Kwanini awamu ya tano wanatudanganya SGR ni mwendo kasi wakati ni mwendo wa wastani?

Mkuu hata ingekuwa ya kasi unayoitaka wewe lazima ungetafuta kasoro ingine...hater is hater hana jina lingine litakalomfaa,la msingi hapa ni kuea hii reli tumeijenga wenyewe kwa fedha zetu za ndani na ndio reli ya kwanza kujenga wenyewe baada ya ile ya kati ya wakoloni..
 
What about quality? Na yenyewe ni bora kuliko ya wakenya?
 
Naamini uzi huu utasomwa na wahusika wa mradi huu kuanzia TRL yenyewe na wizara ya Miundombinu.... Nitumie fursa hii iliyotolewa na mtoa hoja kuhoji maandalizi ya ujenzi wa reli yetu mpya nikijikita zaidi kwenye uchafuzi wa mazingira.

Treni zinazotoa huduma kwenye reli ya kati hata zile za TAZARA zimetengenezwa kwa mtindo unaoruhusu wasafiri kujisaidia juu ya reli huko maporini treni ikiwa kwenye mwendo na kukataza kutumia vyoo vya treni pale inaposimama vituoni. Imekuwa hivyo miaka yote na naamini hadi leo hali ni hiyo.

Ujenzi wa reli hii mpya na miundombinu ya mabehewa na injini zitakazotumika, vitazingatia suala la usafi wa mazingira kwa kutumia vyoo kama vile vinavyotumika kwenye ndege au watu wataendelea kutupa vinyesi kwenye reli?. Ningependa sana kujua changamoto hii wataitatuaje.
 
Hilo haliwezekani hata kwa dawa kwa ujenzi unavyoendelea labda itakamilika 2020 mwishoni
 
Mimi nasubiri hii treni ya mwendokasi itakayotumia saa moja unusu kufika morogoro inaanza lini kazi na tiketi zinapatikana wapi, haya maneno mengine naona kama ni blah blah tu..
 
Shida hakuna Hela jiwe analipuka tu
 
SGR ya Kenya inatumia Mafuta only wakati SGR ya Tanzania itakuwa inatumia Umeme kwa kias kikubwa na mafuta kwa emergence tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…