Si lazima.Watoto ni majaliwa ya MunguWanandoa wameoana na wamefanikiwa kuwa na watoto wote wa kiume ama watoto wote wa kike. Inatokea kwamba wanandoa kuona familia yao hajakamilika pasipokuwa na watoto wa jinsia tofauti yaani wa kike na wa kiume. Na huendelea kuzaa pasipo mafanikio na kujikuta na lundo la watoto na wanazidiwa uwezo wa kuwatunza. SWALI: Je ni lazima kuwa na watoto wa jinsia tofauti kwenye familia? ama si lazima?
Wengine na familia nazo zinachangia, kwa mfano baba katoka katika familia ambayo ina watoto wa kiume tu either atapendelea kupata mtoto wa kike au wa kiume, na inavyokuwa tofauti na matarajio yake ndio matatizo yanaanza.Hii inawasumbua wengi jamani yaani mkiwa na wa kike baba haridhiki anataka mpate japo wa kiume au mkiwa na wa kiume mama haridhiki anataka japo apate 1 wa kike duh tutafika kweli
kwenye kadamnasi unaweza ukasema mtoto ni mtoto,lakini deep down unakuwa unapenda upate watoto wa jinsia tofauti
kwenye kadamnasi unaweza ukasema mtoto ni mtoto,lakini deep down unakuwa unapenda upate watoto wa jinsia tofauti
Nakumbuka kuna jamaa yangu mmoja alikuwa anajigamba bado kuna dume la ng'ombe linakuja kama bile ana makubaliano na muumba baada ya kupata wa kike wawili. Mimba iliyofuata akadai akipata wa kiume basi ndiyo kamaliza kazi akawa wa kike mwingine. Akaendelea kujaribisha dume la ng'ombe, kuja kushtuka ana mabinti sita.