Costa concodia
JF-Expert Member
- Jun 12, 2014
- 209
- 48
ndivyo haswa wote tunatakiwa kuwa hivyo sio unapanda daladala by the time unashuka kila mtu anajua majina yako matatu na wapi unafanya kazi na mkeo alikusaliti na unaumwa kisukari.....what for?
ofisin kuna majungu sana so bora mtu ajifiche fiche...mtu anadanganya kabila ili likizo alipwe hela ndefu,au mtu anatumia cheti cha ndugu yake....sasa huoni why ana umuhimu wa kujicha ficha?Mkuu si huko kwenye sehemu za kukutana kwa mara moja, yaani unafanya kazi au unasoma na mtu wa namna hiyo.
Kuna watu wanapenda privacy. Ni muhimu kuheshimu utashi wa kila mmoja. Kuna watu wako nosy, ukimuambia kitu kimoja anakuganda na maswali kama mia
Hao watu nnaowaelezea hapa wana maswali kama unavyosema, wanapenda privacy ila uzuri wao huwa hawasemi kile ulichowaambia, halafu huwa wanakuwa kama watu wasiowaamini sana wenzao.
Yeah, hiyo tabia naipenda japo sipo hivyo. Wapo watu mnakutana, ndani ya nusu saa umefahamu kila kitu kuhusu yeye na maisha yake. That's just not right, hii nchi ishaharibika, sio vizuri kuji-expose kwa watu usiowajua.
Thats how it should be, sio kila mtu anatakiwa kujua kitu hata kama mna ukaribu sana.
Usiwafosi wakupe siri zao! Tulianao kwa upendo hawatakuangusha hata siku moja!
Phlegmatic upo?
yeah, wapo kama mashushushu hivi, wanapenda kufuatilia details za wengine ila habari zao hutakaa kuzisikia. Uzuri wa wengi wa hivyo, hawatoi siri za watu ovyo, coz wao ni wasikilizaji wazuri lakini sio waongeaji.Eli79 watu wa hivyo nnavyowajua mimi wanapenda kujua mambo ya watu bila wao kujulikana, anaweza kukuuliza maswali kuhusu mtu fulani ukimuuliza kwanini unauliza hivyo anaweza kukujibu kuwa "....namfananisha na mtu fulani" baada ya hapo anakuwa kimya.