge limevunjwa? Makatibu wakuu walipaswa kuendesha wizara wakati huu

Kwanini bado mawaziri wapo ofisini ilhali bunge limevunjwa? Makatibu wakuu walipaswa kuendesha wizara wakati huu

ngaiwoye

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
2,436
Reaction score
3,771
Leo katika pitapita zangu mitandaoni nimeona waziri Dakta Jafo amefanya uteuzi na amemteua Fred Vunjabei nikashangaa na kushtuka sana.

Tanzania Ili uwe waziri ni lazima uwe mbunge (mhimili mwingine). Kwa Sasa bunge hilo lilishavunjwa, je uhalali wa kuendelea kuwa mawaziri na kutoa amri na kufanya teuzi unatoka wapi? Tena mawaziri wengine wapo kwenye mbio za kuwania ubunge huko majimboni, je kwa nafasi hizo haionwi kwamba wanaweza kutumia nafasi hiyo kujipendelea huko majimboni?

Na ni kwanini tunaachia katiba inaendelea kujikanganya kwa kuchanganya mihimili inayojitegemea..Yani serikali ni mhimili unaojitegemea, bunge linajitegemea na mahakama inajitegemea, unamfanya mbunge anakuwa waziri..Sasa hiyo mihimili itajitegemeaje??

Maoni yangu ni kwamba hata hafla ya Rais pale ikulu ya uapisho wa viongozi kama wakuu wa mikoa , mabalozi na kadhalika haitakiwi jaji mkuu wala spika kupewa nafas ya kutoa nasaha kabisa, ushirikiano hapana Ili mihimili ijitegemee. Haitakiwi kushirikiana...hayo ni maoni tuu

SWALI langu: kwanini makatibu wakuu wa wizara ambao kimsingi ni watendaji wakuu wa hizo wizara kwa Sasa wasiendeshe hizo wizara Ili kutuondolea taharuki sisi watanzania ambao tuna vishauku vya kujua mambo.

NB: Ikiwa Kuna SHERIA inaowaruhusu kuendeleza KUKAA kwenye hizo ofisini wakati kikatiba Ili uwe waziri lazima uwe mbunge na bunge limeshavunjwa basi SHERIA hiyo ibadilishwe MAANA kikatiba hawawezi kuwa na uhalali wa kuendelea kuwa mawaziri
 
Huu upuuzi aliufanya Kikwete kufanya mabadiliko madogo ya Katiba kuwafanya mawaziri kuendelea kuwa Mawaziri wakati kimsingi kikatiba huwezi kuwa Waziri bila kuwa mbunge. Na bunge likivunjwa maana yake na uwaziri wako ndo basi.

Kipindi cha Mkapa, Mwinyi na Nyerere kipindi hiki Taifa lilikuwaga na utulivu sana maana nchi ilikuwa inaongozwa na Makatibu Wakuu
 
Leo katika pitapita zangu mitandaoni nimeona waziri Dakta Jafo amefanya uteuzi na amemteua Fred Vunjabei nikashangaa na kushtuka sana.

Tanzania Ili uwe waziri ni lazima uwe mbunge (mhimili mwingine). Kwa Sasa bunge hilo lilishavunjwa, je uhalali wa kuendelea kuwa mawaziri na kutoa amri na kufanya teuzi unatoka wapi? Tena mawaziri wengine wapo kwenye mbio za kuwania ubunge huko majimboni, je kwa nafasi hizo haionwi kwamba wanaweza kutumia nafasi hiyo kujipendelea huko majimboni?

Na ni kwanini tunaachia katiba inaendelea kujikanganya kwa kuchanganya mihimili inayojitegemea..Yani serikali ni mhimili unaojitegemea, bunge linajitegemea na mahakama inajitegemea, unamfanya mbunge anakuwa waziri..Sasa hiyo mihimili itajitegemeaje??

Maoni yangu ni kwamba hata hafla ya Rais pale ikulu ya uapisho haitakiwi jaji mkuu wala spika kupewa nafas ya kutoa nasaha kabisa, ushirikiano hapana Ili mihimili ijitegemee. Haitakiwi kushirikiana...hayo ni maoni tuu

SWALI langu: kwanini makatibu wakuu wa wizara ambao kimsingi ni watendaji wakuu wa hizo wizara kwa Sasa wasiendeshe hizo wizara Ili kutuonfolea taharuki sisi watanzania ambao tuna vishauku vya kujua mambo.

NB: Ikiwa Kuna SHERIA inaowaruhusu kuendeleza KUKAA kwenye hizo ofisini wakati kikatiba Ili uwe waziri lazima uwe mbunge basi SHERIA hiyo ibadilishwe

Sawa kabisa mkuu,ila kwa ccm hii imeharibu hii nchi kuanzia mwanzo mpaka mwisho
 
Mkuu katiba inawawaweka madarakani ijapokua bunge limevunjwa!
Mbaya zaidi hata Leo rais anaweza kuteua mtu ambaye aliwahi kuwa mbunge kuwa waziri! Yaani kutoka bunge lililovunjwa!

Katiba yetu ina utata sans.
 
Katiba inajikanganya sana. Wasomi wa nchi hii wanatuangusha sana. Wanashindwa kushauri vitu wazi kabisa
 
Na wanalipwa mshahara isivyo halali, hii ni matumizi mabaya ya ofisi kwa mwajiri wao na ni ufisadi kuendelea kuwalipa kwani waziri nilazima awe mbunge...
Hii nchi tunafata katiba au kichwa cha mtu
 
Back
Top Bottom