Kwanini baada ya kuoana tumeachana?

Hivi humu mnajua ndoa za aina ngapi? Kuishi na MTU miezi sita tuu ni ndoa sasa msije kuleta ndoa juu ya ndoa hapo ndipo tatizo linapoanzia
 
The thing is mmekaa kwamuda huo bila kufunga ndoa na nakuomba tu ufanye uchunguzi kwani haya mahusiano yapo sana,lakini baada tu ya kufunga ndoa mambo yanakuwa mengine

Kwanini?

Hilo ndilo swali la msingi!

Inategemea ni kwa nini muda wote huo hawakufunga ndoa,Kama tatizo lilikuwa ni la nje(mfano wazazi walikuwa hawataki baadae wakawaruhusu)inawezekana hiyo ndoa kudumu.

Pia kama taratibu za kuunganisha mahusiaon zilifanyika mahari ilitolewa wazazi wakabariki mkaishi bila ndoa ya karatasi hata mtakapoamua kuwa na karatasi mtadumu.

lakini kama tatizo ni kukosekana kwa utayari wa kufunga ndoa kati ya wapenzi hao wawili,pamoja na kuishi miaka mingi na kuzaa watoto hiyo ndoa ikifungwa kuna uwezekano mkubwa ikafa.kabla ya ndoa yule asiyekuwa na utayari wa ndoa anafikiri muda wowote anaweza akaondoka kwenye hayo mahusiano,anaweza akamfanyia chochote mwenzie bila kujali maumivu yake, na mwenye utayari ni rahisi kuvumilia hasa kama wamesha zaa. baada ya ndoa yule aliyekuwa na utayari wa ndoa atakuwa na matumaini ya kuwa mwenza wake atam-treat vizuri kwakuwa ameji-commite kwenye ndoa inapokuwa tofauti ni ngumu kuvumilia tena.Na wengine wapo kulipa visasi.

Kuna binti alipobeba mimba boyfriend alimnanga sana kuwa amemtega na hawezi kuwa na mke kama yule,baada ya ushauri wa marafiki na ndugu boyfriend akaamua kuishi na binti wakazaa na mtoto wa pili wakaishi maiaka4,mume akaokoka akaamua afunge ndoa na mkewe,ndoa imefungwa tu usiku mke akamkumbusha mume alivyomnanga na akamwambia alikaa nae ili alipe kisasi, toka siku hiyo amani ikatoweka mke hana muda na mume,akatafuta uhamisho kazini kwenda mkoa mwingine ili awe mbali na mumewe huu mwaka wa pili,mke hajishughulishi na chochote cha mumewe,mume aliwahi kumfuata kuona watoto akaambiwa akitaka kuongea na watoto zaidi ya siku moja akakae hotelini asubuhi anawachukua jioni anawarudisha.

Pia ukifuatilia sana hayo mahusiano ya miaka 8 bila ndoa bila sababu ya maana na watoto mnazaa hamna furaha/amani ya kweli, kuna mmoja anaumia na kuvumilia sana.
 

Naweza Kuwa Mimi Kweli Ni "Bogasi"

Lakini Ukweli Ni Kwamba Uko So Boring.
 
Kwanini watu wa aina hii huwa ni wakristo tu?

Yani mnawekana kinyumba kama baba na mama huku hamjawa verified, inatokea mara nyingi kwa dini hii tu,

Nani kahalisha huu utamaduni?

Excel hata Waislam baadhi ya vijana wanafanya hivyo haswa vijana wanaoishi mijini
 
Rafiki yetu alikuwa na mpenzi wake kwa muda mrefu tuu! akawa anamwona kama mtoto mtoto hajakua akaamua kupata mwanamke mwingine alikuwa anajifake kupita maelezo mahusiano yakafikia mpaka ndoa .
Wamekaa miezi tisa migogoro ikaanza mwanamke ni mtu wa kaskazini huko anataka kumcontroll mwanaume mpaka anamchagulia marafiki jamaa kahama nyumba kapanga ni mwaka tuu ndoa yao imedumu. sasa ni nini hiki?
 

it should be noted that winning arguments in marriage is not the sole goal that brought the two together

yeah arguments exist now and then just to prove that the relationship is strong enough to survive

if there is a misunderstanding should be fixed up and not just raising arguments unnecesserily

no one in this world is perfect but one can learn to live with imperfect person and will finally become they way you want

it just requires patiency if one thinks well right!
 

Natamanile kizungu maayo ...!!
 
^^
Kuna tofauti ya maisha kabla ya ndoa, ndani, na baada ya ndoa. Kabla ya ndoa ni kukubaliana ili usipoteze penzi, ndani ya ndoa ni sheria, na baada ya ndoa ni kanuni ya majuto na lawama.
^^

Ni kweli kabisa!!I hand you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…