Kwanini baada ya …… ndo tunakumbuka kupima vvu/hiv?

Kwanini baada ya …… ndo tunakumbuka kupima vvu/hiv?

KITAULO

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2018
Posts
1,926
Reaction score
2,843
Naomba kuwakilisha kwa wadau,

Kuna la kujifunza kutokana na mazoeya/mwenendo mbaya miongoni mwetu sisi vijana(kwa vijana wa jinsia zote mbili).Kumekuwa na kasumba kwa vijana kupimana afya kwa kuangalia hali ya afya ya mtu kwa macho au mwonekano wake.Hii imepelekea vilio na majuto kwa wengi miongoni wetu hususani tunapokuja kugundua kwamba macho yetu yametulaghai (unwanted pregnancy and tested HIV +)

Tabia ya kushiriki kwichikwichi/zinaa/mapenzi au mahusiano ya kimwili na mtu msiyefahamiana (Crush) au kwa wale wenzangu na mimi kula tunda kimasihara.Baada ya tendo watu ndo wanakumbuka kwenda kupima roho zikIwa juu juu.Tabia hii imekuwa kama fashion miongoni mwetu sisi vijana.



Kwa uchunguzi mdogo nilioufanya kupitia machapisho mbali mbali ya mahusiano kwenye hii platform JF hususani ule uzi wetu pendwa “umeshawahi kula tunda kimasihara” by His Excellence Rikiboy…Vijana wengi wamekuwa wakiweka wazi experience zao za kimapenza na jinsi walivyoshiriki mahusiano ya kimwili (pasipo kuchukua tahadhari yoyote) na baadae kwenda kupima.Tena kushiriki bila kutumia vitendea kazi vilivyoshauriwa na wataalamu wetu wa afya ya uzazi eg Condom.

Napenda kutoa rai yangu kuwa vijana tuwe makini,na tutambue wazi kwamba mwenye ngoma hauwezi kumtambua mtu kwa kumtazama kwa mach😵nce unapokuwa mpigaji matumizi ya mipira iwe ndo sera yako na kama hauwezi kucheki afya iwe ndo slogan yako.

Ukiwa mpigaji you have to live by two principles.

1st Use condom all the time

2nd check your healthy status before engaging in unsafe sex.




AIDS is there and it kills.
 
Back
Top Bottom